Wednesday, 11 October 2017

WAAJIRI WA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI JIJINI MWANZA WALAUMIWA



Mkufunzi wa mafunzo kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani katika Kata ya Buhingwa Jijini Mwanza, akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo hii leo. Mafunzo hayo yafanyika kwenye ukumbi kwa kanisa la AICT Buhingwa kuanzia jana na yatafikia tamati kesho Oktoba 12,2017.





Na George Binagi-GB Pazzo


Baadhi ya waajiri wa watoto wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza wameelezwa kuwa kikwazo cha kuwaruhusu watoto hao kupata elimu ya utambuzi yanayotolewa na shirika la WoteSawa.


Mratibu wa shirika hilo linalotetea haki na maslahi kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani, Cecilia Nyangasi ameyasema hayo hii leo wakati wa mafunzo kwa watoto wafanyakazi katika Kata ya Buhongwa jijini hapa.



“Waajiri wamekuwa ni changamoto kubwa kwa sababu wengi wao wanadhani kwamba tunakuja kuwapotosha watoto wao”. Alisema Nyangasi na kubainisha kwamba shirika la WoteSawa linatoa elimu ya kuwajengea uwezo wa kutambua haki zao kisheria, wajibu wao kazini pamoja na elimu ya afya ya uzazi ili kuondokana na mimba za utotoni.


Nyangasi alisema baada ya mafunzo hayo ya siku tatu kuanzia jana, itaundwa kamati ya watoto wafanyakazi wa nyumbani Kata ya Buhongwa kama ilivyofanyika kwenye Kata za Nyakato, Mecco, Isamilo, Pasiansi, Kirumba na Mkuyuni ambapo jukumu kubwa la kamati hizo ni kuwa mabalozi wa watoto wengine ambao hawakufikiwa na mafunzo hayo.


Suzana John na Lugwisha Zakaria ambao ni baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo yaliyojumuisha watoto 47 katika Kata hiyo ya Buhongwa, wamesema mafunzo hayo yamewasaidia kutambua haki zao kisheria na pia wajibu wao kama waajiriwa.






Mwanasheria Joseph ambaye ni mkufunzi wa mafunzo hayo


Mkufunzi wa mafunzo hayo akifafanua jambo


Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo yaliyoanza jana katika Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza akiuliza swali


Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo yaliyoanza jana katika Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza akiuliza swali


Washiriki wa mafunzo hayo katika Kanda ya Buhongwa Jijini Mwanza


Washiriki wa mafunzo hayo katika Kanda ya Buhongwa Jijini Mwanza


Mratibu wa WoteSawa, Cecilia Nyangasi (kushoto) akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo


Afisa kutoka shirika la WoteSawa la Jijini Mwanza


Suzana John, mshiriki wa mafunzo hayo


Lugisha Zakari, mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo.


LHRC YAPINGA ADHABU YA KIFO


KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeitaka serikali kubadilisha sharia, kuondoa adhabu ya kifo kwa kuweka adhabu mbadala kwenye makosa ya jinai na wafungwa waliopo katika vifungo vya muda mrefu gerezani.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa LHRC Anna Henga akizungumza na waandishi wa habari juu ya kupinga adhabu ya kifo leo jijini Dar es Salaam.


Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Anna Henga akizungumza na Mtandao wa Matukio360, amesema kuwa kituo hicho kinaungana na Mtandao wa Kupinga Adhabu ya Kifo Duniani katika maadhimisho ya 15 siku ya kupinga adhabu ya kifo.


Henga amesema adhabu ya kifo ni adhabu ya kikatili ambayo inakinzana na misingi ya utu na haki za binadamu kama ilivyoainishwa katika mikataba mbalimbali ya kimataifa.


“Adhabu ya kifo ni adhabu ya kikatili isiyo ya staha, inayotweza utu wa binadamu, inafanya serikali ionekane pia kama mhalifu kwa kuua, tuitake serikali ibadilishe sharia na kuondoa adhabu ya kifo na kuweka adhabu mbadala kwenye makosa ya jinai na kwa wafungwa waliopo mfano vifungo vya mrefu,” amesema Henga.


Aidha LHRC kime mpongeza Rais John Magufuli kwa kuweka wazi msimamo wake wa kutounga mkono adhabu ya kifo kwani ni ya kinyama na isiyostahili binadamu yeyote.


Kwa upande mwingine Henga ametoa sababu za kituo hicho kupinga adhabu hiyo. Miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na adhabu kuwa ya kibaguzi kwani mara nyingi wanaopatikana na hatia na kupewa adhabu hiyo ni maskini wasioweza kuwa na ushauri wa kisheria na watu wengine.


