Thursday, 22 December 2016

MBUNGE VITI MAALUM RITTA KABATI KUKARABATI SHULE YA MSINGI AZIMIO


Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya iringa Abeid Kiponza,mbunge wa viti maalumu mkoani iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakiwa katika moja ya madarasa ya shule ya msingi Azimio wakati wa kujadili jinsi gani ya kutatua changamoto za shule hiyo



Mbunge wa viti maalumu mkoani iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akikagua miundombinu ya shule ya msingi Azimio sambamba na wananchi na viongozi wa shule hiyo.



Hili ni moja kati ya madarasa ya shule ya msingi Azimio ambalo lipo taabani kabisa na likiwa linakaribia kuanguka kutokana na kuwa na nyufa nyingi ambazo ni kubwa sana 




Hili ni moja kati ya madarasa ya shule ya msingi Azimio ambao linaonekana afadhari kidogo na kuwashawishi viongozi mbalimbali kuketi na kujadili maswala ya kutatua changamoto za shule hiyo ambapo madarasa mengine yapo taabani kuliko hili.





Na fredy mgunda,Iringa


Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa Ritta Kabati anatarajia kukarabati shule ya msingi ya Azimio iliyopo manispaa ya Iringa kutokana na uchakavu wa majengo hayo.


Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya shule hiyo mbunge Kabati alisema ni aibu kwa shule kongwe kama hiyo kuwa miundombinu mibovu kama hiii.


Kabati aliongeza kuwa shule hiyo imeharika hovyo na inahitaji msaada wa haraka kuikarabati kwa kuwa wananfunzi wanasoma katika mazingira magumu na kudumisha elimu ya wanafunzi hao.


“Hii shule imeanza sawa na siku niliyozaliwa mimi lakini ukiiangalia imechakaa na imechoka hivyo sina budi kuanza kuikarabati shule hii kwa kuwa ni aibu kwangu haiwezakani shule ikawa manispaa ya iringa halafu ikawa katika muundo huuu”alisema kabati


Aidha Kabati alisema kuwa hadi kufikia siku ya ijumaa ya tarehe 23 mwezi wa kumi na mbili atahakikisha anakarabati shule yote ili iwe katika ubora unaotakiwa kama shule nyingine zilizopo manispaa ya iringa.


“Tunashule bora sana hapa manispaa ya iringa lakini hii ya Azimio imekuwa katika hali mbaya sana ni jukumu langu kama mbunge wa mkoa wa iringa kutatua changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa wangu”alisema Kabati


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema haiwezekani shule ya azimio ikawa katika mazingira mabovu ya miundombinu kama yale hiyo hadi kufikia siku ya ijumaa atahakikisha anakarabati shule hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.


Naye mkuu wa shule ya msingi Willfrid Chotipembe alimshukuru mbunge wa viti maalum Ritta Kabati pamoja na mkuu wa wilaya kwa kufika shuleni hapo na kuahidi kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo.


MEYA DAR ES SALAAM AWAONYA WAKUSANYA USHURU WA MAEGESHO


Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akifafanua jambo kwa wandishi wa habari leo kuhusiana na suala zima la tozo za maegesho ya magari



MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amewataka wakandarasi hususani wanaokusanya ushuru wa maegesho, waanze kutumia mashine za EFDs walizokabidhiwa vinginevyo mikataba yao iko hatarini kusitishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Meya Mwita amesema kwa muda mrefu wakandarasi hao walikuwa wakitumia mashine za mkono, wamebaini mapato mengi yalikuwa yakipotelea mifukoni mwa watu wachache na sasa ni agizo kwa wazabuni wote wa wilaya za Daresalaam kutumia mashine za Kielectroni.

Amesema kupitia mashine hizo wanahakika mapato yataongezeka kutoka shilingi milioni 170 iliyokuwa inakusanywa hapo awali kwa mwezi hadi kufikia Zaidi ya Shilingi Milioni 370 kwa mwezi.

Katika hatua Nyingine, Isaya Mwita amewaonya wakandarasi hao kuangalia namna ya kuwadhibiti wafanyakazi wao kwani hivi sasa wamezusha tabia ya kuwanyanyasa wakazi wa Jiji la Darsalaam kinyume cha makubaliano ya mkaba.

Amesema kumekuwa na tabia za wakandarasi isivyo halali wakazi wa jiji wanaoegesha magari yao,pamoja na kutumia lugha za matusi kwa kisingizio cha kufuata sheria za Jiji.


