MAGAZETI YA LEO IJUMAA KWA HISANI YA CHOCOLATE IVORI
Thursday, 16 March 2017
WANANCHI WA KIJIJI CHA IDETE WILAYANI KILOLO YALIA NA UKOSEFU WA ZAHANATI
Na Friday Simbaya, Kilolo
OFISA Tathimini na Ufuatiliaji wa Shirika la MMADEA kupitia mradi wa afya bora kwa ustawi wa jamii, Hezron Kalolo amewataka viongozi wa serikali za kijiji na wananchi kwa ujumla kujenga mazoea ya kuweka akiba ya fedha zitakazowasaidia pindi wanawake wanapo karibia kujifungua na baada ya kujifungua badala ya kusubiri serikali.
Alisema kuwa pamoja na changamoto zilizopo zinazowakabili wananchi wa vijiji mbalimbali, lakini shirika la MMADEA linatoa elimu juu ya afya ya uzazi na madhara ya mimba za utotoni katika vijiji kumi na moja (11) vya mradi.
Hezron alisema haya jana kuwa mradi huo unatekelezwa katika kata za Idete, Nyanzwa na Ibumu kupitia ufadhili wa shirika la Foundation for Civil Society (FCS), huku wakifanya kampeni ya kuibua uelewa wa watu juu ya changamoto za sekta ya afya.
Alisema kuwa Wilaya ya Kilolo ni moja ya wilaya ya Mkoa wa Iringa yenye changamoto ya mimba za utotoni na ndoa za utotoni ambapo wasichana wengi hupata mimba kabla yakifikisha miaka 18.
Aidha, Afisa Tathimini na Ufuatiliaji wa Shirika lisilo la kiserikali la MMADEA huyo alizitaja baadhi ya visababishi vya mimba za utotoni kuwa ni kiwango kidogo cha elimu ya uzazi, umaskini, tamaa, ngono zembe, shinikizo rika, ndoa za utotoni na utamaduni.
Kwa upande wao, wananchi wa Kijiji cha Idete wilayani Kilolo, mkoani Iringa wameiomba serikali kuwajengea zahanati kwa ajili ya kuweza kuboresha huduma za afya ya uzazi kijijini hapo.
Walisema kijiji hicho hakina zahanati ya serikali kunakopelekea kuongezeka kwa vifo vya wajawazito na watoto vitokanavyo na uzazi, kumbe kungekuwepo na zahanati ya serikali huduma za afya zingetolewa kwa gharama nafuu kupitia mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF).
Wakizungumza jana katika nyakati tofauti wakati wa mkutano wa hadhara, wananchi hao walilipongeza shirika lisilo la kiserikali la Mazombe Mahenge Development Association (MMADEA) la mkoani Iringa kwa kutoa elimu ya masuala ya afya ya mama na mtoto, huku wakisema kumekuwa na hali yasintofahamu katika kutetea afya zao.
Walisema kuwa wanatumia gharama kubwa za huduma za afya kutokana na zahanati iliyopo ambayo sio ya serikali kutoza gharama kubwa za matibabu na kuongeza kuwa kungekuwepo na zahanati ya serikali gharama hizo zingekuwa nafuu.
Wananchi hao walisema kuwa wamekuwa wakilazimika kutembea mwendo mrefu kutoka Kijiji cha Idete hadi Kituo cha Afya cha Kidabaga kilichopo katika kata nyingine wilayani kilolo, mkoani Iringa.
Walisema kuwa kukosekana kwa kituo cha afya katani kwao ni sababu inayopelekea wananchi hao kutembea kwa mwendo mrefu kufuata huduma ikichangia na miundombinu mibovu ya barabara, ambapo magari mengi yanashindwa kufika na kulazimika kukodi gari ya kanisa katoliki kwa gharama kubwa kutokana na kutokuwepo gari la wagonjwa katika zahanati ya inayomilikiwa na kanisa la KKKT.
Walisema kuwa kungekuwepo na mfuko wa afya wa CHF kungesaidia katika kupunguza gharama za huduma za afya huku wa kihoji kwanini wachangie gharama kubwa ya gari ya wagonjwa kutoka halmashauri wakati serikali inatoa huduma bure za afya ya uzazi.
Wananchi hao wa Kijiji cha Idete, wilayani Kilolo mkoani Iringa wapo hatarini ya kukumbwa na changamoto ya kuwapoteza wanawake wajawazito na watoto kutokana na umbali wa kituo cha afya, huku wakilazimika kuchangia gari la wagonjwa kutoka halmashauri na la kanisa katoliki.
Tumpe Mwadisa ni mkazi wa Kijiji cha Idete, akiongea na mwandishi wa habari wa Nipashe wakati akishuhudia akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa ya Rufaa ambako alikwenda kujifungua kwa kupata msaada wa gari la halmashauri lililofika kijijini hapo kwa shughuli zingine.