Nyingine ni vigumu kuthibitisha kuwa inatekelezwa tu kwa watu ambao wametenda na kukutwa na hatia ya kosa hili au wabaya Zaidi, Adhabu hiyo ikitolewa kwa mtu asiye na hatia kimakosa huwezi kuirekebisha kwani mfumo wa utoaji haki huwa pia na uwezekano wa kuwa na mianya ya makosa.


Ameongeza nyingine kuwa ni adhabu kutompa nafasi mtuhumiwa kujirekebisha bali ni ya kulipiza kisasi na wala haimsaidii mtu yeyote hata familia ya muathirika, hakuna ushahidi wowote kuwa adhabu hiyo inazuia watu wengine kutokwenda makosa kama hayo.


Pia amesema sharia hiyo inamianya ya makosa na ni vigumu kuwa na uhakika kuwa haki itatendeka kila wakati. Wapelelezi –ubambikiwaji wa kesi, changamoto za kiupelelezi, waendesha mashtaka, huweza kufanya makosa, majaji kufungwa mikono kulingana na uwakilishi mbele yao na kubanwa na sharia inayowataka kutoa adhabu ya kifo kwenye makosa tajwa.

WANA GDSS WAFANYA UCHAMBUZI NA KUANGALIA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI KATIKA BAJETI YA TAIFA


Washiriki wa semina za jinsia na maendeleo (GDSS) wamekutana jumaatano hii lengo likiwa ni kujadili ushirikishwaji wa moja kwa moja wa wananchi katika upangaji wa bajeti kuu ya taifa.

Mlaghbishi wa semina ya GDSS wiki hii Bw. Hancy Orote akitoa ufafanuzi juu ya jambo fulani katika semina iliyofanyika mapema wiki hii makao makuu ya TGNP Mtandao Mabibo Dar es salaam.


Akiongoza semina hiyo mwanaharakati kutoka GDSS Bw. Ance Obote alisema dhumuni la kukutana mahali hapo ni wanaharakati kubadilishana uwezo kuhusu ufahamu, ushiriki na jinsi gani wanatoa elimu hiyo kwa wananchi kuhakikisha wanaitumia haki yao ya msingi ya kushiriki katika bajeti.


Muwezeshaji huyo amesema kuwa wananchi huusika sehemu kuu mbili ambazo ni kwenye kupanga vipaumbele na ufuatiliaji(utekelezaji) lakini wananchi hawapewi nafasi ya kupanga vipaumbele na kinachofanyika ni diwani anakutana na mtendaji wa kata na kupanga kipi kianze kama kipaumbele na kipi kiwe cha mwisho.
Mshiriki wa semina za GDSS Bw. Geofrey Chambua akitoa mchango wake katika semina iliyofanyika mapema wiki hii Mabibo jijini Dar es salaam.


Na jambo lingine ni kwamba kwa maeneo ya mijini hakunaga vikao vinavyokaliwa na kujadili maendeleo ya mtaa ama kata hivyo mambo yanaendeshwa kienyeji na mambo mengi yanayofanywa yanakuwa ni akili za viongozi na siyo mawazo ya wananchi hali inayoweka ugumu katika utekelezaji wa mambo mengi kama hili la kuweka vipaumbele.


Aidha wanaharakati wameamua kuweka utaratibu wa kujipima kwa kuangalia harakati zao zinafika umbali gani na katika hili wameamua kupeleka ushawishi katika kata walau tatu na kuja kuangalia ushawishi wao wa kubadilisha dhana hii ya viongozi kupanga vipaumbele wenyewe bila kushirikisha wananchi inaweza kuisha?.
Bw. Msafiri Shabani akitoa maoni yake ya nini kifanyike ili kuhakikisha wananchi wanapata haki yao ya moja kwa moja ya kushiriki katika kupanga vipaumbele katika bajeti ya Taifa.


Lakini pia kupitia semina hiyo wanaharakati wameweka mipango mbalimbali ya kufuatilia jambo hilo na kugawana majukumu mpaka ifikapo tarehe 29 novemba kila kundi lililochaguliwa kufuatilia katika kata husika liwe limeleta mrejesho wa kilichopatikana na mgawanyo wenyewe ulikuwa kama ifuatavyo.


