Pamoja kwamba kuna kibao kinachokataza kutofanya shughuli zozote zile katika ofisi ya maliasili na utalii, wananchi hao walikutwa wakutenganeza gari eneo hilo bila kujali ilani ya kibao kama mpigapicha wetu alivyowakuta wakifanya shughuli katika Mtaa ya Ujasili (Ujasili Road) Mlangege Gereji Manisapaa ya Iringa, mkoani Iringa.
Monday, 9 May 2016
AZANIA BENKI YASHEREHEKEA SIKU YA MAMA KWA KUGAWA DAWA NA VIFAA VYA USAFI HOSPITALI YA AMANA
Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara wa Benki ya Azania, Mwanahiba Mzee (kulia), kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa benki hiyo, akimkabidhi kiongozi wa wagonjwa wa ndani wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Francis Yango (kushoto), dawa na vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh.milioni 5 vilivyotolewa na benki hiyo ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake Dar es Salaam leo asubuhi. Wapili kulia ni Muuguzi wa zamu,Getrude Massawe na Antusa Lasway.
Wafanyakazi wa benki ya Azania wakiwa mbele ya vifaa na dawa walivyotoa msaada kwa Hospitali hiyo.
Hapa ni furaha tupu kabla ya kukabidhi msaada huo.
Mwonekano wa maboksi yenye msaada huo baada ya kupokelewa.
Vifaa hivyo vikipelekwa kwa walengwa.
Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara wa Benki ya Azania, Mwanahiba Mzee (kushoto), akimkabidhi dawa za meno na sabuni, Judith Kimei katika wodi ya wazazi. Kulia ni Muuguzi wa zamu Antusa Lasway.
Ofisa wa benki hiyo, Neema Tumsifu akimjulia hali mtoto aliyezaliwa katika wodi hiyo.
Wafanyakazi hao wa Bebki ya Azania wakiondoka Hospitalini hapo baada ya kukabidhi msaada huo.
BENKI ya Azania imetoa msaada wa dawa na vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. milioni 5 katika Hospitali ya Rufaa ya Amana Ilala Jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo wakati wa kukabidhi msaada huo Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara, Mwanahiba Mzee alisema kila mara benki hiyo imejiwekea utaratibu wa kusaidia jamii kulingana na ratiba yao ambapo mwaka huu waliona ni vema msaada huo waupeleke Hospitali hiyo.
Alisema mwaka katika kusherehekea sikukuu ya wanawake waliona ni vema kutoa msaada hasa katika wodi ya wajawazito ukizingia kuwa sikukuu hiyo inawahusu.
"Tumetoa msaada wa dawa mbalimbali kama dettol, spiritis, mabomba ya sindano, micoprostol, vitamini k na nyingine nyingi pamoja na vifaa vya usafi kama vile mifagio, sabuni na dawa za mswaki" alisema Mzee.
Kiongozi wa wagonjwa wa ndani wa Hospitali hiyo, Francis Yango akizungumza wakati wa kupokea msaada huo kwa niaba ya Mganga Mkuu, Shadrack Shimwela aliishukuru benki hiyo na kuwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia.
"Tunawashukuru sana Azania Bank Ltd kwa msaada wenu lakini tunawaomba muende mbele zaidi kama mtaweza mtujengee walau wodi ambayo itaingiza walau vitanda 30 na wodi hiyo muandike jina la benki yenu kwani changamoto kubwa tulionayo kwa sasa licha ya kuwa na vitanda vya kutosha tuna uhaba wa wodi" alisema Yango.
HATIMAYE CHAMA CHA ADC CHAFANYA MKUTANO MKUU,MSAJILI AWAMWAGIA PONGEZI
Waziri wa kilimo wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar amnbaye ni mlezi wa chama cha ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE -ADC nchini Tanzania Mh HAMAD RASHID akihutubia wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho unaofanyika Jijini Dar es salaam leo(Picha na EXAUD MTEI)
Baada ya chama cha ALIANCE FOR DEMOCTARIC CHANGE –ADC kuingia katika migogoro ya kiuongozi ndani ya chama hicho siku za hivi karibuni Hatimaye hali ya Amani imerejea ambapo chama hicho leo kimeingia katika mkutano mkuu uliowakutanisha wajumbe mbalimbali kutoka kila kona ya nchi.
