Thursday, 24 November 2016

RAIS MAGUFULI NA RAIS MSTAAFU MWINYI WAKUTANA IKULU



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 23 Novemba, 2016 amekutana na kufanya Mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Dkt. Ali Hassan Mwinyi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.



Baada ya mazungumzo hayo, Alhaji Dkt. Ali Hassan Mwinyi amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli na kufanya nae mazungumzo kwa mara ya kwanza ni kumpongeza kwa kutimiza mwaka mmoja tangu aingie madarakani na pia kumpongeza kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi kifupi cha uongozi wake.

Alhaji Dkt. Ali Hassan Mwinyi ameyataja baadhi ya maeneo ambayo Rais Magufuli ameyafanya kwa mafanikio makubwa kuwa ni mapambano dhidi ya rushwa na amebainisha kuwa hatua zilizochukuliwa katika kipindi cha mwaka mmoja zimedhihirisha kasi kubwa ya kukabiliana na tatizo hilo ikilinganishwa na wakati uliopita.

“Rushwa ilikuwepo tangu enzi ya Hayati Mwalimu Nyerere, aliipondaponda kabisa lakini hakuimaliza, na sote tuliosalia ni hivyo hivyo, kila mmoja amefanya kwa kiasi chake, lakini Rais Magufuli kwa mwaka mmoja ameleta Sunami, nafurahi sana” amesema Alhaji Mwinyi.

Eneo jingine ni kuimarisha utendaji kazi Serikalini ambapo Alhaji Dkt. Ali Hassan Mwinyi amesema hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Rais Magufuli zimeongeza kasi zaidi na ametoa wito kwa Viongozi na Wananchi kuunga mkono juhudi hizo.

“Tuliobaki tumsaidie, tumsaidie kwa kumuombea Dua, tumsaidie kurekebisha kwa kusema ukweli pale ambapo watu wanapotosha, tuseme sio hivyo, ilivyo ni kadhaa kadhaa kadhaa, tusiwaache watu wakapata nafasi ya kuongea uongo, kila mtu anaweza kuwa anasema kutokana na nia yake na lengo lake, lakini hakuna asiyejua kuwa kazi aliyoifanya mwenzetu ni nzuri nzuri nzuri ya ajabu” amesisitiza Rais Mstaafu Mwinyi.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Novemba, 2016


WAZIRI MWAKYEMBE AJIPANGA KUWAFUKUZA MAHAKIMU WENYE CHETI NA DIPLOMA



Waziri wa katiba na sheria Mh. Dkt Harrison Mwakyembe amesema serikali itawafuta kazi mahakimu wote wa mahakama ya mwanzo wenye elimu ya cheti na diploma ya sheria.

“Tunahitaji mahakimu wenye uwezo wa sheria ambao wamehitimu shahada ya kwanza,hivyo serikali itawafuta kazi mahakimu wote wenye elimu ya cheti na diploma” 

Dkt Mwakyembe ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mswada wa sheria ya msaada wa kisheria ambapo amewaomba wananchi na wadau wa sheria nchini kufanyia mapitio mswada huo na kutoa maoni yao kwa kamati ya bunge ya katiba na sheria wakati utakapowadia.

Dkt Mwakyembe amesema bunge litaweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kupokea maoni ya wadau wote watakaofika mbele ya kamati na wale watakao wasilisha maoni yao kwa njia ya maandishi.

Aidha waziri mwakyembe ameelezea mswada huo ambao umesomwa bungeni kwa mara ya kwanza tarehe 10 novemba utawatambua watoa huduma za msaada wa kisheria na utakuwa ni ukombozi kwa jamii ya watanzania walio wengi ambao hushindwa kumudu gharama za kuwalipa mawakili.


WASHINDI WA SINGELI IRINGA WAOMBA KUUNGWA MKONO


Innocent aka Lusso Mnyama 



Isihaka aka Msangazi baharia





WASHINDI wa mashindano ya kuimba singeli mkoa wa Iringa, Isihaka Msangazi ‘Baharia’ na Innocent Chanafi’ Lusso Mnyama’ wamewataka wadau kuwaunga mkono katika harakati zao kuupandisha muziki huo nyanda za Juu Kusini.

Wakizungumza na SIMBAYABLOG jana mara baada ya kushinda mashindano ya kuimba sengeli katika mkoa wa Iringa yaliandaliwana kituo cha Radio cha Nuru Fm, Mshindi wa kwanza, Isihaka na Innocent walisema kuwa muziki huo unakuwa kwa kasi zaidi kutokana na ubora wake na kuonyesha uhalisia wa kitanzania zaidi.

Walisema kuwa wawekezaji wakiwa wengi katika aina hiyo ya muziki ni lazima ajira iongezeke kupitia fani ya muziki hasa huu wa singeli ambao kwa sasa unazidi kuteka hisia za mashabiki wengi hasa katika sherehe mbalimbali.

Kwa upande wake mshindi wa kwanza, Isihaka Msangazi alisema kuwa ushindi wake umekuja kutokana na kujituma kwa bidii katika mazoezi na kuupenda muziki huo ambapo lengo ni kufika mbali zaidi katika kuwakilisha mkoa wa Iringa na taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa mshindani wake alikuwa mkali lakini baada ya majaji kuona anastahili ushindi alimpongeza mshindani wake Lusso Mnyama kwa kuweza kukubali hali halisi ya mashindano hivyo natoa wito kwa wadau kutuunga mkono katika harakati za kuinua muziki wa singeli nyanda za juu kusini.

. “Watu waje wengi kuusaidia muziki huu kuanzia mapromota na wengineo kwa kuwa wananchi wanaupenda na kazi ni kuuinua zaidi na sio kuuona ni kama muziki wa kawaida kwani kwa sasa wengi wanachukulia kama mziki wa kihuni kitu ambacho sio kweli” alisema

Alisema kuwa hadi sasa anatarajia kuingia studio na kuandaa vibao mbalimbali vyenye staili ya singeli ambavyo vitakuwa moto wa kuotea mbali ndani ya nyanda za juu kusini na Tanzania kwa ujumla.

Naye Innocent Chanafi ambaye alikuwa mshindi wa pili katika mashindano hayo alisema kuwa asilimia kubwa ya watu kwa sasa wako katika muziki wa bongo fleva lakini baada ya mashindano hayo ana uhakika Iringa itakuwa moja ya mikoa yenye waimbaji wengi wa muziki wa singeli.

Alisema kuwa mashindano hayo ya kuimba singeli mkoa wa Iringa yamemsaidia sana kuweza kutambua ni kwa kiasi gani kwa sasa yanaweza kuwa moja ya aina ya muziki ambao utaubeba uhalisia wa Mtanzania Kimataifa kutokana na vionjo vyake.

Alisema kuwa aina hii ya uimbaji inaonekana kuwa ni aina mpya ambayo inaweza kuutambulisha muziki wa kitanzania nje ya nchi hasa kutokana na aina yake ya uimbwaji, uchezaji hata mashabiki wake kwani wengi wao ni vijana ambao ni taifa la kesho katika kusogeza mbele maendeleo ya Tanzania.

Alisema hadi sasa anatarajia kutoa nyimbo mbili za ‘Shem Lake’ na 'Baki na Mimi ambazo amefanya katika studio za Familly rekodi chini ya produza Yuda Tz zilizoko jiji Dar es salam.










WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...