CHAMA Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Tawi la Mkoa wa Iringa kimemuomba Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuhakiksha kuwa makundi yote maalumu yanapata haki sawa na mengine ili kuondoa dhana ya ubaguzi.
Akiongea na SIMBAYABLOG Katibu wa CHAVITA Mkoa wa Iringa Shaibu Juma ambapo alisema kuwa wanamshukuru Rais John Magufuli kwa kutoa kibali cha kufanya sherehe za siku ya Walemavu kitaifa Mkoani Mwanza.
Alisema kuwa kuna makundi mengine, yamekuwa yakiwezeshwa mara kwa mara aidha kupitia kwa mashirika yasiyo ya Kiserikali na hivyo kuweza kupata maendeleo kwa haraka na kumudu maisha yao ya kila siku.
Juma alisema kuwa katika Kampeni zake za kutafuta Urais Dkt. Magufuli alisema katika utawala wake hatabagua makundi maalum hasa wenye ulemavu katika uongozi wake hali ambayo imeonyesha dhahiri kuwa amedhamiria kuwasaidia.
“Tunampongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kuongoza Taifa la Tanzania na sisi kama makundi ya watu wenye Ulemavu tumeahidi kumpa ushirikiano wa hali ya juu kutokana na utendaji wake wa kazi hali ambayo itasaidia katika kuleta mabadiliko kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na kutekeleza kauli mbio ya “hapa kazi tuu,” alisema katibu hiyo wa CHAVITA.
Aidhi, katibu huyo alielezea masikitiko yake kwa Chama cha Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Mkoa wa Iringa kwa kushindwa kuviunganisha vyama vya watu kwenye walemavu mbalimbali mkoani hapa na kumemuomba Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuhakiksha kuwa makundi yote maalumu yanapata haki sawa na mengine ili kuondoa dhana ya ubaguzi.
Alisema tangu kuanzisha kwa tawi hilo la Chavita mkoa wa iringa mwaka 1994 hakijawahi kupata msaada wote kutoka kwa idara ya ustawi wa jamii mkoa, manispaa ya iringa pamoja na SHIVIWATA.
Kwa upande wake mjumbe wa CHAVITA Mkoa wa Iringa Alfred Emmanuel Chengula alisema kuwa ni vema kwa Serikali akangalia makundi kama hayo kwa sasa ili na wao pia wawe na uwezo wa kumudu changamoto nyingi zinazowakumba watu wa makundi ya Wenye ulemavu.
“Ni vema sasa kwa Serikali ya awamu ya tano Chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk,John Magufuli kuliangalia kwa jicho la kipekee kundi hilo na kuangalia changamoto mbalimbali zinazolikumba ili kuweza kuwawezesha kiuchumi na kuweza kumudu maisha yao ya kila siku,” alisema Mjumbe huyo.
Mjumbe mwingine aliyeambatana na katibu huyo wa Chavita ni pamoja na Zawadi Boniface aliyehoji kuwa ile asilimia kumi inayotenga na serikali kila mwaka kwa ajili ya watu wenye ulemavu inaenda wapi.
Tarehe 3, Desemba ya kila mwaka ni siku ya Watu wenye Ulemavu duniani. Siku hii inatokana na uamuzi wa Umoja wa Mataifa kui tangaza siku hii kuwa ni siku ya Watu wenye Ulemavu duniani kufuatia Azimio Na. 47/3 la mwaka 1992.
Tanzania kama nchi mwanachama imeridhia na kusaini mkataba huu, na imekuwa ikiadhimisha siku hii kitaifa katika mikoa toufati na mwaka jana maadhisho huyo walifanyika mkoani Iringa.
maadhimisho haya ni kwa lengo la serikali na wadau mbalimbali utambua uwezo wa Watu wenye U lemavu na kujenga mazingira yanayotoa fursa na ushiriki wao katika shughuli mbalimbali za maendeleo hapa nchini.
Kutangazwa kwa siku hii kumelenga kuinua u fahamu wa jamii kuhusu masuala ya Haki za Witu Wenye Ulemavu pamoja na kutoa fursa kwa Serikali za kila nchi duniani kutafakari juu ya utoaji wa huduma endelevu kwa nia ya kuinua hali za maisha ya Watu Wenye Ulemavu.
No comments:
Post a Comment