Saturday, 22 April 2017

KAMATI MALALUM YA TFF KUSIMAMIA UCHAGUZI WA LIPULI FC YA MJINI IRINGA




Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeunda kamati maalum kwa ajili ya kusimamia uchaguzi wakupata viongozi wapya wa klabu ya mpira ya Lipuli ya mjini Iringa inayoongozwa na mjumbe wa kamati ya uchaguzi TFF Hamimu Mahmud Omary (mwenye kaunda suti) (Picha na Friday Simbaya).

Katibu mpya wa CCM mkoa wa Iringa, Christopher Magala akizungumza na waandishi wa habari mkoani Iringa jana kuhusu kuutunza na kuulinda uwanja Samora. (Picha na Friday Simbaya)

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeunda kamati maalum kwa ajili ya kusimamia uchaguzi wakupata viongozi wapya wa klabu ya mpira ya Lipuli ya mjini Iringa, imeelezwa.

Hatua hiyo imekuja baada yakuwepo mgogoro usiokwisha ndani ya klabu hiyo, na kupelekea TFF kufuatilia kwa kina mgogoro wa kiuongozi ndani ya klabu ya Lipuli FC ya Iringa.

Baada ya uchunguzi wake,TFF imetoa maagizo manne yafanyike mara moja.

1. Klabu ya Lipuli ifanye uchaguzi mkuu wa kupata viongozi wake.
2. Kamati ya uchaguzi ya TFF itasimamia mchakato mzima wa uchaguzi huo.

3. Uchaguzi huu utafanyika kwa mujibu wa Katiba ya Lipuli FC uliofanyika tarehe 22 Juni 2014.

4. Kamati ya uchaguzi ya TFF itahakiki na kutoa orodha ya wapiga kura.

Akizungumza na waandishi wa habari mjumbe wa kamati ya
uchaguzi TFF Hamimu Mahmud Omary alisema zoezi la kuchukua fomu kwa wagombea limefungulia leo (jumamosi) ambapo tarehe uchaguzi itakuwa 29/05/2017.

“Mchakato wa kuchukua fomu umefunguliwa tarehe 22/04/2017 hadi 28/04/2017 na wanachama wanaruhusiwa kuchukuwa fomu na kugombea nafasi zilizotangazwa...,” alisema Omary

Alisema tayari Kamati ya Uchaguzi ya TFF imepewa jukumu la kusimamia uchaguzi wa Klabu ya mpira wa miguu ya Lipuli FC na fomu zinapatikana katika Uwanja wa Kumbukumbu wa Samora, mjini Iringa.

Omary alisema kuwa fomu zinapatikana kwa gharama ya Sh 200,000/- kwa nafasi za mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu mkuu na makamu katibu mkuu, kwa nafasi za na mweka hazina na makamu mweka hazina kwa wagombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ada ya fomu Sh 100,000/-.

Alisema kuwa orodha ya rejesta ya wanachama ni 109 nawatakiwa kulipa ada ya mwaka ndio watakaoruhusiwa kupiga kura kwa sasa.

Alizitaja sifa za mgombea uongozi wa klabu ya lipuli kuwa ; awe ni raia wa Tanzania, awe amesoma kidato cha nne na kufaulu au elimu ya juu zaidi ya hapo, awe na uzoefu angalau miaka mitano katika mambo ya utawala wa mchezo wa mpira wa miguu na awe hajawahi kukutwa na hatia ya kosa la jinai na kuhukumiwa kufungwa bila ya kutolewa adhabu ya faini.

Sifa zingine awe na umri usiopungua miaka 25, awe na uwezo, heshima, uadilifu na haiba ya kuweza kuiwakilisha klabu ya lupuli ndani na nje ya mkoa wa Iringa na Tanzania, na asiwe mwamuzi wa mpira wa mguu anayefanya shughuli za uamuzi kwa kipindi hiki.

Wakati huohuo, CHAMA cha Mapinduzi mkoa wa Iringa (CCM) wanaomiliki uwanja wa mpira wa miguu wa Samora wamesema wanatarajia kuwatumia wataalamu wa michezo katika kuutunza na kuulinda uwanja huo uweze kudumu katika ubora wake kwa kipindi kirefu.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake jana Katibu mpya wa CCM mkoa wa Iringa, Christopher Magala alisema kuwa mara baada ya uwanja huo kukamilika watahakikisha wanawatumia wataalamu mbalimbali wenye elimu ya michezo kuweza kutoa huduma wakishirikiana na meneja wa uwanja, Lazaro Manila.

Alisema kuwa wanatarajia kuunda timu ya wataalamu ambao watahakikisha uwanja unaendelea kudumu katika ubora wake kwa kipindi kirefu bila kuharibika kwani kuna vongozi mbalimbali ndani ya ccm ambao wana elimu ya kutosha katika kuhakikisha uwanja unakuwa bora kuanzia eneo la kuchezea hadi majukwaani.

Magala alisema kuwa uwanja huo ambao unatarajia kukamilika hivi karibuni na kuwa moja ya viwanja vya michezo bora nchini Tanzania unatakiwa kutumiwa katika matumizi yanayohitajika ili kuweza kuulinda na usiweze kuharibika katika eneo la kuchezea na sehemu ya jukwaa ambalo litafanyiwa ukarabati mkubwa.

“Uwanja wa Samora baada kukamilika utakuwa moja ya viwanja vinavyokubalika na tunatarajia hata mechi za kimataifa zitachezewa uwanjani hapa hivyo matunzo yake yanatakiwa kuwa ya kisasa na kubwa tutatumia menejementi inayotambua mambo ya michezo katika kuweza kuhudumia na kuutunza uwanja huu” alisema

Alisema kuwa licha ya kukamilika kuzungushiwa fensi ndani ya uwanja na kukamilika kwa vyumba vya kubadilishia nguo vya wachezaji, mageti ya kuingilia watahakikisha uwanja unatumika kwa malengo yake ili udumu na wataalamu watakaoajiriwa watatumika kutoa maelekezo.

Alitoa wito kwa wadau mbalimbali mkoani hapa kuutumia uwanja wa Samora kistaarabu na kuachana na ile kasumba ya kuharibu kitu ambacho kinaleta gharama kubwa katika kuufanyia ukarabati na matamasha mingine yote yatafanyika uwanjani hapo pembezoni mwa sehemu ya kuchezea.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...