Katika mkutano ambao umehudhuriwa na viongozi wakuu wa chama hicho akiwemo waziri wa kilimo wa serikali ya Zanzibar ambaye alikuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho ambaye pia ndiye mlezi wa chama Mh HAMAD Rashid,viongozi kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na wajumbe mbalimbali wa chama hicho.
Makamu mwenyekiti wa ADC Mama ADELA STOLIC akihutubia wakati akifungua mkutano huo Mkuu mapema leo
Akizngumza wakati wa Ufunguzi wa mkutano huo HAMAD RASHID amesema kuwa chama cha ADC ni chama ambacho kimeanzishwa kwa ajili ya kuwasaidia watanzania,kikiwa na itikadi zake,sera zake na mipango yake hivyo hakipo tayari kufwata sera za chama kingine chochote nchini na swala la kushiriki chaguzi mbalimbali ni moja kati ya sera zao hivyo hawapo tayari kususia uchaguzi wa aina yoyote kwani ndio njia pekee ya kupata viongozi wa nchi.
Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa nchini A SISTY LEORNAD NYAHOZI akitoa hotuba fupi kwa niaba ya msajili wa vyama vya siasa nchini
Ameleza kuwa chama chake kimeanza mipango kabambe ya kujiimarisha Zaidi kwa lengo la kuwaletea mabadiliko ya kweli watanzania baada ya wapinzani wao waliokuwa wakiongoza serikali iliyopita na sasa hawapo kushindwa kufanya hivyo kwa miaka yote iliyopita hivyo amewataka watanzania kuanza kukiamini chama cha ADC kwani ndio dira pekee ya mabadiliko kwa watanzania kwa sasa.
Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa viongozi wa chama hicho mara baada ya kuondolewa kwa aliyekuwa mwenyekiti wa chama kiongozi huyo amewataka wanachama wa chama hicho wakae tayari kwa kuwa siku yoyote chama kitaitisha uchaguzi wa kupata viongozi wapya.
Naye msajili msaidizi wa vyama vya siasa nchini Mh SISTY LEORNAD NYAHOZI akizungumza katika mkutano huo amekipongeza chama hicho kwa kukubali kuingia katika uchaguzi wa marudio Visiwani Zanzibar ambapo walishika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 3 jambo ambalo amesema ni ukomavu wa kisiasa kwa chama kichanga kama hicho kushiriki uchaguzi mkubwa kama ule na kupata mafanikio hayo.
Aidha amesema kuwa chama hicho kimeonyesha ukomavu Zaidi baada ya kutokea mtafaruku na aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho na kufanikiwa kulimaliza kidemocrasia jambo ambalo amesema linafaa kuigwa na vyama vingine vya siasa nchini.
Chama hicho kilijikuta katika migogoro iliyosababisha hadi kutimuliwa kwa aliyekuwa mwenyekiti wake SAID MIRAAJ kwa kile kiliichoitwa kukiuka matakwa katiba ya chama ambapo ilielezwa kuwa mwenyekiti huyo alipinga kitendo cha viongozi wa chama kuingia katika uchaguzi wa Zanzibar wa marudio jambo ambalo alilipinga na kusababisha mtafaruku baina yake na aliyekuwa mgombea wa chama hicho visiwani Zanzibar ambaye kwa sasa ni waziri HAMAD RASHID
TIGO YASHIRIKIANA NA MADEREVA WA BODABODA UKEREWE
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph Mkirikiti,akihutubia madereva bodaboda wa wilaya yake jana wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa madereva hao na mtandao wa Tigo kwa ajili ya utendaji wao wa kutoa huduma ya usafiri ,Wa pili toka kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya ziwa, Ali Maswanya na Mkurugenzi wa Mikakati wa Tigo Kobbina Awuah(kulia)
Mkurugenzi wa Kanda ya ziwa wa mtandao wa Tigo Ali Maswanya, akizungumza wakati wa kuzindua ushirikiano wao na madereva Bodaboda Wilaya ya Ukerewe jana, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph Mkirikiti na Mkurugenzi wa Mikakati wa Tigo Kobbina Awuah(kulia)
Madereva Bodaboda Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza,wakinyoosha mikono juu kuashilia kuzinduliwa kwa umoja wao na Mtandao wa Tigo,kwenye hafla iliyofanyika
Baadhi ya bodaboda zikiwa nje ya eneo hilo la ukumbi wa Mmikutano Ukewe.
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...