Tuesday, 13 September 2016

DC IKUNGI AITAKA KAMPUNI YA SHANTA GOLD MINE KUWALIPA FIDIA WANANCHI WALIOFANYIWA TATHIMINI



Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa kikao cha pamoja kilichohudhuriwa na Wawakilishi wa kampuni ya Shanta Gold Mine Ltd, Wananchi wawakilishi kutoka Kijiji Cha Mlumbi na Uongozi wa kikosi kazi


Wananchi wawakilishi kutoka Kijiji Cha Mlumbi na Uongozi wa kikosi kazi wakijadili jambo nje ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya kabla ya kuingia kwenye kikao


Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd Philbert Rweyemamu akielezea namna ambavyo watawalipa wananchi 67 ndani ya wiki hii






Wananchi wawakilishi kutoka Kijiji Cha Mlumbi na Uongozi wa kikosi kazi wakisikiliza kwa makini maelezo ya mkuu wa Wilaya 




Kamishina wa Madini Kanda ya Kati Sospita Masorwa akielezea namna ambavyo uthamini unakuwa umekamilika kuwa ni mara baada ya Mthamini Mkuu wa serikali kupitisha


Kutoka kushoto ni Afisa Tarafa ya Ikungi Josephine, Kamishina wa Madini Kanda ya Kati Sospita Masorwa, Ally Kassim Mjiolojia kampuni ya Shanta Gold Mine Ltd, Meneja Mkuu Shanta Gold Mine Ltd Philbert Rweyemamu, David Rwechungura Meneja Rasilimali watu kampuni ya Shanta Gold Mine Ltd, na Daniel Mwita



















Na Mathias Canal, Singida


KAMPUNI ya Uchimbaji wa Madini ya dhahabu (Shanta Gold Mining Limited) iliyopo katika kijiji cha Sambaru Kata ya Mang’onyi Wilayani Ikungi, Mkoani Singida imetakiwa kuwalipa wananchi 69 waliosalia kulipwa fidia zao kwa ajili ya kupisha mradi wa uchimbaji dhahabu.


Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kufuatia malalamiko ya wananchi wa maeneo mbalimbali waliopo kwenye eneo la mradi huo waliotaka kufahamu hatima ya malipo yao kutokana na awamu ya kwanza kuonyesha kuwa watu 67 ndio watakaolipwa mwishoni mwa wiki hii na wengine waliobaki kulipwa katika awamu zijazo.


Dc Mtaturu ametoa agizio hilo wakati wa kikao cha pamoja kilichohudhuriwa na Wawakilishi wa kampuni ya Shanta Gold Mine Ltd, Wananchi wawakilishi kutoka Kijiji Cha Mlumbi na Uongozi wa kikosi kazi ambacho kilipewa jukumu la kuhakikisha wananchi wote ambao watapitiwa na mradi huo wanalipwa fidia sambamba na kusimamia uhamishaji wa makazi.


Kapuni ya Shanta Gold Mine ltd imetakiwa kutumia siku 68 yaani hadi kufikia mwezi Novemba mwaka huu kumaliza malipo ya watu 69 kati ya 136 ambao wanatakiwa kulipwa katika awamu ya pili ili wananchi hao waweze kupisha mradi huo ambao kwa kiasi kikubwa umeshindwa kuanza uchimbaji wa madini aina ya dhahabu kutokana na malalamiko ya malipo ya fidia kwa baadhi ya wananchi ambao tayari wamefanyiwa uthamini wa maeneo yao.


Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa wilaya ameagiza kikosi kazi kuendeleana kazi yake mpaka pale malipo ya wananchi hao yatakapokamilika pamoja na kuwapo kwa maneno kuwa kilivunjwa mwanzoni mwa mwezi wa tatu, jambo ambalo limepingwa vikali na uongozi huo wa Wilaya.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd Philbert Rweyemamu amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi hao juu ya kutaka wananchi wote walipwe kwa wakati mmoja jambo ambalo sio rahisi kutokana na pesa iliyopatikana kutoka kwa wawekezaji wa hisa tangu mwaka 2012 mpaka sasa bado inatumika haijaanza kuingiza faida hivyo malipo ya awamu yatakuwa muarobaini wa malipo hayo mara baada ya kuanza kwa uchimbaji hivyo kadri mradi unavyoendelea kuchelewa kuanza ndivyo ambavyo fedha inapoteza thamani.


Hata hivyo amejibu hoja ya wananchi kuwa Kampuni hiyo ndiyo ilileta Mthamini wa maeneo ya wananchi jambo ambalo halina ukweli halisi kwani wananchi wenyewe ndio walioamua juu ya Mthamini wanayemtaka kutokana na makubaliano yao.


Rweyemamu alisema kuwa endapo kama mradi huo ungeanza mapema kama vile ilivyokuwa imepangwa ni dhahiri sasa ungekuwa umezalisha ajira zaidi ya mara tano kwa wakazi wa maeneo husika na Taifa kwa ujumla jambo ambalo lingerahisisha kuongeza pato la wananchi wa Wilaya husika na Taifa kwa ujumla.


Naye Mwenyekiti wa wananchi walio katika eneo la mradi huo Ramadhani Said Nyeri amesifu juhudi za utendaji kazi wa serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kumteua Mkuu huyo wa Wilaya ambaye anaonyesha maslahi mapana na wananchi kutokana na juhudi mbalimbali za utendaji kazi.


Pamoja na pongezi hizo Nyeri amesema kuwa endapo viongozi mbalimbali wa serikali watafanya kazi kwa mazoea kwa kutumia vibaya nafasi zao ni dhahiri kuwa lawama na malalamiko ya wananchi yatakuwa laana kwao.

Nyeri alisema kuwa kikosi kazi hicho kilianza kazi hiyo mwaka 2014 ambacho kilianzishwa na Kampuni ya Shanta gold Mine ltd kwa makubaliano na wananchi wa maeneo husika ambapo katika kipindi chote hicho vimefanyika vikao vitano ambavyo viliendeshwa vyema pasina malalamiko kwa upande wowote ule.


Akifunga kikao hicho Dc Mtaturu alisema kuwa katika makubaliano ya namna ya kuendesha utendaji kazi wa kikosi kazi hicho mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Tundu lissu alipaswa kuwepo lakini hajawahi kushiriki hata kikao kimoja jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaashiria mbunge huyo kukimbia majukumu yake kama muwakilishi wa wananchi.






Aidha amekipongeza kikosi kazi hicho kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya kwa kipindi chote hicho huku akiitaja miaka 10 waliyofanya kazi kumekuwa na daraja kutokana na baadhi ya viongozi kukimbia majukumu yao na kuwaacha wananchi kujishughulikia na kumaliza matatizo yao wao wenyewe.


WASOMI WAIPONGEZA MeTL GROUP KWA KUFANYA CAREERS FAIR, 25 KUPATA AJIRA




Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd, Hassan Dewji akizungumza wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.




Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akizungumzia idara yake ya masoko inavyofanya kazi wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.



Mtaalamu wa kilimo wa kampuni ya MeTL Group, Bw. George Mwamakula akizungumza wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.



Mtaalamu wa masuala ya fedha wa MeTL Group, Bi. Hasina Ahmed akizungumza wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.



Mtaalamu wa idara ya uzalishaji wa nyuzi na nguo ya MeTL Group, Bw. Clement Munisi akizungumza wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.










Mtaalamu kutoka kitengo cha mauzo wa MeTL Group, Bw. Yusuf Ali, akizungumza kwenye Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.




Mtaalamu wa idara ya uzalishaji na matengenezo wa MeTL Group, Bw. Vijay Raghavan akizungumza kwenye Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.









