Thursday, 3 December 2015
MEYA WA MANISPAA YA IRINGA KUZUNGUMZA NA WANAHABARI KESHO
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Iringa, ambaye pia ni diwani kata ya Isakalilo, Alex Kimbe (Chadema) pichani kesho saa 5 asubuhi ataongea na waandishi wa habari ofisini kwake, juu ya mustakabali ya Manispaa ya 2015-2020.
Diwani wa kata ya Isakalilo, Alex Kimbe (Chadema) jana alichaguliwa kwa kura 21 kuwa Meya wa Manispaa ya Iringa.
Kuchaguliwa kwa Kimbe kumemaliza mvutano wa ndani kwa ndani uliokikumba chama hicho wakati kikiwa katika mchakato wa kumpata mgombea wa nafasi hiyo na kumaliza historia enzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoa Meya kila baada ya Uchaguzi Mkuu.
Katika kinyang’anyiro hicho ambacho CCM walikuwa wasindikizaji kwasababu ya kuwa na idadi ndogo ya madiwani; mgombea wake Bashir Mtove alijipatia kura 6.
Mtove aliwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi na aliyekuwa Meya wa miaka mingi wa manispaa hiyo, Amani Mwamwindi ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, alishinda kwa kura chache kiti cha udiwani wa kata ya Mlandege dhidi ya mgombea wa Chadema, Richard Mfune.
Baraza hilo la madiwani lilimchagua pia Joseph Lyata wa Chadema kuwa Naibu Meya kwa kujinyakulia kura 21 dhidi ya kura 6 alizopata Dora Nziku wa CCM.
Awali katika salamu zake kwa madiwani hao, Katibu wa CCM Manispaa ya Iringa, Elisha Mwampashi aliwataka madiwani na halmashauri hiyo kufanya kazi, kupunguza tambo za barabarani na kushirikiana na wananchi kuleta maendeleo kupitia Ilani ya CCM.
Chadema imeunda halmashauri hiyo baada ya kufanikiwa kushinda kata 14 kati ya 18 za Jimbo la Iringa Mjini linaloongozwa kwa awamu ya pili na Mchungaji Peter Msigwa aliyemshinda mgombea wa CCM, Frederick Mwakalebela katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
CHAVITA wamuomba Rais Magufuli awakumbuke
CHAMA Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Tawi la Mkoa wa Iringa kimemuomba Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuhakiksha kuwa makundi yote maalumu yanapata haki sawa na mengine ili kuondoa dhana ya ubaguzi.
Akiongea na SIMBAYABLOG Katibu wa CHAVITA Mkoa wa Iringa Shaibu Juma ambapo alisema kuwa wanamshukuru Rais John Magufuli kwa kutoa kibali cha kufanya sherehe za siku ya Walemavu kitaifa Mkoani Mwanza.
Alisema kuwa kuna makundi mengine, yamekuwa yakiwezeshwa mara kwa mara aidha kupitia kwa mashirika yasiyo ya Kiserikali na hivyo kuweza kupata maendeleo kwa haraka na kumudu maisha yao ya kila siku.
Juma alisema kuwa katika Kampeni zake za kutafuta Urais Dkt. Magufuli alisema katika utawala wake hatabagua makundi maalum hasa wenye ulemavu katika uongozi wake hali ambayo imeonyesha dhahiri kuwa amedhamiria kuwasaidia.
“Tunampongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kuongoza Taifa la Tanzania na sisi kama makundi ya watu wenye Ulemavu tumeahidi kumpa ushirikiano wa hali ya juu kutokana na utendaji wake wa kazi hali ambayo itasaidia katika kuleta mabadiliko kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na kutekeleza kauli mbio ya “hapa kazi tuu,” alisema katibu hiyo wa CHAVITA.
Aidhi, katibu huyo alielezea masikitiko yake kwa Chama cha Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Mkoa wa Iringa kwa kushindwa kuviunganisha vyama vya watu kwenye walemavu mbalimbali mkoani hapa na kumemuomba Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuhakiksha kuwa makundi yote maalumu yanapata haki sawa na mengine ili kuondoa dhana ya ubaguzi.
Alisema tangu kuanzisha kwa tawi hilo la Chavita mkoa wa iringa mwaka 1994 hakijawahi kupata msaada wote kutoka kwa idara ya ustawi wa jamii mkoa, manispaa ya iringa pamoja na SHIVIWATA.