Amesema sheria ya Jiji hairuhusu matumizi ya mabavu, matusi, kejeli kwa watu wanaoegesha gari zao, wanachopaswa kufanya ni kufuata sharia ambazo wamekubaliana katika mikataba yao ya kazi.


Meya ameyataja majukumu ya kimkataba ambayo wakandarasi wote wanapaswa kufuata ni kama ifuatavyo,:
1 .Wakala atafanya kazi hii bila Kuvizia magari ya wananchi kwa lengo la kujipatia pesa .


2. Wakala atafanya kazi hii kwa weledi mkubwa kwa kuzingatia Sheria, Miongozi, Maelekezo, Kanuni na taratibu zilizopangiwa pasipo kusababisha bughuza ,kero na usumbufu kwa Wananchi.


3. Wakala anatakiwa kutoa muda wa dakika sitini [60] kabla ya kuchukua mamuzi ya vuta gari, Bodaboda au bajaji lililovunja sheria, kuzuia . Lakini kwa gari , Bajaji au Bodaboda iliyozuia barabara itaondolewa mara moja ili kuondoa msongamano.


4.Wakala anapaswa kuepuka kutoa Lugha ya Matusi au udhalilishaji .


4.Wakala anapaswa kuruhusu gari ,Pikipiki au Bajaji kuegeshwa kwa dharura sehemu isiyoruhusiwa kwa muda usiozidi dakika Thelasini [30] kama Dereva ameweka viashiria vya tahadhari. Isipokuwa kwa wale wenye magari yenye hitilafu inaweza kuzidi mpaka saa moja [yaani dakika 60] baada ya kujirizisha na dharura iliyojitokeza.


5. Wafanyakazi wanapaswa kuwa na sare pamoja na vitambulisho vya kazi .


6. Wakala anatakiwa kutoa faini zilizoainishwa na jiji na sio vinginevyo.


7. Wakala anapaswa kutumia risiti za mashine za Kielekronikia.


8.Magari yanayotumika katika utekelezaji wa kazi hii yanatakiwa yawe na Stika kubwa inayoonyesha jina la kampuni pamoja na namba ya simu ya wakala.


9.Wakala anatakiwa kutumia risiti [Point of Sale, [POS] za Halmashauri ya jiji.




10. Wakala anatatakiwa kutoa taarifa ya utekelezaji wa kazi hii kwa MWAJIRI Kila baada ya Wiki Mbili.
11.Wakala anatakiwa kufanya kazi katika maeneo aliyoelekezwa na MWAJIRI nasio vinginevyo.


12. Wakala anapaswa kushirikiana na jeshi la polisi pamoja na Mamlaka zingine pale inapohitajika katika utekelezaji wa kazi husika.


Sasa anashangazwa kuona mikataba hiyo inavunjwa, amesema hatosita kufuta zabuni zote kwa kitendo cha kukiuka makubaliano hayo.

MAZISHI YA KIHISTORI IRINGA MAREHEMU AZIKWA KABURI MOJA NA KONDOO


Wanafamilia wakiwa wamelizungika kaburi la marehemu Ngaga aliyezikwa kaburi moja na kondoo pamoja na kuku mweusi leo kwenye kitongoji cha Mkawaganga kijiji cha Mbigili wilaya ya Kilolo mkoani Iringa 

Mganga wa kienyeji Galasiano Nyenza (kulia) akiwa na mtoto wa marehemu Andrea Ngaga ,Kurugenzi Ngaga kushoto baada ya kufanyika kwa mazishi ya kimila katika kijiji cha Mbigili Kilolo kwa marehemu kuzikwa kaburi moja na kondoo na kuku mweusi 

Mganga Nyenza aliyeongoza mazishi hayo katikati akiwa na baadhi ya ndugu kando ya kaburi 

Waombolezaji wakitoka kuzika 

 
 Marehemu enzi za uhai wake 

Nyumbani kwa marehemu waombolezaji wakiwa kwenye foleni 
....................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog
MAMIA ya wakazi wa kijiji cha Mbigili na mji wa Ilula katika wilaya ya Kilolo wamefurika katika mazishi ya aina yake yaliyofanyika katika kitongoji cha Mkawaganga kijiji cha Mbigili wilaya ya kilolo mkoani Iringa kushuhudia mazishi hayo ya kihistoria baada ya mzee mmoja aliyefariki dunia ghafla kuzikwa kaburi moja na kondoo pamoja na kuku mweusi.


