Thursday, 8 September 2016

KUMEKUCHA DODOMA,TIZAMA MAKAZI YA WAZIRI MKUU DODOMA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia kwake ) wakikagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Badhi ya Mawaziri na viongozi wa mkoa wa Dodoma baada ya kukagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016. Katikati ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



SERIKALI YAPITISHA MISWAADA HII KUWA SHERIA



Na Eleuteri Mangi-Maelezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameridhia na kusaini Miswada mitano kutumika kama Sheria kamili za nchi.


Hayo yamesemwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai mara baada ya kufungua Mkutano wa nne wa Bunge la 11 leo mjini Dodoma.


Miswada iliyoidhinishwa na Rais ni pamoja Sheria ya Fedha na Matumizi ya mwaka 2016, Sheria ya Fedha namba 2 ya mwaka 2016, Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya mwaka 2016, Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbambali namba 2 na 4 ya mwaka 2016 na Sheria ya Marekebisho ya Ununuzi ya Umma namba 5 ya mwaka 2016.



Aidha, Mhe. Spika amewakumbusha Wabunge kusoma na kuelewa kila kinachokuja Bungeni ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kibunge ipasavyo kwa niaba ya wananchi waliowatuma kufanya kazi hiyo ili kuwaletea maendeleo.


Wabunge wametakiwa kutekeleza majukumu hayo ya uwakilishi wa wananchi ili waweze kujadili masuala mbalimbali kwa kuzingatia haki, ustahimilivu, busara, hekima na kutumia lugha ya staha katika mijadala ya Bunge.


Vile vile Mhe. Spika amempongeza Naibu Spika Dkt. Tulia Akson kuongoza vema mkutano wa tatu wa Bunge ulioanza Aprili 19 na kumalizika Juni 30 mwaka huu kwa kushirikiana na wenyeviti wa Bunge Andrew Chenge, Mussa A. Zungu na Najima Giga.


Katika hatua nyingine Mhe. Spika amemshukuru Rais Dkt. Magufuli, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Watanzania wote walimuombea alipokuwa kwenye matibabu nje ya nchi pamoja na Madaktari waliomhudumia akiwa kwenye matibabu na kumshukuru Mungu kwa kumwonesha upendo alipokuwa kwenye mapito ya kuugua.


Katika mkutano huo wa Bunge yameulizwa maswali 14 ambayo yalielekezwa kwenye Wizara mbalimbali na kujibiwa kwa llengo la kutolea ufafanuzi masuala yanayotekelezwa kwa Serikali





Mfanyabiasha Leonard Materu (31) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka ya kutuma ujumbe wa kumtishia Rais John Magufuli kupitia mtandao wa WhatsApp.


Materu ambaye ni mkazi wa Moshi Bar Kwadiwani, alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka yake na Wakili wa Serikali, Diana Lukondo mbele ya Hakimu Mkazi Magreth Bankika.


Akisoma mashitaka Wakili Diana alidai, mshitakiwa huyo amefunguliwa kesi hiyo ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa WhatsApp chini ya Sheria ya Mtandao ya mwaka 2015.


Ilidaiwa kuwa, Julai 17, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Materu aliandika ujumbe wenye lengo la kudanganya umma kupitia WhatsApp ukisomeka; “Magu ajiandae tunaenda kupindua mpaka Ikulu.”



Inadaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa na lengo la kumtishia Rais John Magufuli. Baada ya kusomewa mashitaka, mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo, na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.


Mshitakiwa aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja alisaini hati ya Sh milioni tano. Kesi itatajwa tena Septemba 20, mwaka huu.


MKURUGENZI MTENDAJI MPYA WA TACAIDS AJITAMBULISHA KWA WADAU WA UKIMWI




Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids, Dk. Leonard Maboko.



Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko (kushoto), akizungumza na wadau wa ukimwi katika mkutano wa kufahamiana uliofanyika Makao Makuu ya Tacaids Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria (Tacaids), Elizabeth Kaganda na Mkurugenzi wa Ufatiliaji na Tathmini, Dk. Jerome Kamwela.



Wadau wa ukimwi wakimsikiliza mkurugenzi wao mpya.



Wadau wa ukimwi wakimsikiliza mkurugenzi wao.



Mkurugenzi wa wa Habari na Uraghibishi, Jumanne Isango na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Tacaids, Yasin Abbas wakiwa kwenye mkutano huo. 



Taswira ya mkutano huo.


WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...