Sunday, 22 March 2015

Lee Kuan Yew afariki dunia

Waombolezaji wakiweka mashada ya maua mbele ya hospitali aliyofia baba Lee Kuan Yew.
Waziri mkuu mwanzilishi wa Singapore, Lee Kuan Yew amefariki dunia.Lee amefariki akiwa na umri wa miaka tisini na mmoja kutokana na ugonjwa wa mapafu.
Kwa miongo mitatu ya utawala wa Lee alifanikiwa kuipitisha nchi yake katika kipindi cha mpito na kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi hasa katika usafirishaji majini kwa kutumia rasilimali kidogo walizokuwa nazo na sasa kuwa kitovu kikubwa cha kibiashara cha kimataifa.
David Adelman ni balozi wa zamani wa Marekani nchini humo, ametuma salamu zake za rambi rambi.Kifo cha Lee ni mwisho wa zama zake.mwisho wa mwanamume mwenye nguvu ya ushawishi aliyeingia madarakani katikati ya miaka ya sitini .
Lee alifanikiwa kuanzisha ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi yake na Marekani ambao umedumu hata leo na unaweza kuvuka mipaka sio kwa singapore tu bali hata kwa watu wa Asia ya kusini Mashariki. (BBC)

ARUSHA YAMKUBALI KINANA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Arusha mjini kwenye uwanja wa mkutano wa Sheikh Amri Abeid ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa CCM itaendelea kuwatetea watu masikini na itahakikisha inawapa nafasi za uongozi watu wanaokubalika na wananchi.


Mwenyekiti wa CCM wa mkoa Onesmo Ole Nangole akihutubia wananchi wa Arusha ambapo aliwataka mawaziri kufanya ziara vijijini badala ya kukaa maofisini.

Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Arusha mjini na kuwaambia pesa isitumike kununulia madaraka .


Amani Ole Silanga aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Monduli na kujiunga na CCM akihutubia wananchi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Amani Ole Silanga aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Monduli na kujiunga na CCM akihutubia wananchi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo alisema Chadema hakina watu wenye sifa za kuongoza.

MANYONI MVUA HAIJANYESHA KWA MUDA MREFU MPAKA MAZOA YAMEKAUKA...!


Wakazi wa babati wilayani manyoni wakiwa katika pilikapili leo kama walivyokutwa stendi ya basi. 



Administrator wa blog ya SIMBAYA (FRIDAY SIMBAYA) akiwa Manyoni akichagua vinyago. NAMSHUKURU MUNGU NIMEFIKA SALA ARUSHA KUUNGANA NA KIKOSI KAZI.



Manyoni Lodge abiria tukipata chakula cha mchana baada ya safiri ndefu ya kutoka iringa kwenda Arusha. 

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...