Tukio hilo limetokea leo wakati wa mazishi ya mzee Andrea Ngaga (90) mkazi wa kitongoji cha Mkawaganga aliyekuwa akijishughulisha na kazi za uganga wa kienyeji kijijini hapo enzi za uhai wake .


Baadhi ya wananchi waliofika katika mazishi hayo walisema kuwa walilazimika kusitisha shughuli zao za shamba na biashara na kufika kushuhudia mazishi hayo ambayo ni mara ya kwanza kufanyika katika kijiji hicho alisema John Mfaligoha kuwa kabla ya kifo marehemu huyo alipata kuwaeleza aina ya mazishi yake yatakavyokuwa .


Hivyo alisema wananchi waliowengi walifika kutaka kushuhudia tukio hilo la mazishi na ndio sababu iliyopelekea wananchi kusukumana msibani wakati wa mazishi kwa kila mmoja kutaka kushuhudia tukio hilo la kihistoria katika kijiji hicho.


Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mbigili Ibrahim Rashid (46) alisema amezaliwa katika kijiji hicho tukio hilo ni la kwanza kufanyika hajapata kushuhudia mazishi ya aina hiyo zaidi ya kusikia katika vyombo vya habari kutoka nje ya kijiji chake na kuwa mazishi hayo yamefanyika kimila zaidi na kimsingi huwa marehemu anachagua mtu wa kuzikwa nae kabla ya kifo .


Ila hakuweza kuacha maagizo zaidi ya kuomba pindi atakapokufa kuzikwa kimila na ndio sababu aliyeongoza mazishi hayo ni mganga wa kienyeji kutoka Ifunda wilaya ya Iringa Galasiano Mfaume Nyeza ambae ni baba mdogo na marehemu huyo .




Mtendaji wa serikali ya kijij hicho cha Mbigili Thabith Kalolo alisema kuwa kimsingi hakuna kosa lolote familia ambalo wamelifanya kwa kufanya mazishi ya aina hiyo kwani serikali haiingilii uhuru wa wananchi wake kuamini masuala ya mila na kuwa iwapo mazishi hayo yangekiuka haki za binadamu mwingine mfano kama wangekata kumzika marehemu na binadamu mwingine aliyehai hapa isingewezekana ila kwa kumzika na kondoo na kuku mweusi hakuna shida .


Hata hivyo alisema tofauti ya rekodi ya misiba iliyopata kutokea katika kijiji hicho ,msiba wa mganga huyo umevunja rekodi kwa kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watu na kuwa msiba uliovunja rekodi kwa michango ni huo pekee kwani misiba mingine fedha za rambi rambi huwa ni kati ya Tsh 300000 hadi 500000 mwisho ila msiba huo rambi rambi ni zaidi ya Tsh milioni 1.3


Mtoto wa marehemu Kurugenzi Ngaga alisema kuwa babake alifariki dunia juzi Desemba 20 majira ya saa 6 usiku mwakla huu kuwa alikuwa akisumbuliwa na tatizo ya chembe ya Moyo na kuwa ameacha wajane wawili na watoto 19.


Kurugenzi alisema kimila kama ingekuwa zamani marehemu angezikwa na mjukuu wake aliyemteua kushika mikoba yake ila kutokana na mambo ya mila kwa sasa kupewa kisogo waliona ni vema wakamzika na kondoo na kuku huyu mweusi .

KIKAO CHA BARAZA LA BIASHARA LA MKOA WA IRINGA KINAENDELELEA...

Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Iringa Lucas Mwakabungu akisoma taarifa kutoka sekta binafsi wakati wa kikao cha baraza la biashara cha mkoa wa Iringa kinachofanyika mjini Iringa leo. (Picha na Friday Simbaya)





Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha baraza la biashara cha mkoa wa Iringa wakifuatilia kikao hico kwa makini kinachofanyika mjini Iringa leo. (Picha na Friday Simbaya)



Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Biashara Mkoa wa Iringa akifungua kikao cha baraza hilo kinachofanyika mjini Iringa leo. Walioketi kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Iringa Lucas Mwakabungu na Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa (RAS) Wamoja Ayubu (Picha na Friday Simbaya)



Mweka Hazina kutoka TCCIA Iringa ambaye pia ni mmoja ya wajumbe wa sekretatrieti akisoma taarifa wakati wa Kikao cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Iringa (RBC).

Sekretarieti, kushoto niJames sizya mtendaji TCCIA (M) Iringa na Rose mjumbe.



Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kikao cha Baraza la Biashara cha Mkoa wa Iringa kinachofanyika mjini Iringa leo katika Ukumbi wa VETA. (Picha na Friday Simbaya)






WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...