Kwa upande wake mjumbe wa CHAVITA Mkoa wa Iringa Alfred Emmanuel Chengula alisema kuwa ni vema kwa Serikali akangalia makundi kama hayo kwa sasa ili na wao pia wawe na uwezo wa kumudu changamoto nyingi zinazowakumba watu wa makundi ya Wenye ulemavu.
“Ni vema sasa kwa Serikali ya awamu ya tano Chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk,John Magufuli kuliangalia kwa jicho la kipekee kundi hilo na kuangalia changamoto mbalimbali zinazolikumba ili kuweza kuwawezesha kiuchumi na kuweza kumudu maisha yao ya kila siku,” alisema Mjumbe huyo.
Mjumbe mwingine aliyeambatana na katibu huyo wa Chavita ni pamoja na Zawadi Boniface aliyehoji kuwa ile asilimia kumi inayotenga na serikali kila mwaka kwa ajili ya watu wenye ulemavu inaenda wapi.
Tarehe 3, Desemba ya kila mwaka ni siku ya Watu wenye Ulemavu duniani. Siku hii inatokana na uamuzi wa Umoja wa Mataifa kui tangaza siku hii kuwa ni siku ya Watu wenye Ulemavu duniani kufuatia Azimio Na. 47/3 la mwaka 1992.
Tanzania kama nchi mwanachama imeridhia na kusaini mkataba huu, na imekuwa ikiadhimisha siku hii kitaifa katika mikoa toufati na mwaka jana maadhisho huyo walifanyika mkoani Iringa.
maadhimisho haya ni kwa lengo la serikali na wadau mbalimbali utambua uwezo wa Watu wenye U lemavu na kujenga mazingira yanayotoa fursa na ushiriki wao katika shughuli mbalimbali za maendeleo hapa nchini.
Kutangazwa kwa siku hii kumelenga kuinua u fahamu wa jamii kuhusu masuala ya Haki za Witu Wenye Ulemavu pamoja na kutoa fursa kwa Serikali za kila nchi duniani kutafakari juu ya utoaji wa huduma endelevu kwa nia ya kuinua hali za maisha ya Watu Wenye Ulemavu.
Australia Tanzania society donates hospital equipment to Mafinga Hospital
Mufindi district hospital is now going to reduce the problem of shortage of beds for the pregnant women, after the hospital receiving medical equipment and supplies from Australia Tanzania society (ATS) yesterday.
The overcrowding of pregnant women in the maternity ward with the shortage of beds at the hospital has forced the pregnant women to sleep more than one in one bed and others are left sleeping on the floor.
Speaking to the journalist yesterday the acting medical officer in charge Dr. Abdul Mussa Msuya said that the donation will go a long way in reducing some of the problems the hospital was facing on a daily basis.
He said that lack of hospital equipment and medical supplies was a major barrier for doing surgical operations and limitation of nurses and midwives is also another challenge but with that donations it will help minimize the huge challenge that they face on daily basis.
Dr. Msuya said the hospital is at the moment facing the big challenges of doctors, health workers in all cadres, buildings and a laundry machine for washing hospital bedding.
Although he did not specify the number of doctors and health workers the hospital needed, he said that his hospital is badly in need of health workers in all cadres.
He said the hospital is also facing the challenge of overcrowding of patients because it is the only big hospital in the district.
"The hospital receives more than 130 outpatients’ everyday and it has the capacity of accommodating 237 inpatients due to the limited number of beds in wards, which means the hospital needs more buildings for wards," he said.
However, the newly elected Member of Parliament for Mafinga Town Constituency, Cosato Chumi has handed a number of hospital equipment and medical supplies to the district hospital yesterday.
He said the donation came from their development partner called Australia Tanzania Society (ATS) through Rafiki Surgical Missions which includes beds, mattresses, trolleys, wheelchairs, crutches, walking frames and many others.
Chumi said that ambition is to see help the community in Mafinga and Mufindi residents excel in health and water sectors as their major challenges the people is facing.
Rafiki Surgical Missions is part of the Australia Tanzania Society, an Australian and Tanzanian is a non-government organization.
Rafiki's mission is to help Tanzania deal with its reconstructive surgery needs whilst at the same time assist in capacity building through the transfer of surgical, anesthetic, physiotherapy and nursing skills to medical professional in Tanzania.
In an effort to help alleviate severe shortages in medical and hospital equipment, Rafiki also aims to provide much-needed equipment to hospitals and medical facilities in Tanzania.