Washiriki wakiuliza maswali juu uendeshaji wa vitengo mbalimbali vya makampuni ya MeTL Group wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.








Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd, Hassan Dewji akijibu maswali yaliyoulizwa na washiriki wa kongamano hilo.



Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer (katikati) akikabidhi box la zawadi kwa mmoja wa washiriki aliyejishindia kwenye mchezo wa kuokota majina wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd, Hassan Dewji.






Na Mwandishi Wetu


Safari ya Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) kutoa ajira kwa Watanzania 100,000 hadi mwaka 2021 imeanza kufanyika kupitia Job Affairs ambapo limewapa nafasi wasomi mbalimbali nchini kutumia sehemu hiyo kuonyesha uwezo wao, na kati yao wasomi 25 wakipata nafasi ya kujiunga na familia ya zaidi ya wafanyakazi 28,000 wa kampuni ya MeTL Group.



Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanyika kwa kongamano hilo, wasomi mbalimbali waliipongeza kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited kwa kufanya kongamano la Job Affairs kwani licha ya kutoa nafasi za kazi lakini pia limewasaidia kujijengea uwezo mpya ambao hawakuwa nao awali.


Mmoja wa wasomi hao, Dennis Mtani alisema kupata nafasi ya kuhudhuria kumewajengea jambo lipya kuhusu jinsi ya kuomba nafasi za kazi hadi kuwa wafanyakazi bora katika kampuni.


Alisema kutokana na ukubwa wa kampuni ya Mohammed Enterprises kwa bara la Afrika ni matarajio yao kuwa wamejifunza jambo ambalo hata kama hawatapata nafasi za kazi basi watabaki na uwezo ambao utawasaidia kujua jinsi ya kuomba nafasi katika makampuni mengine ya kimataifa.


“Tumekuja katika kongamano hili wengine hata CV walikuwa hawajui jinsi ya kuandika ili kuomba nafasi na kuajiriwana na kutokana na ukubwa wa hii kampuni kwa nchi za Afrika tumepata elimu ambayo inaweza kutusaidia kwenda kufanya kazi kwa makampuni mengine,” alisema Mtani.


Nae Monica Mziray alisema alijumuika katika kongamano hilo ili kujaribu kutafuta nafasi ya kujiunga na kampuni ya Mohammed Enterprises kwani anaamini ni kampuni kubwa ambayo anaamini ana ndoto za kuifanyia kazi na ambayo inawajali wafanyakazi wake.

“Nimefanya kazi na kampuni zingine lakini niliacha sababu nataka kampuni ambayo inanilia vizuri na inanipa kitu na mimi naipa kitu, nilisoma historia ya Mohammed Enterprises, nimeona ni kampuni kubwa Afrika, nimeona bidhaa zake na naona inaweza niongezea kitu,” alisem Mziray.


Aidha akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Rasilimali wa Mohammed Enterprises, Hassan Dewji aliwambia washiriki ambao wametoka katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu, kwamba Idara ya Rasilimali Watu ya MeTL imekua ikitoa ajira, mafunzo ya kukuza vipaji kwa watanzania wa kada mbalimbali ili kuchukua nafasi za juu katika Makampuni shiriki ya MeTL.






Kuhusu kongamano hilo la kazi alisema linalengo la kupata wasomi wenye taaluma mbalimbali kutoka kwa vijana wa Kitanzania. Kwamba Idara ya Rasilimali Watu imelenga kupata wahitimu katika nyanja za Uhasibu wa fedha, Rasilimali watu, Masoko, Uhandisi, Kilimo na Viwanda vya nguo lakini pia vijana wasomi watapewa mafunzo kwa kipindi cha wiki 52 huku wakiwa wanalipwa na watakapomaliza mafunzo watapewa ajira na kuingizwa katika mfumo wa uwajibikaji.






