Monday, 13 November 2017

RC AIPONGEZA RUAHA KWA KUPAMBANA NA UTAPIAMLO

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kushoto) akitembelea banda la Ruaha Miling Company Limited katika uzinduzi wa Kampeni ya Mama Msosi Lishe mkoani Iringa jana. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)


Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza akimpatia uji wa lishe mtoto katika uzinduzi wa Kampeni ya Mama Msosi Lishe mkoani Iringa jana. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)



IRINGA: MKUU wa Mkoa wa Iringa (RC) Amina Masenza ameipongeza kampuni ya kusaga unga wa lishe ya ‘Ruaha Milling Company Limited’ ya mjini Iringa kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na tatizo la utapiamlo.

RC alisema huyo katika uzinduzi wa Kampeni ya Mama Msosi Lishe mkoani Iringa jana, ambayo ili lenga kuhamasisha lishe bora ili kupambana na udumavu pamoja na kuhamasisha usafi na uhifadhi wa mazingira.

Alisema kuwa kampuni ya Ruaha Milling imekuwa mstari wa mbele katika kupambana na utapiamlo mkaoni hapa kwa kutengeneza unga uliotiwa virutubisho.

Masenza alisema kuwa Kampeni ya Mama Msosi Lishe ni mojawapo ya njia ya kuboresha Lishe kwa familia na kuondoa matatizo yanayosababishwa na Lishe duni. 

“Wataalam wa masuala ya Lishe wanatuambia kuwa watoto waliopata huduma bora za Lishe, katika kipindi cha siku 1,000 za kwanza za uhai wao ambazo zinaanza tangu mama anapopata ujauzito hadi mtoto anapotimiza umri wa miaka miwili wanapata faida zitakazodumu katika maisha yao yote,” alisema.


Hiki ndicho kipindi mtoto anapojenga msingi wa ukuaji wa mwili na maendeleo ya akili. 

Kwa bahati mbaya madhara ayapatayo mtoto katika ukuaji wake kimwili na maendeleo ya kiakili kutokana na Lishe duni katika siku 1,000 za kwanza za maisha yake hayawezi kurekebishwa kwa maisha yake yote.

Kwa mujibu wa utafiti (TDHS, 2015/2016) umebaini kuwa hali ya Lishe ya wanawake na watoto bado ni mbaya Mkoani Iringa. 

Asilimia 28 ya wanawake wajawazito wana upungufu wa damu. Asilimia 42 ya watoto wamedumaa, asilimia 13.8 wana uzito pungufu, asilimia 3.6 wana ukondefu na asilimia 7.2 tu ndiyo wanalishwa vyakula vya nyongeza ipasavyo.

Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali umekuwa ukichukua hatua za kukabiliana na tatizo la utapiamlo. 

Hatua hizo ni pamoja na kutoa elimu ya Lishe katika vituo vya kutolea huduma, kutoa matibabu ya utapiamlo, kuhamasisha jamii kubadilli tabia za ulaji usiofaa na kufuata mtindo bora wa maisha, kuhamasisha usafi wa mazingira, kuwahi kliniki pindi mama anapogundua kuwa mjamzito. Na Friday Simbaya, Iringa

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...