RAS: Fufuani mifumo ya kukagua maziwa ili kulinda afya ya mlaji
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, (RAS) Wamoja Ayubu ametoa wito kwa wakaguzi wa maziwa kutoka mikoa ya iringa, njombe na mbeya kuwa jukumu la ukaguzi wa maziwa ni kazi yao ya msingi na sio kazi ya ziada kwao.
Alisema kuwa jukumu la ukaguzi wa maziwa kwa wakaguzi sio kazi ya ziada bali ni kazi yao ya msingi na kusisitiza watoe ushirikiano wa dhati kwa bodi ya maziwa na mradi wa uendelezaji sekta ya maziwa afrika mashariki (EADD II), ili kujenga na kuimarisa vituo vya mauzo ya maziwa.
RAS huyo alitoa rai hiyo jana wakati akifungua mafunzo ya siku nne ya wakaguzi wa maziwa kutoka mikoa ya iringa, njombe na mbeya yaendelea mkoani Iringa.
Alisema kuwa kukagua maziwa ni muhimu sana kwakuendeleza tasnia ya maziwa na kulinda afya ya mlaji na hasa kwa viwanda ili kuweza kusindika maziwa wanahitaji maziwa yaliyo na viwango vya juu vya ubora.
“Napenda pia nichukue nafasi hiikuwahamasisha halmashauri zote nchini kuanzisha au kufufua mifumo ya kukagua maziwa ili kulinda afya ya mlaji,” alisema Ayubu.
Alisema kuwa katika sheria za kulinda afyaya mlaji wa maziwa nchini Tanzania zipo sheria mbalimbali kama vile sheria ya maziwa ‘The Dairy Industry Act, 2004, Tanzania food, drugs and cosmestics Act, 2003, the local government act, 1982 na ‘the public health act,1992, sheria zote hizo zina lengo kuu ka kuhakikisha maziwa yanashughuliwa kwa usafi na kumfikia mlaji yakiwa bora na salama.
lisema kuwa serikali ina jukumu la kumwahakikisha mlaji anapata maziwa bora na salama na bila ya udanganyifu kama kuchanganywa maji na pia kudanganywa kwenye vipimo.
“maziwa ni kinywaji na ni chakula muhimu katika mwili wa binadamu, kwani ni katika maziwa ndiko unapopata virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini kwa wakti mmoja. Maziwa ya protini, wanga, vitamin na madini ya aina nyingi,” alisema.
Soko la mawaziwa linashikiliwa namfumo wa soko lisilo rasmi ambalolinaaendeshwa na wachuuzi na wafanyabiashara wadogowadogo ambao huuza kati ya lita 20-100 kwa siku kutoka kwa wafugaji wadogo na mara nyingi wanatumia baiskeli kwa kusafirishia na kusambazia maziwa yakiwa ghafi.
MRATIBU WA UN NCHINI, ALVARO RODRIGUEZ ZIARANI MKOANI SINGIDA KUKAGUA MIRADI YA SHIRIKA HILO
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone alipomtembelea na kufanya mazungumzo ofisini kwake jana mjini Singida.
Na Modewjiblog team, Singida
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone ofisini kwake kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wa utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mkoani humo.
Mratibu huyo yupo Mkoani hapa kwa siku mbili kukagua miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Katika siku yake ya kwanza atatembelea mradi wa afya ambao unashughulikia watu wanaoishi na VVU katika kijiji cha Puma wilaya ya Ikungi. Pia atatembelea kikundi cha ufugaji nyuki kinachojihusisha na uzalishaji wa asali na utengenezaji wa mishumaa.
Aidha akiwa kijiji cha Puma atatembelea kambi waliokolazwa watu wenye ugonjwa wa Kipindupindu.
Katika ukaguzi wa miradi hiyo Mratibu huyo atapata nafasi ya kuzungumza na walengwa wa miradi hiyo ili kupata mafanikio na changamoto zilizojitokeza.
Katika siku yake ya pili na ya mwisho mkoani Singida Bw. Alvaro Rodriguez atatembelea mradi mkubwa wa ufugaji nyuki kisasa unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP).