“Kundi la Makampuni ya MeTL limepata umadhubuti wake kutokana na kuwa na utamaduni wa kuhakikisha kwamba wanakuwa karibu na wafanyakazi wake na kuwajali. Wafanyakazi wa Idara ya Rasimali Watu wamekua wakiandaa mafunzo kuboresha elimu ya wafanyakazi, maarifa na utaalamu,






“Ushiriki wa wafanyakazi ni sehemu ya maono ya wafanyakazi wa Idara ya Rasilimali Watu katika kundi hili la makampuni. Kampuni hii huhakikisha kwamba wafanyakazi wanapata mapumziko, kujitengeneza upya, wanakuwa na siku ya familia, siku ya michezo na kwamba shughuli hizo zinafanywa kwa mpangilio ili kuwezesha kuwepo kwa utamaduni wa familia moja inayofanya kazi kwa kushirikiana kwa kiwango cha juu,” alisema Dewji.


SEMINA KUBWA YA KARATE AFRIKA MASHARIKI, KATI NA KUSINI YAANZA JIJINI DAR




Senpai Esther Thomas (kushoto) akipangua chudan tzuki (ngumi ya kifua) wakati semina hiyo ikiendelea.




Anafundisha kwa mifano! Shihan Okuma akishambuliwa na Jerome Sensei kama sehemu ya maelekezo katika semina hiyo






Na Daniel Mbega




SEMINA kubwa ya Shotokan Karate kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini, imeanza leo hii jijini Dar es Salaam ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya mchezo huo nchini Tanzania, inaongozwa na mkufunzi mkuu, Shihan Koichiro Okuma (6th Dan), kutoka makao makuu ya chama cha karate cha Japan Karate Association/World Federation (JKA/WF), Tokyo, Japan.

Semina hiyo – maarufu kama JKA/WF- Tanzania Southern, Central & East African Region Gasshuku – ambayo imeandaliwa na chama cha Japan Karate Association/World Federation-Tanzania (JKA/WF-Tanzania) ni ya nane kufanyika ambapo kwa mwaka huu inashirikisha makarateka 45 kutoka Zimbabwe, Zambia, Uganda, Kenya na wenyeji Tanzania.


Kwa mujibu wa JKA/WF-Tanzania, semina hiyo ya wiki nzima inatarajiwa kufikia tamati Jumamosi.




Makarateka ambao wameanza kushiriki leo hii, kutoka Tanzania ni Jerome Mhagama Sensei, Justine Limwagu, Seberian Dagila, Said O. Kissailo, Lulangalila Lyimma, Athumani Kambi, Mikidadi Kilindo Sensei, Marcus George, Khamis K. Sambuki, Hamis Said Mkumbi, Selemani A. Mkalola, Christopher William, Eliasa Mohammed, Adson Aroko Sensei, Nestory Federicko, Daniel Mbega, Willy Ringo Rwezaura Sensei, na Shihan Dudley Mawala Sensei, ambaye alikuwa mgeni mwalikwa.




Makarateka wengine na nchi zao kwenya mabano ni Gibson Sangweni (Zimbabwe), Robert Chisanga (Zambia), Thobias B. Rudhal (Kenya), George Otieno (Kenya), Joshua Oude (Kenya), George Warambo (Kenya), George Okeyo (Kenya), Florence Kieti (Kenya), Asana Mahmoud Ulwona (Uganda), Ofubo Issa Yahaya (Uganda), Magezi Yasiin (Uganda), Wanyika Abdurahman (Uganda), Frederic Kilcher (Ufaransa) na Koichiro Okuma (Japan).




Mkufunzi mkuu wa JKA/WF-Tanzania, Jerome George Mhagama Sensei (5th Dan), amesema hata hivyo kwamba, tofauti na miaka iliyotangulia, safari hii hakutakuwa na mashindano ili kutoa fursa kubwa kwa Shihan Okuma kufundisha vyema na kuwapandisha madaraja makarateka mbalimbali kuanzia ngazi ya Sho-Dan, Ni-Dan, San-Dan na Yon-Dan (1st – 4th Dan).