Alisema kuwa changamoto ya kuwapoteza wanawake wajawazito na watoto inatokana na kutokuwepo zahanati ya serikali na kituo cha afya kwa kata nzima ya Idete.
Kwa upande, wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Idete, Bimas Mkemwa pamoja na Diwani wa Kata ya Idete Bruno Kauku wamesema kuwa elimu inayotolewa na shirika la MMADEA imewafungua kwa kiasi kikubwa wananchi, kwani hawakuwa na elimu ya kutosha juu ya mfuko wa afya jamii na upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi. huku wakiiomba serikali kuwajengea zahanati ili kunusuru maisha ya mama na mtoto.
Kufuatia hali hiyo wakazi na viongozi wa Kijiji cha Idete katika kata Idete, wilayani Kilolo mkoani Iringa wameiomba serikali kusaidiana kujenga zahanati ili waweze kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu hususan wajawazito ya kufuata huduma za afya.
Hata hivyo, wananchi wamelia na viongozi wa kitaifa kutofika kijijini hapo kwa miaka mingi ili kujionea adha wanazozipata wananchi wa kijiji hicho pamoja na kijiji hicho kuwa ni makao makuu ya kata.
Mwisho
TANGA UWASA INAHITAJI BILIONI 15 KUTEKELEZA MPANGO WA KUSAFISHA MAJITAKA
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu maadhimisho ya wiki ya Maji
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorra Killo akizungumza jambo wakati wa kikao hicho leo
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu maadhimisho ya wiki ya Maji
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa kulia akiteta jambo na Meneja Rasilimali watu na Utawala wa Mamlaka hiyo,Haika Ndalama.
Waandishi wa Habari Mkoani Tanga wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa ambaye hayupo pichani.
Waandishi wa Habari Mkoani Tanga wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa ambaye hayupo pichani katikati mwenye hijabu ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania
Watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa wakiandaa baadhi ya dondooo kuhusiana na wiku ya maji
Mwandishi wa Gazeti la Daily News Mkoani Tanga Amina Kingazi akiuliza swali kwenye mkutano huo kulia ni Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Mkoani Tanga,Raisa Saidi.
Mwandishi wa Azam TV Mkoani Tanga,Mariam Shedaffa akifuatilia kwa umakini taarifa mbalimbali za mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)
Waandishi wa Habari Mkoani Tanga Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania wa pili kulia wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa kwenye semina hiyo
Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania, Amina Omari akuliza swali kwenye mkutano huo
MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka katika Jiji la Tanga (Tanga-Uwasa), linahitaji kiasi cha shilingi bilioni 15 hadi 20 kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kusafisha majitaka yaweze kutumika kwa shughulinyingine za kibinadamu ikiwemo kilimo cha umwagiliaji.
Akizungumza katika semina kwa wanahabari Jijini hapa Mkurugenzi wa Tanga-Uwasa Injinia Joshua Mgeyekwa, alisema kutokana na kuzaliza kiasi cha mita za ujazo zipatazo 2,700, wameonelea wayasafishe kwa kujenga mfumo utakaosaidia maji hayo kutumika tena.
Mgeyekwa alisema tayari wametenga eneo la Utofu kama sehemu
itayokusanya maji taka ambayo kwa sasa kiasi cha asilimia 10 cha wateja wao maji wanayoyazalisha kupelekwa baharini hivyo mfumo huo utasaidia suala zima la uchafuzi wa mazingira.
“Tupo na mpango wa kuyatumia maji taka kwa shughuli nyingine kama kilimo cha mbogamboga, unaimani kwa kufanya hivyo tutaongeza kipato cha mtu mmoja moja…Lakini ili mpango huu uweze kutimia tunahitaji kiasi cha shilingi bilioni 15 hadi 20 kutekelezwa,” alisema.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa mfumo wa kutumia majitaka kwa shughuli nyingine za kibinadamu umekuwa ukitumika katika nchi zilizoendelea kama China, Israel na kwingineko ambako teklonojia hiyo imeanza.
Katika hatua nyingine Mamlaka hiyo imeanza mpango wa kufunga mita za watumiaji maji wa malipo ya kabla zinazojulikana kwa jina la ‘Lipa Maji Kadiri Unavyotumia’ (LIMAKU) ambazo tayari wamezifunga katika baadhi ya maeneo yakiwemo vikosi vya jeshi hapa nchini.
Mkurugenzi huyo alisema hadi sasa wamefunga katika vikosi vya jeshi vilipo mkoani hapa pamoja na shule 20 za msingi zilizopo katika Jiji la Tanga na maendeleo yake yanaenda vizuri.
“Tumeagiza mita nyingine za Limaku zipatazo 300 hizi pia tutazifunga katika taasisi za serikali na watu wengine hasa wateja wetu wenye madeni makubwa,” alisema Mgeyekwa.
