Wednesday, 25 January 2017

MADC WATEMBELEA SHAMBA LA JARIBIO LA MAHINDI LA KITUO CHA MAKUTUPORA


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, Profesa Faustine (kushoto), akizungumza na wakuu wa wilaya za Dodoma na maofisa watendaji na wenyeviti wa serikali za mitaa na wadau wa kilimo alipotembelea shamba la Jaribio la Mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) chini ya Mradi wa Mahindi Yanayostahimili Ukame (WEMA) katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mkoani Dodoma leo.



Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye mkutano na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, Profesa Faustine (hayupo pichani), walipotembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mkoani Dodoma leo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembi, Bahi, Elizabeth Kitundu, Mpwapwa Jabir Shekimweri na Mshauri wa Kilimo Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Aziza Mumba.



Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Hussein Mansour akizungumza (kushoto), akiwaelekeza jambo Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Dodoma walipotembelea shamba la Jaribio la Mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) chini ya Mradi wa Mahindi Yanayostahimili Ukame (WEMA) katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mkoani Dodoma leo. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Elizabeth Kitundu, Kongwa, Deogratius Ndejembi, Mpwapwa, Jabir Shekimweri na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, Profesa Faustine Kamuzora.







Wanahabari, watafiti wa kilimo, wenyeviti wa serikali za mitaa na watendaji wakiwa kwenye mkutano kabla ya kutembea shamba hilo la jaribio la mahindi.



Wanahabari, watafiti wa kilimo, wenyeviti wa serikali za mitaa na watendaji wakiwa nje ya lango kuu la kuingia katika shamba hilo wakisubiri kupewa taratibu za kuingia.



Mshauri wa Mradi wa Mahindi Yanayostahimili Ukame (Wema), Dk.Alois Kullaya (kulia), akitoa maelezo kabla ya kuingia kwenye shamba hilo la jaribio la mahindi.





Mtafiti wa Kituo hicho,Ismail Ngolinda (kulia), akitoa maelekezo kuhusu shamba hilo. 






Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange (kushoto), akizungumza na viongozi mbalimbali baada ya kutembelea shamba hilo. Kutoka kulia ni Mshauri wa Mradi wa Mahindi Yanayostahimili Ukame (Wema), Dk.Alois Kullaya, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, Profesa Faustine, Kaimu Mkurugenzi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Richard Muyungi, Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Hussein Mansour na Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kati Dodoma, Dk. Leon Mroso. 










Mshauri wa Mradi wa Mahindi Yanayostahimili Ukame (Wema), Dk.Alois Kullaya, akielekeza kuhusu mahindi hayo ya jaribio hilo.



Picha ya Pamoja. 



Na Dotto Mwaibale, Dodoma

KATIBU Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, Profesa Faustine Kamuzora amesema utafiti wa kilimo ni muhimu ili kuongeza chakula nchini.


Kamuzora alitoa kauli hiyo alipotembelea shamba la Jaribio la Mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) chini ya Mradi wa Mahindi Yanayostahimili Ukame (WEMA) katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mkoani Dodoma leo.


Alisema bila ya kuwepo kwa utafiti wa kilimo hatuwezi kufikia ufanisi wa kupata chakula kingi hivyo matokeo mazuri ya utafiti ni muhimu kwa maendeleo ya kilimo.


Alisema majaribio ya kisayansi ni muhimu na ni mkombozi kwa mkulima hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya tabia nchi na ukame.


Katika hatua nyingine Kamuzora aliwataka wakuu wa wilaya na watendaji na wenyeviti wa serikali za mitaa wa mkoa wa Dodoma waliotembelea shamba hilo kuwa mabalozi kwa wananchi wao kwa kile walichokiona kwenye shamba hilo la majaribio. 


Aliomba kuwepo na subira wakati utafiti huo ukiendelea na kusubiri kuthibitishwa na vyombo vyenye dhamana na kama wataona unafaa basi utatumika.


" Utafiti haufanywi kwa siku moja na kuanza kutumika una mlolongo mrefu ili kutoa nafasi kwa vyombo husika kuona kama upo salama na kuruhusu kutumika" alisema Kamuzora


Alisema vyombo vyenye dhamana vikiridhika vitatoa kibali cha kuanza utumiaji wa teknolojia hii mpya licha ya nchi nyingine za wenzetu kuanza kuitumia,” alisema.


Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembi alisema ni muhimu sasa kuharakisha matumizi ya teknolojia hiyo badala ya kupoteza muda mwingi ukizingatia kuwa hivi sasa nchi inakabiliwa na ukame hasa katika wilaya yake.


"Kazi inayofanywa na watafiti wetu ni nzuri ila nawashauri wafanye utafiti utakaosaidia katika kipindi hiki cha mabadiliko ya tabia nchi yaliyopo maeneo mbalimbali.