Washiriki wa semina za GDSS wamepewa majukumu ya kufuatilia katika serikali zao za mitaa kwa kuwahoji viongozi wa mitaa yao na kuleta mrejesho kwanini wananchi hawapati nafasi ya kushiriki katika kupanga vipaumbele na matokeo yake wanahusishwa katika hatua za mwisho ambazo ni utekelezaji.
Baadhi ya washiriki wa semina za GDSS walioudhulia mapema wiki hii.


Lakini vituo vya taarifa na maarifa wao wameombwa kufuatilia serikali kuu hii ikiwa ni katika wizara mbalimbali zinazohusika na hili ili kuweza kukusanya majibu ya serikali za mitaa pamoja na wizara kuweza kuwa na jibu moja lililokamilika kuhusu swala hilo.


Na jambo lingine ni kuabadilisha mtindo wa kuingia katika sekta hizi kwani wengi uenda kwa njia ya kujiita wanaharakati jambo ambalo linawafanya watu hawa kuwaona wao ni wapinzani na kuweka chuki miaongoni mwao, na pia imeelezwa sio vizuri kwenda mtu mmoja mmoja na wanatakiwa kuunda makundi madogo madogo yatakayowafanya waonekane ni wananchi kweli wanaohitaji taarifa za kata au mtaa wao.
Baadhi ya wanaharakati wakifuatilia kwa umakini semina iliyoendeshwa na Hancy Orote mapema wiki hii Mabibo Dar es salaam.


Aidha wanaharakati wameshauriwa kufanya kazi kwa moyo wa kijitolea na kuleta mabadiliko katika jamii yao na siyo kufanya ili waonekane na TGNP au kwa ajiri ya kuleta ripoti kwa mtu Fulani bali wafanye kwa manufaa yao na jamii iliyowazunguka. 



WAZIRI MWIJAGE AMJIBU DANGOTE...

SERIKALI kupitia kwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage imekanusha madai yaliyotolewa na Aliko Dangote kuwa, sera za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt Magufuli zinatishia wawekezaji.


Akizungumza jana, Waziri Mwijage amesema kuwa sera za uwekezaji ziko wazi na zina lenga kuhakikisha kuwa, serikali pia inanufaika na rasilimali za nchi.


Dangote ambaye ni tajiri namba moja Afrika alinukuliwa akisema kuwa, serikali imeweka sera ambazo zinaifanya imiliki asilimia kubwa ya hisa kwenye mali.


"Wanawatisha wawekezaji wengi, na kuwatisha wawekezaji sio kitu kizuri kufanya," alisema Dangote katika mkutano wa Afrika uliofanyika jijini London.


Dangote ni miongoni mwa wawekezaji Tanzania ambapo anamiliki kiwanda cha saruji chenye thamani ya Tsh 1.3 trilioni katika Mkoa wa Mtwara.


Waziri Mwijage alisema kuwa, wawekezaji katika Sekta ya Uchimbaji wanatakiwa kutoa umiliki wa asiliimia 16 kwa serikali ili kuhakikisha kuwa nchi inafaidika kutokana na rasilimali zake. Aliongeza waziri huyo kwamba, anategemea mtu kama Dangote ambaye ni mwekezaji mkubwa nchini, awe na uelewa kuhusu sheria za nchi.


"Kampuni inapokuja kuwekeza katika sekta ya uchimbaji, hisa za serikali hazitakiwi kuwa chini ya asilimia 16, na hili si kosa kabisa kwa sababu rasilimali ni zetu," alisema Waziri Mwijage.


Aidha, Waziri Mwijage alisisitiza kuwa atahakikisha wawekezaji wote nchini wanafuata sheria, na kwamba hakutegemea kama Dangote angekuwa mmoja wa watu ambao wangekosoa mazingira ya uwekezaji Tanzania.


“Dangote amekuwa hana tatizo hapa. Wakati wowote anapokumbwa na tatizo, serikali yote hukimbia na kumsaidia. Unakumbuka alipokuwa na tatizo mwaka jana, wote tulikuwepo kwa ajili ya kumsaidia,” alisema Waziri Mwijage.


Katika mkutano huo, Dangote alisema uhusiano wake na Rais Magufuli ni mzuri, lakini akamshauri kuangalia upya sera zake za uwekezaji.

The Citizen:

Wasanii wa Tigo Fiesta watembelea Duka la Tigo Iringa


Msanii Madee akisalimiana na mtoa huduma wa Tigo mara baada ya kuwasili dukani hapo.


Wasanii wakisalimiana na watoa huduma wa Tigo Iringa.


Wasanii wakiwa kwenye picha ya pamoja duka la Tigo Iringa

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...