Wafanyakazi wa Kampuni ya kuchimba visima Yatula wakisaidiana kutoa udongo kutoka chini ya kisima chenye urefu wa mita 19 kwa kutumia kamba ya waya jana. Kampuni hiyo ya kuchimba visima imechimba jumla ya visima vinne katika Chuo cha Ufundi Stadi cha Peramiho (PVTC) wilayani Songea , Mkoa wa Ruvuma ili kukabiliana na tatizo la maji chuoni hapo. Aidha visima hivyo ni kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya maji, kilimo cha bustani na mifugo chuoni hapo. Picha ndogo ni sehemu ya bustani iliyonyauka kutokana na uhaba wa maji katika taasisi hiyo. (Picha na Friday Simbaya)
Mkazi wa Kitongoji cha Kichangani katika Kijiji cha Peramiho ‘B’ wilayani Songea (V), Mkoa wa Ruvuma Mzee Benedict Mahinya (60) akishona viatu vya wateja jana. Mzee Mahinya alianza shughuli ya kushona viatu baada ya kufanya kazi ya udereva kwa miaka 30 katika Kiwanda cha Mbao cha Twiko mkoani Tanga, kama sehemu ya kujikimu kimaisha. (Picha na Friday Simbaya)
No comments:
Post a Comment