Mkuu wa Wilaya ya Mpwawa Jabir Shekimweri alisema utafiti huo umeonesha mafanikio makubwa hasa pale unapoyaangalia mahindi yaliyotumia mbegu iliyotokana na teknolojia hiyo kuwa ni bora na makubwa wakati yale yaliyotumia mbegu za kienyeji kuwa dhaifu.


"Nisema kuwa mbegu za utafiti huu zitakapoanza kutumika zitasaidia sana wakulima hasa wa wilaya yangu ambayo inakabiliwa na ukame katika baadhi ya maeneo" alisema Shekimweri.

VIONGOZI WA VIJIJI WAHOFIA UTEKELEZAJI WA KODI YA MAJENGO



Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na wenyeviti wa vijiji, watendaji wa vijiji, watendaji wa kata, tarafa pamoja na wakuu wa idara wa halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuhusu utekelezaji wa kodi ya majengo kwa vijiji wakati wa kikao cha kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Iringa jana. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)







Mwenyekiti wa Kijiji cha Mahuninga, Kata ya Mahuninga wilayani Iringa, mkoani Iringa Lonjino Mkwele akimuuliza swali Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela (hayupo pichani) kuhusu utekelezaji wa kodi ya majengo kwa vijiji wakati wa kikao cha kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Iringa jana. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)





VIONGOZI wa vijiji vyote wa Wilaya ya Iringa, mkoani Iringa waagizwa kusoma mapato na matumizi ili kuwarahisishia wananchi kufahamu jinsi fedha zao zinavyotumika na kutoa fursa kwa wananchi kupata nafasi ya kuhoji ili kujiridhisha pale wanapokuwa na mashaka.

Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa (DC), Richard Kasesela wakati wa mkutano na wenyeviti wa vijiji, watendaji wa vijiji, watendaji wa kata, tarafa pamoja na wakuu wa idara wa halmashauri ya Wilaya ya Iringa .

Kikao hicho cha kazi kililenga kuwakumbusha wenyeviti na watendaji wa vijiji na Kata kutambua majukumu yao na kuyapatia majibu sawia pamoja na swala zima la ukusanyaji mapato .

DC Kasesela ameagiza kufanyanyika uchunguzi ili kubaini kama kuna watendaji waliohamishwa kazi na wanatuhumiwa kuhujumu mapato ya serikali na michango ya wananchi kwa ajili ya shughuli za maendeleo kurudishwa haraka. 

Mkuu huyo wa Wilaya amewaagiza watumishi wote wa serikali ngazi ya Vitongoji, Vijiji na Kata kufanya kazi kwa haki, Usawa na uwazi na kiwashirikisha wananchi katika kila jambo linalohusu vipaombele vya maeneo yao. 

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa vijiji waliohudhuria katika mkutano huo wamempongeza mkuu wa Wilaya ya Iringa kwa kufanya mkutano uliyolenga kuwakumbusha majukumu yao pamoja na kuwakutanisha kwa pamoja.

Wakati huohuo, watendaji wa vijiji, watendaji wa kati pamoja na watu wa mapato wamekumbushwa kukusanya kodi ikiwemo kodi ya majengo.

Hata hivyo baadhi ya viongozi wa vijiji wamekuwa na wasiwasi kuhusu utekelezaji wa kodi ya majengo kwa kusema wananchi wengi katika maeneo hawana uelewa juu ya kodi hiyo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mahuninga, Kata ya Mahuninga wilayani Iringa, Lonjino Mkwele alitaka kujua Kodi ya Majengo itatozwaje.

Kwa upande wake, Mdhamini wa Wilaya ya Iringa, John Brayson aliwaomba wananchi wote kulipa kodi ya majengo kwa maendeleo ya uchumi.

Alisema wameanza zoezi kwa kuthamini na ukusanyaji wa kodi ya majengo na mchakataji wa taarifa za majengo umeanza katika jumla ya vijiji 133 vya wilaya pamoja na kata 28.

Brayson alisema kuwa wanapata changamoto katika kutekeleza sheria ya kodi ya majengo hasa maeneo ya vijiji hapo awali walikuwa hawatozwi.

ADHABU KWA ATAKAYESHINDWA KULIPA KODI YA MAJENGO

· Kutozwa faini ya asilimia 50 ya kodi yake.

· Asipolipa halmashauri imepewa mamlaka ya kukamata mali yenye thamni sawa na kodi na kuuza kufidia kodi hiyo.


Kodi ya majengo katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ilianza kutozwa mwaka 1983, katika kipindi hicho kodi hii ilitozwa katika maeneo ya majiji, manispaa, miji midogo na makao makuu ya halmashauri ya wilaya tu.

Lakini mwaka 2015 yalifanyika marekebisho ya sheria kuruhusu hata maeneo mengine ya halmashauri ya wilaya kutoza kodi ya majengo kwa kuthamini majengo kwa njia ya mkupuo.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...