Baada ya hapo atatembelea ujenzi wa hospitali ya rufaa inayoendelea kujengwa kijiji cha Mandewa nje kidogo ya mji wa Singida.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone alitoa Shukrani kwa Umoja wa Mataifa kwa misaada yake ya kuisaidia serikali katika kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Hata hivyo ameomba Mashirika hayo yaendelea kusaidia katika Nyanja za upatikanaji wa ajira kwa vijana na masoko kwa wakulima.
Mratibu huyo baada ya kumaliza ziara yake mkoani Singida ataelekea mkoa wa Tabora ambapo ataanza ziara yake tarehe 3 mwezi Desemba na baada ya kumaliza mkoa wa Tabora atelekea mkoani Kigoma tarehe 4 hadi 6 nwezi Desemba.
Singida ni kati ya mikoa itakayounufaika na mpango mpya wa malengo ya maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals-SDGs) unaotarajiwa kuanza kutekelezwa 2016-2030.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone akisalimiana na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kulia) aliyeambatana na Bw. Rodriguez. Aliyeketi ni Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Festo Kang'ombe.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone (wa kwanza kulia) akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (wa tatu kushoto) pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mkoani humo. Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Singida, Mdala Fedes. wengine pichani ni Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Festo Kang'ombe (wa kwanza kulia).
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone akisoma baadhi ya mambo yaliyomo kwenye kitabu cha 'Mwongozo wa wadau wa kilimo na mifugo' kilichoandaliwa na ofisini kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani). Kulia ni Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Festo Kang'ombe.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu akitoa maelezo ya lengo namba 3 ambalo ni 'Afya Njema na Ustawi' wakati wa kutambulisha malengo mapya ya maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals-SDGs) kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone walipomtembelea ofisini kwake jana.
Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Festo Kang'ombe akioorodhesha mambo muhimu yanayotakiwa kufanyika katika mkoa wa Singida ili kufanikisha utekelezaji wa lengo namba 3 ambalo ni 'Afya Njema na Ustawi' kati ya malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) yanayotarajiwa kuanza kutekelezwa 2016-2030. Wanaoshuhudia tukio hilo kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone (wa kwanza kulia), Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Festo Kang'ombe (wa pili kulia) pamoja na Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Singida, Mdala Fedes (wa tatu kushoto) wakimkabidhi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez bango hilo lenye mambo muhimu yanayotakiwa kufanyika katika mkoa wa Singida ili kufanikisha lengo namba 3 kati ya malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) aliyeambatana kwenye ziara hiyo na Afisa a Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (katikati kulia).
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone (wa pili kulia), Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Festo Kang'ombe (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) kwenye bango maalum lenye rangi mbalimbali zinazowakilisha malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) yanayotakiwa kumfikia kila mwananchi nchini kwa ajili ya utekelezaji.
Kutoka kushoto ni Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Singida, Mdala Fedes, Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Festo Kang'ombe, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bw. Sute pamoja na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone (katikati) akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Ofisa kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan nje ya jengo la Ofisi ya Mkuu huyo wa mkoa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone.
......AKIWA NJIANI KUELEKEA MKOANI SINGIDA......
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwa ameambatana na Ofisa kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (kulia) mara baada ya kusimamisha gari maeneo ya Babati mjini.
Neema Mikaeli (22)akihamaki kuona watu waliokuwa wakimsogelea (hawapo pichani) katika eneo alilokuwa akifua nguo kwenye dimbwi la maji machafu ya mvua kama yanavyoonekana pichani.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini akiwa njiani kuelekea mkoani Singida alishtushwa kuona mkazi mmoja wa Babati mjini Neema Mikaeli (22) akifua nguo kwenye dimbwi la maji machafu ya mvua na kusimama na kuzungumza nae ambapo aligundua kuna tatizo la maji safi na salama kwa wakazi wa eneo hilo pamoja na ukataji miti ambao unapelekea kuharibu mazingira.
Katika mazungumzo ya Neema alisema kuwa kuna mabomba ya maji yaliyowekwa zaidi ya miaka 3 sasa lakini hayatoi maji na hivyo kupelekea wao kutembelea umbali mrefu ambao kuna mto na wanatumia maji ya mto huo kupikia na kunywa.
Akiongea na Mikaela alimuhakikishia kwamba Umoja wa Mataifa utazidi kufanya kazi ka ukaribu na serikali ya Tanzania sambamba na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Ofisa kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu wakizungumza na Mkazi huyo wa wilaya ya Babati mjini mkoani Manyara, Neema Mikaeli (22) aliyekuwa akifua nguo zake kwenye dimbwi hilo kutokana na kukosekana kwa maji katika eneo lao.
