Wednesday, 27 September 2017

YALIYOJIRI KIAKO CHA BARAZA LA BIASHARA LA MKOA WA IRINGA

Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Mkoa wa Iringa Amina Masenza, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoawa Iringa akitoa hotuba akionja majani ya stevia yenye sukari nyingi huku Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Iringa Lucas Mwakabungu akishuhudia wakati wa kikao cha Baraza la Biashara la mkoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Valentine mjini Iringa jana.

#######################################
Masenza alitoa rai kwa wajumbe na wadau mbalimbali kutumia fursa vizuri zilizopo mkoani iringa kutengeza ajira kwa wananchi husani vijana. Aidha, ajira hizo zitakuza pato la mwananchi mmoja mmoja kwa kwa taifa nzima.

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akitoa maoni wakati wa kikao cha Baraza la Biashara la mkoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Valentine mjini Iringa jana.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) mkoa wa Iringa Odilo Ngamilaga akitoa maoni wakati wa kikao cha Baraza la Biashara la mkoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Valentine mjini Iringa jana.


Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela na Katibu mtendaji TCCIA (M) James Sizya wakati wa kikao cha Baraza la Biashara la mkoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Valentine mjini Iringa jana.

Makamu mwenyekiti wasindikaji Mafuta ya Alizeti Enok Ndondole akitoa maoni wakati wa kikao cha Baraza la Biashara la mkoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Valentine mjini Iringa jana.

Majani ya aina ya Stevia (Stevia sweetener ) ambayo ni majini ya yanayotumika kutengenezia sukari ambayo yaliletwa na mwekekezaji kutoka Stevia Tanzania limited CEO James Davison wakati wa kikao cha Baraza la Biashara la mkoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Valentine mjini Iringa jana.

Mwekezaji kutoka Stevia Tanzania Limited James Davison (kulia) akitambulisha kilimo cha stevia yaani majani wa kutengenezia sukari wakati wa kikao cha Baraza la Biashara la mkoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Valentine mjini Iringa jana.

Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Mkoa wa Iringa Amina Masenza akionja majani ya stevia yenye sukari nyingi huku Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Iringa Lucas Mwakabungu akishuhudia wakati wa kikao cha Baraza la Biashara la mkoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Valentine mjini Iringa jana.

Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Iringa Lucas Mwakabungu akimkaribisha mweneykiti wa baraza la biashara la mkoa wa Iringa wakati wa kikao cha baraza hilo.



TANAPA: INAKUPELEKA KUTALII HIFADHI YA RUAHA KWA 30,000/- TU KWENDA NA KURUDI




IRINGA: Wananchi wa mikoa ya nyanda za juu kusini wameaswa kutumia fursa ya siku mbili maonesho ya utalii karibu kusini kuitembelea hifadhi ya taifa ya Ruaha iliyopo wilayani Iringa, mkoani Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habari ya meneja masoko wa shirika la hifadhi za Tanzania (TANAPA) aliwaomba wananchi kutumia siku mbili za maonesho ya utalii yanayofanyika kwa wiki moja mjini iringa kwenda hifadhi ya ruaha kwa gharama nafuu.

Alisema kuwa TANAPA kupitia maonesho ya utalii ya karibu kusini inatenga siku mbili maalumu kwa ajili wananchi kwa ajili ya wananchi kutembelea hifadhi hiyo kwa gharama nafuu katika ya septemba 28 -30 mwaka huu.

“Kwa kupitia ofa hiyo kutakuwa na mchango mdogo wa fedha; mtu mzima atalazimika kuchangia Sh 30,000 na mtoto Sh 10,000 tu kumuwezesha kwenda kwa siku moja kutalii katika hifadhi hiyo kubwa kuliko zote nchini,” alisema.

Alisema mchango huo unahusisha gharama ya usafiri, kiingilio cha hifadhini, utalii na muongoza wageni atakayewapitisha katika vivutio mbalimbali ndani ya hifadhi hiyo.

“Tuna nafasi 50 tu tumetoa kwa kupitia ofa hii. Safari ya kwanza itahusisha watu 25 na safari ya pili watu 25 pia, kwahiyo wanaotaka wafike na kujiandikisha katika banda letu lililopo katika viwanja vya Kichangani yanapofanyika maonesho haya,” alisema.

Akizungumzia baadhi ya vivutio vilivyoko katika hifadhi hiyo, Mhifadhi wa Idara ya Utalii Ruaha, Hellen Mchaki alisema Hifadhi ya Ruaha pamoja na wingi wa vivutio inabeba pia historia muhimu ya Chifu Mkwawa, kiongozi wa kabila la Wahehe mkoani Iringa aliyeongoza mapambano dhidi ya wajerumani katika karne ya 19.

Alitaja baadhi ya wanyama waliopo katika hifadhi hiyo kuwa ni kudu wakubwa na wadogo, viboko, mamba, pofu, swala pala, makundi makubwa ya samba, tembo na nyati, chui, mbweha, fisi, twiga, pundamilia na mbwa mwitu.

Akizungumzia idadi ya watalii katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Mchaki alisema mwaka 2012/2013 walipokea watalii wa nje 14,299 na wa ndani 9,094, mwaka 2013/2014 wa nje 13,489 na wa ndani 9,673 na mwaka 2014/2015 wa nje 13,272 na wa ndani 8,291.







WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...