Wednesday, 5 October 2016

SERIKALI YARUHUSU WIMBO WA CHURA WA MSANII SNURA KUPIGWA



Snura Mushi



Msemaji wa Msanii Snura Baraka Nyagenda akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salamm leo.



Msanii Snura Mushi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu kupigwa kwa wimbo wa chura ya kuufunga kwa kuwa haukuwa na maudhui mazuri ya kitanzania. Kushoto ni Msemaji wake, Baraka Nyagenda.




Mkutano na wanahabari ukiendelea.




N a Dotto Mwaibale


SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu kupigwa kwa wimbo wa chura wa msanii Snura Mushi baada ya kuufunga kwa kuwa haukuwa na maudhui mazuri ya kitanzania.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Snura Mushi alisema wimbo wake na video umeruhusiwa kupigwa baada ya audio ya chura kufanyiwa marekebisho na kuifanya kuwa katika maudhui ya kitanzania.

Alisema ruhusa hiyo imetolewa kwa barua iliyoaandikiwa Septemba 26, 2016 yenye kumbukumbu HA.26/375/01'B'/137 ambayo gazeti hili lina nakala yake.

Kupitia mkutano huo msanii Snura Mushi kwa mara nyingine aliomba radhi kwa watanzania na Serikali kwa ujumla kwa usumbufu walioupata kwa video yake ya kwanza na kuwaomba waendelee kuiona video mpya iliyorekebishwa baada ya kuifuta ya kwanza.

FAST JET YAANZISHA SAFARI ZA NDEGE MPYA NCHINI



Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kuanza kutumia ndege mpya aina ya Embraer 190 kusafirisha abiria. Kulia ni Ofisa Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo, Lucy Mbogoro.


Ofisa Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo, Lucy Mbogoro (kulia), akizungumza katika mkutano huo.



Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse (katikati), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Huduma kwa Wateja, Christina Kausan.



Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.






Dotto Mwaibale






WANANCHI wametakiwa kuchangamkia usafiri wa ndege wa Kampuni ya Fast jet baada ya kampuni hiyo kuanza kutumia ndege mpya aina ya Embraer 190 ambayo ni nafuu zaidi kwa matumizi.






Mwito huo umetolewa na Dar es Salaam leo na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse wakati akizungumza na waandishi wa habari jana kuwa ndege hizo ni rahisi kwa matumizi ya usafiri hapa nchini. 






Alisema kuwa ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 108 aliongeza kuwa zitahudumia kwa miezi 6 huku ikitoa nafasi kwa mafunzo wa marubani wa Fast jet hapa nchini.






Aliongeza kuwa kwa kuwa Fast jet hapa nchini imepata hasara kiuendeshaji hivyo ndege hizo kwa kuwa hazitumii matufa mengi itasaidia kuiimarisha biashara.






" Hii imetokea tu kuwa wakati serikali imeleta aina ya ndege zisizotumia mafuta mengi na sisi tulikuwa pia tumeshaanza mchakato huo na hivyo kwa sasa binafsi naona kuwa watanzania watanufaika zaidi" alisema Corse.






Pia aliipongeza serikali kwa kuleta ndege mpya aina ya Bombardier 8, Q400 ambazo zinaenda mikoa ya Rukwa, Mara, Kagera na Dodoma ambapo ndege za Fast jet hazifiki.






Alisema kwa kuwa lengo la Fast jet ni kuwapatia watanzania huduma nafuu za usafiri wa anga hivyo inafurahia pale ambapo inaona kuwa ndege za serikali zinafika mikoa ambayo Fast jet haifiki. 









Alisema kuwa kwa kupeleka ndege kwenye mikoa hiyo ni hatua ambayo inatimiza lengo la Fast jet la kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za anga kwa bei rahisi na kwa wakati.


WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...