MBUNGE WA JIMBO LA TANGA AMUANGUKIA WAZIRI MWIJAGE
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza na waandishi wa Habari ambao hawapo pichani kuhusiana na suala hilo
Mkurugenzi Uzalishaji wa kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro, Vivek Pandey akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na shirika la viwango Tanzania (TBS) kutotoa kibali cha ubora unaohitajika na hivyo kusitisha uzalishaji
Mkurugenzi Uzalishaji wa kiwanda cha Saruji cha
Kilimanjaro ,Vivek Pandey kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na shirika la viwango Tanzania (TBS) kutokutoa kibali cha ubora unaohitajika wa kiwanda hicho na hivyo kusitisha uzalishaji kulia ni Msimamizi wa Kiwanda hicho,Paskal Dimelo
Msimamizi wa Kiwanda cha kuzalishaji Saruji Mkoani
Tanga cha Kilimanjaro, Paskal Dimelo akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na shirika la viwango Tanzania (TBS) kutokutoa kibali cha ubora unaohitajika na hivyo kusitiza uzalishaji wake kushoto ni Mkurugenzi Uzalishaji wa kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro, Vivek Pandey,
MBUNGE wa Jimbo la Tanga kupitia Chama cha Wananchi CUF Alhaj Mussa Mbaruku amemuomba Waziri wa Viwanda na biashara Charles Mwijage kuingilia kati ucheleweshawajiwa wa cheti cha ubora wa viwango unaotolewa na shirika hilo la TBS na kusababisha zaidi ya watumishi 300 kupoteza ajira baada ya kiwanda hicho kufungwa.
Ameyazungumza hayo jana baada ya siku kadhaa kutolewa taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa shirika hilo limechangia kwa kiasi kikubwa kupoteza ajira kwa zaidi ya watumishi 300 kutokana na agizo lao la kusitiza uzalishaji katika kiwanda hicho kwa madai ya kukosa ubora unaotakiwa.
Alionyesha masikitiko yake hayo juu ya hataua iliyochukuliwa na shirika hilo la Ubora wa viwango Tanzania (TBS) ya kukifungia kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro kilichopo Jijini Tanga kwa kudaiwahawajafikia ubora unatakiwa katika bidhaa hiyo bila ya kuangalia athari za mwekezaji huyo na ajira zilizopotea kiwandani hapo.
Aidha alisema ni jambo la kushangaza kwa viongozi wa mamlaka hiyo husika(TBS)ambapo kwa namna moja au nyingine wanaonekana wanaikwamisha Serikali katika mpango wake wa kukua katika uchumi wa viwanda ambavyo vinaweza kuwa mkombozi wa ajira hapa nchini.
“Serikali inapambana na uchumi wa viwanda vitakavyoweza kusaidia ajira kwa vijana wetu sasa kinachotokea katika kiwanda hiki kunaonekana kuna watu wachache wanataka kumkwamisha muwekezaji huyu,hivi wizara husika iko wapi?nini hatma ya mwekezaji huyu na kufanya hivi hatuoni kama tunawafukuza hawa wawekezaji?”Alihoji Alhaj Mbaruku.
Hatua ya kusitiza huduma ya uzalishaji wa kiwanda hicho licha ya kuathiri ajira za wafanyakazi hao lakini pia itasababisha serikali kukosa mapato yanayoweza kusaidia kukuza uchumi wa Taifa na Mkoa wa Tanga .
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Kiwanda hicho,Vivek Pandey alisema kinachowaasumbua wao ni cheti bora kutoka kwa shirika la viwango cha kutambuliwa hivyo wanaomba suala hilo liingiliwe kati na mamlaka husika ikiwemo serikali ili waweze kuendelea na uzalishaji ambao utaweza kuongeza wigo wa ajira kwa vijana.
Alisema baada ya taarifa zao kutoka kwenye vyombo vya habari alifika mmoja kati ya wataalamu kutoka katika shirika hilo Jijini Dar es saalm na kuondoka na sampo ya bidhaa hiyo ambapo mpaka sasa bado hawajapata majibu sahihi ya hatma yao.
“Baada ya taarifa zetu kuruka kwenye vyombo vya habari siku ya pili tu alitumwa mtu kutoka makao makuu ya TBS Jijini Dar es salaam na niliondoka nae sambamba na sampo ya bidhaa hiyo nahii leo ja (jana)kwenda tena ili kuona hatua gani zimechukuliwa dhidi
yetu”Alisema Pandey.
Aidha alisema hatua hiyo ya kusitisha uzalishaji mbali na kupoteza ajira kwa vijana lakini wamekisababisha hasara kiwanda kwa zaidi ya shilingi Milioni 200 ambazo zinatokana na tani elfu 11 zilizozalishwa kisha kuonekana zipo chini ya kiwango.
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...