Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mabaoni, Sailas Ndenga (kushoto) akipekea hati ya jengo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Green Resources Ltd, Anthony Kisondella wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika Kijiji cha Mabaoni, wilayani Mufindi, mkoani Iringa jana. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
Wananchi wa Kijiji cha Mabao, viongozi wa Green Resources Ltd pamoja na viongoizi wa serikali wakiwa nje jengo jipya lililojengwa na Kampuni ya GRL na kukabibidhiwa kwa serikali ya kijiji hicho baada ya hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika Kijiji cha Mabaoni, wilayani Mufindi, mkoani Iringa jana. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mufindi (DED) akihutubia wananchi wa Mabaoni.
Rai hiyo imetolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa GRL, Anthony
Kisondella kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Roselyne Mariki, wakati akikabidhi
jengo la ukumbi na ofisi kwa Kijiji cha Mabaoni katika Kata ya Makungu, wilaya ya
Mufindi, mkoani Iringa.
Kaimu mkurugenzi huyo aliwataka wananchi kutoa ushirikiano unaostahili na michango
iliyo ndani ya uwezo wao kama nguvukazi na vifaa kama mawe, matofali na
mchanga.