Thursday, 23 June 2016
ASILIMIA 89 YA WATANZANIA WAMKUBALI RAIS MAGUFULI; UTAFITI WA CZI WABAINISHA
Mwanasheria msomi, kutoka taasisi huru inayojishughulisha na ushauri wa mambo ya habari, (CZI), David Saile Manoti, (katikati), akiwa na wasomi wenzake, Bi Dotto Nyirenda, (kushoto) na Juma George Chikawe, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Juni 23, 2016. Wanazuoni hao ambao ni wanachama wa CCM, wamesema utafiti unaonyesha Watanzania wengi wanaimani kubwa na Rais Magufuli katika mageuzi yake ya uchumi na nidhamu.
David Saile Mnoti, Mwanasheria, czi
NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
TAASISI ya ushauri wa mambo ya Habari ijulikanayo kama CZI, imetoa utafiti unaoonyesha kuwa katika kipindi cha miezi 8 ya utawala wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Watanzania wengiwanamkubali Rais na wanayo imani kubwa Tanzania itarudi kwenye “mstari’.
Watafiti hao, ambao ni David Saile Manoti ambaye amebobea kwenye masuala ya Sheria, Juma George Chikawe, yeye ni mtaalamu wa Teknohama, na Dotto Nyirenda ambaye amebobea kwenye masuala ya Kidiplomasia, wamesma sambambana utafitihuo pia wameelezea kuwa Rais Magufuli atakapopewa dhamana ya kukiongoza Chama Cha Mapinduzi CCM hapo Julai 27 kwenye mkutano mkuu maalum wa chama hicho tawala, ufanisi wake katika kuongoza nchi utaongezeka.
Kwa mujibu wa wanazuoni hao, walisema utafiti wao ulifanyika nchi nzima na walitumia njia ya kuwahoji watu papo kwa hapo, kuwahoji kwa kupitia simu au kuwahoji kimakundi.
Akizungumzia utafiti wa miezi 8 ya Rais Magufuli akiwa madarakani, Mwanasheria David Saile Manoti, alsiema, kundi la kwanza walilolihoji ni lile la vijana wenye umri kati ya miaka 14-18 ambao wengi wao ni wanafunzi. “Baada ya kundi hili kuhojiwa lilionyesha imani kubwa ya Rais kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi, atarejesha nidhamu ya masomo mashuleni.” Alsiema Manoti.
Kuhusu kundi la vinaja wa miaka 10-30 asilimia 82 ya waliohojiwa wameonyesha imani kuwa Rais John Magufuli ataleta mageuzi kwenye elimu hususan masuala ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na kumaliza tatizo la mabweni wka wanafunzi.
Akizungumzia kundi la miaka 30-60, Manoti alisema, Watumishi wa umma wameonyesha imani kuwa Rais Magufuli atarejesha imani kwa serikali kutokana na jinsi anavyoshughulikia mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.
Aidha utafiti unaonyesha kuwa asilimia 89.0 ya kundi hili limeonyesha imani kubwa kwa Rais kumaliza matatizo ya wazee kwa kuanza kuwalipa posho kwa mwezi.
Katika utafiti huu, Manoti amebainisha kuwa umoja na mshikamano mongoni mwa Watanzania utaimarika zaidi, vile vile kundi hili limesema Rais Magufulu anazidi kuwa maarufu huku wapinzani wakionekana kupoteza umaarufu klutokana na kushindwa kubuni mbinu mpya ya mapambanoya kisiasa. "Kwa ujumla wake Mh. Rais Magufuli anakubalika kwa asilimia 89% huku akiwapiku Edward Lowassa na Mh. Jakaya Kikwete ambao wao wamegawana zilizobaki, Mh. Kikwete asilimia 7% na Mh. Edward Lowassa akiwa na asilimia 4%.
Akizungumzia mkutano mkuu maalum wa CCM, Mwanadiplomasia Dotto Nyirenda yeye amewaasa wana CCM kutambua mambo 10 ambayo Rais Magufuli anatosha kuyasimamia.
Aliyateja mambo hayo kuwa ni pamoja na rasilimali watu, rasilimali ardhi, majengo na viwanja, wanazuoni wa kila taaluma, wafanyabiashara ndogondogo (machinga), wanayabiashara, wanachama wanaozidi milioni 9, Mashabiki wake wanaozidi milioni 28.9, wakulima, wavuvi, na wafugaji, laini pamoja na “utajiri” huo, CCM haiwezi kujiendesha na inategemea ruzuku kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, pamoja na wafadhili ambao wengine sio wasafi kwenye rekodi zao.
Dotto Nyirenda, Mwanadiplomasia, czi
Juma George Chikawe, Mtaalamu wa Teknohama CZI
JPM AZINDUA SARAFU MPYA YA SHILINGI ELFU 50 WAKATI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA BOT
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizindua sarafu maalumu ya shilingi 50,000/- kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndullu, na kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar, Khamisi Musa Omar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisimama kwa ukakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango, Dkt Servacius Likwelile,(wapili kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedhana Mipango Zanzibar, Khamis Mussa Omar, (wakwanza kushoto), Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu, 9wapili kushoto), na Mkuu wa Mkoa wa Dar e3s salaam Mhe Paul Makonda(wakwanza kulia). kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Dkt Servacius Likwelile alipowasili kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipokea mfano wa hundi ya bilioni 4 kutoka kwa gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Benno Ndullu ikiwa ni mchango wa benki hiyo kununulia madawati kwa ajili ya wanafunzi, fedha ambazo zimetokana na kubana matumizo. Wanaosjuhudia Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Servacius Likwelile, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ya Zanzibar Khamis Mussa Omar, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na Profesa Paul Collier, mwandishi wa kitabu cha "Tanzania: The path to prosperity" kilichozinduliwa na Rais leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akatika picha ya pamoja na Magavana na Manaibu Magavana na menejimenti ya BOT kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
Wageni waalikwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
Wageni waalikwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akibofya kitufe kuashiria uzi8nduzi rasmi wa maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo
Juni 22, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizindua Kitabu kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...