Thursday, 5 July 2018

Amchinja mtoto wa miaka sita kisa muwa



Jeshi la polisi mkoani iringa linamshikilia mfanyakazi wa bustani (shamba boy) mkazi wa wilaya ya kilolo kwa tuhuma ya mauaji ya mtoto miaka sita. 

Kamanda wa polisi mkoani Juma bwire makanya aliiambia nipashe jana kuwa mfanyakazi huyo Jofrey Jasephat miaka 29 mkazi wa wilaya ya kilolo mkoani iringa anashikiliwa na polisi kwa tuhuma ya mauaji ya mtoto. 

Bwire alisema kuwa tukio hilo lilitokea tarehe 04/07/2018 majira ya saa 5 asubuhi huko maeneo ya Kibwabwa “B” kata ya Kitwiru manispaa ya iringa, mkoani Iringa. 

Alisema kuwa mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa mkazi wa Kibwabwa B aliuawa kwa kukatwakatwa na mapanga sehemu za shingo na mikononi na kisha mwili wake kuhifadhiwa kwenye mfuko wa salefti na kuuficha kwenye pagale. 

Kamanda huyo alifafanua kuwa chanzo cha mauaji hayo ni kutokana na kauli za maudhi kutoka kwa mtoto kwendakwa mtuhumiwa akidai yeye ni mpumbavu hafai baada ya mtoto kunyimwa mua alioomba. 

ACP Bwire alisema kuwa mtuhumiwa alipandwa na hasira kisha kuchukua uamuzi huo. Hata hivyo, upelelezi unaendelea na ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili sheria ichukuwe mkondo wake.

Polisi Iringa laanza operesheni ya kukagua liseni za madereva...





Na Friday Simbaya, Iringa

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa katika kukabiliana na ajali za barabara limeanza kufanya operesheni ya kukagua leseni za madereva wote wa magari yakiwemo mabasi ya abira. 

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire alisema kuwa kutokana na kuwepo na leseni za kugushi pamoja na kukosekana kwa mafunzo kazini kwa madereva. Alisema kuwa mafunzo hayo ni ya kukumbushana

Kamanda Bwire alisema kuwa operesheni hiyo itaanza Julai 4 hadi Julai 7 mwaka huu, ambapo tarehe 9 Julai hadi Jumamosi ya Julai 14 wanatarajia madereva kwa lengo la kuwapatia mafunzo kazini.

Hatua hiyo imekuja kufuatia mabadiliko ya mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) Simon Sirro kufanya mabadiliko ya makanada wa polisi katika baadhi ya mikoa.

Mabadiliko hayo kwa mujibu wa IGP ni kwa lengo la kuoongeza juhudi za kuzuia ajali zinazotokana mara kwa mara katika baadhi ya mikoa.

Kwa upande wake, Salum Chang’a ambaye ni dereva wa mabasi Nani kaona aliponza jeshi la polisi kwa operesheni hiyo na kuwaoba madereva wenzake kutoa ushirikiano katika kukabiliana na ajali za bararani mkoani hapa.

Chang’a ambaye alikuwa ndio dereva wa kwanza kukaguliwa alisema kuwa ili operesheni hiyo iwezo kufanyiwa polisi wanatakiwa kuanza na madereva wa malori na wale gari za IT kupima ulevi.

Alisema kuwa madereva wengi wa magari makubwa wanatabia ya kunywa pombe kila kituo hasa maeneo ya Ruaha Mbuyuni na Mikumi.




Aliongeza kuwa pombe ni kitovu cha uzembe wa ajali za barabarani. Katika hatua nyingine, Polisi mkoani Iringa wameokota mwili wa Yakobi Mhengilolo,23 mkazi wa Usokami na funding sekemara aliyekutwa amefariki dunia katika barabara ya kuelekea kijiji cha Kibengu.


Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa ACP Bwire alisema kuwa tukio hill lilitokea tarehe 02/07/2018 majira ya SAA 19:30hrs katika cha usokami tarafa ya Kibengu wilayani Iringa mkoani Iringa.

Alisema kuwa uchunguzi wa daktari unaonesha kuwa marehemu amevunjika shingo, mbavu mbili pamoja na kuwa na michubuko/ majeraha mwilini.

Iringa Police launches the operation on the drivers’ licenses to reduce road accidents





Iringa Police in their effort to reduce road traffic accidents has begun to conduct the operation of inspecting all drivers’ licenses including the passenger buses.

Speaking to journalists yesterday Iringa Regional Police Commander, Assistant Commissioner of Police (ACP)Juma Bwire said that due to the existence of licensing fake licenses and the lack of training at work for drivers was one of the factor contributing road traffic accidents.

He said that training was to remind drivers on the importance of safe driving that will include refresher course to drivers.

Commander Bwire said the operation will begin on July 4 to July 7 this year, but from 9 July to Saturday of July 14 expecting drivers to be given job on training.

The action has come after the change of police chief in the country (IGP) Simon Sirro to make changes to police commander in some regions.

The change in accordance with the IGP is aimed at increasing efforts to prevent frequent accidents in some regions.

On the other hand, Salum Chang'a who is a bus driver hailed the police force operation and forced his fellow drivers to cooperate in dealing with the crash in the area here.

Chang'a, who was the first driver to be inspected and investigated, said that for the operation of the police, they should start with truck drivers and IT drivers to fight alcoholism.

He said that many motorcyclists used to drink alcoholic beverages at every station especially in the areas of Ruaha Mbuyuni and the Mikumi in Morogoro.

He added that alcohol is a center of traffic accidents and if they can conduct alcohol testing to truck drivers and small vehicles it will help reduce accidents.

At another point, the Iringa police has picked up the body Yakobo Mhengilolo, 23 years resident of Kibengu Village in Iringa District was found dead on a road leading to the Kibengu village.


RPC said took place on 02/07/2018 at around 19:30 hrs at Usokami Village, Kibengu sub district at around, Iringa District in Iringa Region.

He said that a doctor's examination revealed that the late had broken the neck, the two ribs along with the bruises / injuries in the body. By Friday Simbaya, Iringa

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...