Vijana wa kijiwe wakupiga stori huku pembeni mwao kina mama wakifanya biashara ya kuuza ndizi za kuiva katika mtaa wa hospitali Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma leo mchana. Vijana wengi maeneo ya mengi ya mijini hushinda bila kufanyakazi yoyote kwa kutegemea maisha bora kutoka mbinguni, toba!. Ajira kwa vijana ni tatizo kubwa katika maeneo ya mijini hata vijijni na husababisha kuongezeka kwa vitendo vya wa uhalifu nchini na kutishia usalama nchini. Kwa hiyo ni wajibu wa serikali kuwawezesha vijana kiuchumi ili wawezekujitegea bila ya kusubiri 'White-Collar-Job' na hatimaye kuweza kupunguza tatizo la ajira nchini. Take care leaders.
Duh! Mama mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja akiwa ameuchapa usingizi pembeni mwa ukuta kwenye kivuli bada ya kusubiria wateja wake wakununua kandambili kutotokea katika barabara ya Songea-Mbinga Manispaa ya Songea leo. Ni kawaida katika Manispaa ya Songea kukuta wafanyabiashara wamepanga bidhaa zao kandokando mwa barabara, hivyo kusababisha msongomano mkubwa wa watu katika mitaa mbalimabali wakiwemo pia mama ntilie nao kuuza chakula hovyohovyo bila kuzingatia kanuni za afya na viongozi wa serikali ya manispaa wape tu wamelala usingizi bila ya kuweka utaratibu unaoeleweka. Take care.
Sasa ni msimu wa maembe, vijana wengi wanajiusisha na biashara kuuza maembe ili kuweza kujipatia vijiseti kama walivyokutwa binti huyo akiwa na wadogo zake pembeni, watoto hao walikutwa wakikimbilia wateja kwenye magari yanaopita jirani na kijiji chao huko Peramiho Songea vijijini Mkoa wa Ruvuma.
One woman was found sleeping under a shade nearby while she was selling slippers 'kandambili' with her not in the picture, but due to lack of customers coming to buy her merchandize (bidhaa) she decided take a little nap along Songea-Mbinga Road in Songea Town this afternoon.
Watoto wakiwa wanakimbilia gari lililosimama karibu na kijiji chao kwa ajili ya kuuza maembe kwa abiria bila ya kuzingatia sheria za barabarani ya namna ya kuvuka barabara vizuri ili mradi tu wauuze maembe katika kijiji kimoja ambacho kipo jirani na barabara ya kuenda 'Perahimo Mission Hospital' Songea vijijini leo jioni.
Saturday, 18 December 2010
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
Habari ndugu msomaji wetu wa blog, Natumaini unaendelea vyema. Leo tutaanza kujifunza kilimo cha bora cha nyanya, na tutaanza kufahamu vit...