Sunday, 18 November 2012

TATIZO LA MAJI

Wafanyakazi wa Kampuni ya kuchimba visima  Yatula wakisaidiana kutoa udongo kutoka chini ya kisima chenye urefu wa mita 19 kwa kutumia kamba ya waya jana. Kampuni hiyo ya kuchimba visima imechimba jumla ya visima vinne katika Chuo cha Ufundi Stadi cha Peramiho (PVTC) wilayani Songea , Mkoa wa Ruvuma ili kukabiliana na tatizo  la maji chuoni hapo.  Aidha visima hivyo ni kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya maji, kilimo cha bustani na mifugo chuoni hapo. Picha ndogo ni sehemu ya bustani iliyonyauka kutokana na uhaba wa maji katika taasisi hiyo. (Picha na Friday Simbaya)

Mkazi wa Kitongoji cha Kichangani katika Kijiji cha Peramiho ‘B’  wilayani Songea (V), Mkoa wa Ruvuma Mzee Benedict Mahinya (60) akishona viatu vya wateja jana. Mzee Mahinya alianza  shughuli ya kushona  viatu baada ya kufanya kazi ya udereva  kwa miaka 30 katika  Kiwanda cha Mbao cha Twiko mkoani Tanga, kama sehemu ya kujikimu kimaisha. (Picha na Friday Simbaya)

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...