Friday, 6 March 2015

JESCA: SIJASIMAMISHWA UANACHAMA MIMI BADO WANACHAMA...!



Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu amekanusha uvumi unaoenea mkoani hapa kuwa amesimamishwa uanachama pamoja kuvuliwa nafasi zote za uongozi leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofisi za Iringa Press Club (IPC).



UTANGULIZI

Mtakumbuka kuwa tarehe 2/3/2015 kuna kauli ambayo ilitolewa na Katibu wa wilaya ya Mufindi Ndugu Mtaturu. Ambayo ilielekeza baadhi wanachama wetu, ikiwa ni pamoja na kufukuzwa uanachama kwa baadhi ya makada wetu. Akiwemo Shukuru Luhambati, Clara Shirima na Hosea Kaberege. Swala hili limeamusha malalamiko na mjadala miongoni mwa wanaCCM na wapenzi na wakereketwa wa CCM. Kila mtu akiwa na mtizamo wake kuhusu swala hili, ambalo pia kimepelekea kuamsha malumbano katika vyombo mbali mbali vya habari.

MSANII WA NYIMBO ZA INJILI, MKOANI IRINGA REHEMA CHAWE AACHIA ALBAMU YAKE

 
 Muimbaji wa Nyimbo za Injili Rehema Chawe

Muimbaji wa Nyimbo za Injili Rehema Chawe


MSANII wa nyimbo za Injili, nyanda za juu kusini Rehema Chawe ambaye ni Mwanachama wa chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA), anatarajia kuzindua albamu yake ya kwanza, inayoitwa Kusamehe ni afya.

Uzinduzi huo unatarajia kufanyika Jumapili, March 8, mwaka katika kanisa la EAGT, Frelimo kwa mchungaji Mwenda, ambaye ni Mwenyekiti wa makanisa ya Kipentekoste mkoani Iringa.

Akizungumza na wanahabari, Chawe alisema uzinduzi huo utapambwa na waimbaji wengi toka nje na ndani ya mkoa wa Iringa.

Alisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa, ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Iringa, Enock Ugulumo.

Mwenyekiti wa CHAMUITA mikoa ya nyanda za juu kusini, Tumaini Msowoya Kibiki aliwataka wanachama wote kuwepo kwenye uzinduzi huo ili kumsindikiza mwenzao.

“Ni jukumu la waimbaji wote hususani wanachamuita kuhakikisha wanakuwepo siku ya uzinduzi ili kumuunga mkono mwanachama wenzetu,”alisema Kibiki.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...