Kocha Mkuu wa timu ya Panama Queens FC, Miraji Fundi akizungumza na waandishi wa habari baada ya mechi yao dhidi ya Mlandizi Queens FC ya Pwani ambapo timu hiyo ilifungwa bao 5-2 katika Uwanja wa nyumbani wa Samora mjini Iringa Jumapili. (Picha na Friday Simbaya) |
Meneja wa timu ya Mlandizi Queens FC Yassin Ramadhani |
Na Friday Simbaya, Iringa
Timu ya mpira ya wanawake mkoani Iringa Panama FC inakabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo la kukosa vifaa mbalimbali michezo kama vile mipra, imeelezwa.
Akizungumza na Nipashe jana Kocha Mkuu wa timu ya Panama Queens FC, Miraji Fundi baada ya mechi yao dhidi ya Mlandizi Queens FC ya Pwani alisema kuwa timu yake inakabiliwa changamoto mbalmabli ilikiwemo la kukosekana kwa vifaa mbalimabi vya michezo pamoja na kutoungwa mkono na wadau mpira wa wanawake mkoani hapa.
Alisema kuwa kufanya vibaya kwa timu hiyo ligi ya soka ya wanawake Tanzania bara kunatokana na kutoungwa mkono na wadau pamoja na mwitikio mdogo kutoka kwa wanairinga na kuongeza kuwa wasipokaa vizuri wanaweza kukosa timu ya wanawake.
Jana Jumpili (22/04/2018)timu ya Panama Queens iliikaribisha timu ya Mlandizi Queens ya mkoani Pwani katika uwanja wa nyumbani ambao pia ni mabingwa watetezi katika uwanja kumbukumbu wa Samora mjini Iringa na kuambulia kichapo cha magoli 5-2.
Katika timu ya mabingwa watetezi ya Mlandizi magoli yalifungwa na Lucy Mrema aliyefunga magoli matatu, Annatazia Nyandago na Sabina Mbuga waliyefunga goli moja moja na kwa upande wa Panama FC magoli yote yalipachikwa kupitia kwa mshambuliaji Mgeni Kisoda.
Fundi alisema kuwa timu yake inakabiliwa na ukata wa vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo mipra na fedha za kuweza kuiandaa timu hiyo inayoshirika ligi ya soka ya wanawake Tanzania (TWFA) hatua ya nane bora inayoendelea nchini.
Kocha mkuu huyo aliongeza kuwa Timu ya Panama FC katika mechi yao ijao itamenyena na Simba Queens ya jijini Dar es Salaam ambayoitachezwa ugenini.
Naye Meneja wa timu ya Mlandizi Queens FC Yassin Ramadhani alisema kuwa amefurahishwa na matokeo ya timu dhidhi ya Panama Queens FC kwa kuzoa alama tatu na kufanya timu kufikisha pointi tisa.
Alisema kuwa timu ya Mlandizi Queens imekuwa ya kwanza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara baada ya kuifunga Panama FC ya Iringa kwa mabao 5-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mwaka jana.
Ligi ya soka ya wanawake hatua ya nane bora inaendelea nchini katika mtindo wa nyumbani na ugenini.
Mwenyekiti wa chama cha soka cha wanawake Tanzania (TWFA) Amina Karuma, alisema ligi hiyoilisimama kupisha timu ya taifa ya wanawake (Twiga Stars) iliyokuwa ikiandaa na mechi zake mbili za kuwania tiketi ya kucheza fainali za kombe la mataifa ya afrika dhidi ya Zambia lakini ilitolewa.
Ligi hiyo inayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti.
Karuma alisema kuwa ligi hiyo itasimama tena Mei 3 mwaka huu ili kupisha maadalizi ya Twiga Stars inayotarajia kushiriki mashindano ya kombe ya chalenji nchini Rwanda tarehe 11/05/2018.
Mwisho