“Tunataka tupate muda wa kutosha wa kufanya semina pamoja na mitihani, kwani mbali ya kuwapandisha madaraja makarateka mbalimbali, lakini pia kuna ambao watafanya mitihani ya ukufunzi na uamuzi wa kimataifa ili kupanua wigo na kupata walimu na waamuzi wa kutosha katika kanda yetu,” amesema Jerome Sensei, ambaye alipanda daraja Jumanne, Septemba 6, 2016 baada ya kufanya vizuri na kufaulu mtihani wa 5th Dan jijini Nairobi, Kenya chini ya Shihan Okuma.




Hata hivyo, idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kesho ambapo makarateka kutoka Zanzibar nao watahudhuria baada ya kushindwa leo kutokana na sababu mbalimbali.




Jerome Sensei amesema kwamba, changamoto kubwa ambayo inawakabili wao pamoja na mchezo mzima wa Karate nchini Tanzania ni kuwekwa pembeni na wadau mbalimbali wa michezo ikilinganishwa na michezo mingine, hali ambayo imekuwa vigumu kwao kupata udhamini.




Ameiomba Serikali na wadau wengine kuutupia macho mchezo huo, kwani unailetea sifa kubwa Tanzania kutokana na mafanikio ya mchezaji mmoja mmoja.




Katika kipindi cha miaka takriban 10, Tanzania imekuwa kinara wa mchezo wa Karate katika kanda ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini ukitoa Afrika Kusini pekee, hatua ambayo imechangiwa na mafanikio binafsi ya Jerome Sensei, ambaye kwa jitihada zake ameshiriki mashindano ya dunia ya Karate mwaka 2012 na kurudia raundi ya nne, mashindano ambayo yalifanyika Pataya, Thailand, ambapo alitolewa na mtu ambaye alikuja kuwa bingwa wa dunia.




Mbali ya hivyo, ameshiriki mashindano mengine jijini Tokyo, Japan lakini pamoja na kutotwaa ubingwa, ameweza kupanda madaraja kwa viwango vya kimataifa na sasa ni mkufunzi, mtahini na mwamuzi wa kimataifa, ambapo ameweka rekodi ya pekee kwa kuwa mkufunzi mwenye umri mdogo kabisa katika historia ya JKA/WF tangu chama hicho kilipoanzishwa Mei 1947.




Kwa mujibu wa rekodi za JKA/WF, Jerome Sensei (36) ni karateka wa pili wa Afrika Mashariki kuwa na hadhi ya Dan Tano (5th Dan) baada ya David Mulwa Sensei wa Kenya, hivyo ameteuliwa kuwa mkufunzi mwenza mkuu wa Afrika Mashariki.




Akizungumza katika ufunguzi huo, Shihan Okuma, ambaye ametokea Kenya ambako kulikuwa na semina wiki iliyopita, amesema kuwa ujio wake siyo wa bahati mbaya bali umetokana na jitihada ambazo Tanzania imekuwa ikionyesha katika maendeleo ya Karate, hususan mafanikio yasiyo na kifani ya Jerome Sensei.




“Nimetumwa na makao makuu kuja kuiunga mkono Tanzania pamoja na kufundisha semina hii, najua semina kama hii mara nyingi huwa inafanyika makao makuu tu au katika kanda maalum, lakini kwa vile Tanzania imeonyesha mafanikio makubwa, hatuna budi kuja hapa ili kuwapa fursa makarateka wengi waweze kushiriki.




“Kuja Japan ni gharama kubwa, wengi hawawezi kumudu pamoja na kuwa na nia na mchezo huu, ni wachache tu ambao wanapata bahati ya kuja kuhudhuria, lakini hapa nimefurahi kuona kuna makarateka wengi wana viwango vya juu kabisa na hii ni faraja kubwa kwangu na kwa JKA/WF,” amesema.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...