Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mahmood Mgimwa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini akifungua mashindano ya Ligi ya Ujirani Mwema yalioandaliwa kwa udhamini wa Shamba la miti Sao Hill mjini Mafinga wilayani Mufindi, mkoani Iringa jana. walioketi kutoka kushoto ni Meneja wa Shamba la miti Sao Hill Salehe Beleko na Mwenyekiti wa CCM (W) Mufindi ambaye pia Diwani wa Kata ya Makungu Yohanes Cosmas Kaguo
Meneja wa Shamba la miti Sao Hill, Salehe Beleko (kushoto) akisalimia na golikipa wa Timu ya Ihalimba Vijijini FC kabla ya mechi kuanza.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mahmood Mgimwa (kulia) ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini akiwasili katika viwanja vya Ihefu kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi ya Ujirani Mwema ya Sao Hill jana.
SAOHILL imeanzisha mashindano ya Ligi ya Ujirani Mwema kwa kushirikisha vijiji vinavyozunguka shamba hilo ili kulinda na kutunza rasilimali za misitu na nyuki.
Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo, Said Aboubakar alisema kuwa Ligi ya Ujirani Mwema itashirikisha timu nane ambazo ni Ihefu Misitu, Ihalimba Mseto, Ihefu Mseto, Mgololo Misitu, Mgololo Mseto, Irindi Misitu na Irindi Mseto zilizogawanywa katika makundi A na B.