Haya ndio maji ambayo hata sabuni ya unga haikolei yaliyokutwa yakitumiwa na Neema Mikaeli (22) (hayupo pichani) kufulia nguo zake.
Neema Mikaeli (22) akiwa kwenye eneo la dimbi la maji ya mvua akiendelea kufanya usafi wa nguo zake.
MELI MPYA YA MV MAPINDUZI YAWASILI KATIKA BANDARI YA ZANZIBAR, IMETOKA KOREA
Meli Mpya ya MV Mapinduzi Ikiwasili katika Bandari ya Zanzibar Ikitokea Nchini Korea Ilikotengenezwa.
Meli Mpya ya MV Mapinduzi 2 ikiwasili Zanzibar ikitokea Nchini Korea
Meli Mpya ya MV Mapinduzi ikiwasili katika bandari ya Zanzibar ikitokea Nchini Korea baada ya kukamilika kwa Uundaji wake uliochukua miezi 18, ikiwa katika bahari ya Zanzibar ikielekea katika bandari kwa ajili ya ufungaji wa gati katika bandari ya Malindi Zanzibar.
Wananchi wa Zanzibar wakiipokea Meli yao Mpya ya MV Mapinduzo 2 wakiwa katika bustani ya Forodhani Zanzibar.
Wananchi wa Zanzibar wakichukua picha kupitia simu zao Meli Mpya ya MV Mapinduzi wakati ikiwasili Zanzibar katika bandari ya Zanzibar
Meli Mpya ya Mv Mapinduzi 2 ikiwa katika bahari ya Zanzibar.
Wananchi wa Zanzibar wakiwa katika bustani ya forodhani wakiipokea Meli yao Mpya ya MV Mapinduzi 2 ikiwasili Zanzibar ikitokea Nchini Korea ilioundwa meli hiyo.
Wananchi wa Zanzibar wakichukua picha kupitia simu zao Meli Mpya ya MV Mapinduzi wakati ikiwasili Zanzibar katika bandari ya Zanzibar, wakiwa katika bustani ya forodhani Zanzibar
Wananchi wakiwa katika Bandari Kuu ya Malindi Zanzibar wakiipokea Meli yao Mpya ya MV Mapinduzi ilipokuwa ikifunga gati katika bandari hiyo ya Zanzibar.
Wafanyakazi wa Shirika la Meli Zanzibar wakipiga picha Meli Mpya ya Mv Mapinduzi kupitia simu zao kwa ajili ya kumbukumbu kwa kuja kwa Meli hiyo Mpya.
MV Mapinduzi ikiwa katika Bandari ya Zanzibar ambayo ina uwezo wa kuchukua Abiria na Mizigo na Magari.
Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee akiwapungia mikono Wananchi waliofika katika Bandari ya Malindi Zanzibar ikifunga Gati akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dk Juma Malik.
Mwananchi wa Zanzibar akiwa na simu yake baada ya kuchukua picha ya Meli ya Mv Mapinduzi 2 na kuwatumia Wananchi kupitia simu yake.
Wafanyakazi wa Shirika la Meli Zanzibar na wa Shirika la Bandari Zanzibar wakishangilia Meli Mpya ya MV Mapinduzi wakati ikiwasili katika bandari ya Malindi ikifunga Gati
Wafanyakazi wa Shirika la Meli Zanzibar na wa Shirika la Bandari Zanzibar wakishangilia Meli Mpya ya MV Mapinduzi wakati ikiwasili katika bandari ya Malindi ikifunga Gati
Wananchi wakiwa katika Bandari ya Zanzibar wakiipokea Meli ya Mv Mapinduzi 2 katika bandari ya Zanzibar.
Meli Mpya ya MV Mapinduzi 2 ikiwa katika bandari ya Malindi baada ya kufunga gati katika bandari hiyo ya Zanzibar.
Wafanyakazi wa Shirika la Mandari wakiwa katika Bandari ya Zanzibar wakipokea Meli Mpya ya Mv Mapinduzi 2
Waandishi wa habari wa Zanzibar na Viongozi wa Shirikala la Meli Zanzibar wakiwa katika Meli ya Mv Mapinduzi 2 wakitokea katika kisiwa cha Chumbe kuipokea meli hiyo ikitokea Nchini Korea ilikoundwa Meli hiyo. Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com.
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...