Thursday, 24 November 2016

WASHINDI WA SINGELI IRINGA WAOMBA KUUNGWA MKONO


Innocent aka Lusso Mnyama 



Isihaka aka Msangazi baharia





WASHINDI wa mashindano ya kuimba singeli mkoa wa Iringa, Isihaka Msangazi ‘Baharia’ na Innocent Chanafi’ Lusso Mnyama’ wamewataka wadau kuwaunga mkono katika harakati zao kuupandisha muziki huo nyanda za Juu Kusini.

Wakizungumza na SIMBAYABLOG jana mara baada ya kushinda mashindano ya kuimba sengeli katika mkoa wa Iringa yaliandaliwana kituo cha Radio cha Nuru Fm, Mshindi wa kwanza, Isihaka na Innocent walisema kuwa muziki huo unakuwa kwa kasi zaidi kutokana na ubora wake na kuonyesha uhalisia wa kitanzania zaidi.

Walisema kuwa wawekezaji wakiwa wengi katika aina hiyo ya muziki ni lazima ajira iongezeke kupitia fani ya muziki hasa huu wa singeli ambao kwa sasa unazidi kuteka hisia za mashabiki wengi hasa katika sherehe mbalimbali.

Kwa upande wake mshindi wa kwanza, Isihaka Msangazi alisema kuwa ushindi wake umekuja kutokana na kujituma kwa bidii katika mazoezi na kuupenda muziki huo ambapo lengo ni kufika mbali zaidi katika kuwakilisha mkoa wa Iringa na taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa mshindani wake alikuwa mkali lakini baada ya majaji kuona anastahili ushindi alimpongeza mshindani wake Lusso Mnyama kwa kuweza kukubali hali halisi ya mashindano hivyo natoa wito kwa wadau kutuunga mkono katika harakati za kuinua muziki wa singeli nyanda za juu kusini.

. “Watu waje wengi kuusaidia muziki huu kuanzia mapromota na wengineo kwa kuwa wananchi wanaupenda na kazi ni kuuinua zaidi na sio kuuona ni kama muziki wa kawaida kwani kwa sasa wengi wanachukulia kama mziki wa kihuni kitu ambacho sio kweli” alisema

Alisema kuwa hadi sasa anatarajia kuingia studio na kuandaa vibao mbalimbali vyenye staili ya singeli ambavyo vitakuwa moto wa kuotea mbali ndani ya nyanda za juu kusini na Tanzania kwa ujumla.

Naye Innocent Chanafi ambaye alikuwa mshindi wa pili katika mashindano hayo alisema kuwa asilimia kubwa ya watu kwa sasa wako katika muziki wa bongo fleva lakini baada ya mashindano hayo ana uhakika Iringa itakuwa moja ya mikoa yenye waimbaji wengi wa muziki wa singeli.

Alisema kuwa mashindano hayo ya kuimba singeli mkoa wa Iringa yamemsaidia sana kuweza kutambua ni kwa kiasi gani kwa sasa yanaweza kuwa moja ya aina ya muziki ambao utaubeba uhalisia wa Mtanzania Kimataifa kutokana na vionjo vyake.

Alisema kuwa aina hii ya uimbaji inaonekana kuwa ni aina mpya ambayo inaweza kuutambulisha muziki wa kitanzania nje ya nchi hasa kutokana na aina yake ya uimbwaji, uchezaji hata mashabiki wake kwani wengi wao ni vijana ambao ni taifa la kesho katika kusogeza mbele maendeleo ya Tanzania.

Alisema hadi sasa anatarajia kutoa nyimbo mbili za ‘Shem Lake’ na 'Baki na Mimi ambazo amefanya katika studio za Familly rekodi chini ya produza Yuda Tz zilizoko jiji Dar es salam.










No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...