Sunday, 4 February 2018

DKT KIGWANGALLA ASITISHA VIBALI VYA KUHAULISHA MISITU YA HIFADHI ....



Waziri wa maliasli na utalii dkt hamisi kigwangalla akiongoza kamati ya misitu kutembelea msitu wa hifadhi wa Kihesa kilolo uliopo manispaa ya IRINGA kujiridhisha na mipaka kabla ya kuhaulisha sehemu ya msitu huo wenye ukubwa wa zaidi akari 500 kwa ajili shughuli za utalii jana. (Picha na Friday Simbaya)

Image may contain: plant, tree, outdoor and nature

WAZIRI wa maliasili na utalii Dk.Hamis Kigwangala amewaagiza wakuu wa mikoa kote nchini kwamba wasihangaike kuandika barua za kuomba kuhaulisha misitu ya vijiji au halmashauri ili zitumika kwa shughuli za maendeleo.

“Mimi hapa, nina msimamo mkali sana,Naomba Taifa lifahamu, lijuwe na viongozi wote wafahamu wasithubutu kuleta maombi ya kuhaulisha misitu iliyohifadhiwa kwa sababu hayo maombi nimekwisha yakataa kabla hayajafika mezani kwangu.”amesema Dk. Kigwangala na kuongeza: 

“Kwa kipindi ambacho nitakuwa waziri wa mali asili na utalii sitohaulisha misitu hivyo viongozi wasahau kupoteza muda wao kuomba maeneo yaliyohifadhiwa kwamba yahaulishwe kwa ajili ya makazi,kilimo au shughuli nyingine za maendeleo hilo halitofanyika wakati mimi nikiwa waziri.”alisema Dk.Kigwangala

Dk.Kigwangala amesema hayo jana kwenye mkutano wa tatu wa kamati ya kitaifa ya ushauri wa misitu (National Forestry Advisory Committee -NAFAC) uliofanyika mjini Iringa.

Kamati hiyo ilifika mjini Iringa kwa lengo kupitia mapendezo ya kuhaulisha sehemu ya msitu wa Kihesa kilolo uliopo katika manispaa ya Iringa ambapo manispaa iliomba eneo hilo litumike kwa ajili ya shughuli za utalii.

Pia kamati hiyo ilifika kufuatia mapendekezo aliyoyowasilishwa katika kikao cha pili cha kamati ya mwaka jana kama eneo waliloomba ni sahihi ama la.

Dk.Kigwangala alisema kuwa amekuwa na ndoto ya kutaka kubadilisha misitu iliyokuwa ikisimamiwa na kundeshwa na vijiji au halmashauri kumilikiwa na serikali.

“Katika mambo ambayo mimi sikubaliani nayo ni kwamba kuna misitu zipo kwenye halmashauri na vijiji lakini ruhusa ya kutumia inatoka serikalini hii ni mambo ambayo sikubali kwa sababu misitu inapotea,inateketea na umiliki na uendeshaji wa misitu kwa mamlaka za chini zimeonekana hazina faida zozote kwenye uhifadhi hivyo ni wazo ni ndoto nimekuwa nayo baada ya kujifunza namna wizara ya mali asili inatekeleza majukumu yake na nikaona hapa kuna mapungufu makubwa.”alisema Dk.Kigwangala.

Katika hatua nyingine amesikitishwa kuona sekta ya misitu nchini ikichangia pato dogo la taifa ambapo takwimu zinaonesha misitu inachangia takribani asilimia 3.7 katika pato la taifa.

“Sisi kama wizara haturidhishi na mchango huu bado tunaona upo chini sana kiasi cha kutishia kutoaminika kwa takwimu hizi,hili ni eneo ambalo tunaona nilakufanyia kazi iwezekanavyo na hivyo ninaomba kamati hii ije na ushauri ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia sekta hii katika kuongeza pato la taifa.”alisema Kigwangala.

Hata hivyo aliomba kamati ya ushauri ya misitu kuja na ushauri wa jinsi gani wanaweza kuitumia sekta huyo ya misitu katika kuongeza mchango wake katika pato la taifa.

“Kama wizara tunataka tulitazame kwa upya eneo hili la matumizi ya mkaa kama nishati pekee inayotumiwa na wananchi wingi katika kupikia na kuona ni kwa jinsi gani tunaweza tukalitumia zao hili vyema ili kuongeza mapato.” alisema Dk. Kigwangala.

Naye naibu waziri wa mali asili na utalii Japheth Hasunga alisema kuwa alimpongeza mkuu wa mkoa huo kuhakikisha korido ya kusini inafunguka kwenye sekta ya utalii.

“Katika kipindi cha mwaka 2017 watu wengi walienda kutembelea hifadhi za ndani,utalii wa nchi hii unatakiwa utokane na utalii wa ndani wale wa nje iwe ni nyongeza.”alisema Hasunga nakuongeza:

“Najuwa kamati hii itakushauri mambo mengi katika masuala mazima ya misitu kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii na vizazi vijavyo lakini pia tunategemea sana katika kutoa mwelekeo wa namna bora wa kutumia rasilimali hii na kuhakikisha inazalisha faida.”alisema Hasunga.
Image may contain: 1 person, sitting, table and indoor
Katika kipindi kifupi wameshughudia mambo mengi yametokea katika hifadhi ikiwamo malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusiana na hatua mbalimbali ambazo serikali inachukua katika kuhakikisha usimamizi wa mali asili hizo zinakuwa mathubuti.

“Huenda tunafanya sawa au tunakosea hivyo kazi ya kamati hii ni kutushauri sisi kama tunachokifanya sawa au sio sawa huku akiwataka wajumbe hao kufanya kazi yao kwa weledi na kwa kuzingatia taaluma waliyo nayo.”alisema Hasunga.

Naye mkuu wa mkoa huo Amina Masenza aliomba wizara hiyo kufikiria ombi lao la kutaka kuhaulisha sehemu yam situ huo ili waweze kufanya shughuli za utalii huku akihaidi kufanyia kazi maagizo ya wizara ikiwamo kuondoa dampo kwenye eneo la msitu uliohifadhiwa,kuweka mipaka.

Kamati hiyo iliambatana na Waziri wa mali asili na utalii Dk.Hamis Kigwangala,Naibu waziri wa wizara hiyo Japhet Hasunga,Naibu katibu mkuu wa wizara hiyo Dk.Aloyce Nzuki pamoja viongozi wa mkoa wa Iringa kutembelea msitu huo.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...