Baadhi ya watoto yatima wa kituo cha Daru Fatma kinachomilikiwa na taasisi ya kiislamu Dhinureyn (Dhinureyn Islamic foundation) wakimsikiliza naibu meya wa manispaa ya iringa Gervas Ndaki alipotembelea kituo hicho na kutoa msaada wa vyakula. Ndaki alikuwa kiongozi wa msafara wa timu ya manispaa ya iringa pamoja na baraza la madiwani walipotembea kituo hicho kama sehemu ya maadhimisho ua siku ya ukimwi duniani.
Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii katika taasisi ya kiislamu Dhinureyn (Dhinureyn Islamic
foundation) Abbas Upete wakitoa shukrani kwa viongozi wa halmashauri ya manispaa kwa msaada wa vyakula kwa niaba ya taasisi hiyo. Taasisi hiyo ya Dhinureyn inamiliki vituo viwili vya watoto yatima ambavyo ni Daru Fatma ambacho kina watoto yatima wasichana 51 na Daru Bilali kwa upande wa wavulana ambao wapo jumla 50.
Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ilala akikabidhi msaada wa vyakula kwa watoto yatima wa kituo cha Huruma kinachomilikiwa Kanisa ka Kiinjili la Kilutheri Tanzania - Dayosisi ya Iringa leo. Viongozi wa halmashauri ya iringa kwa kushirikiana na baraza la madiwani wa halmashauri hiyo wafanya ziara katika kituo hicho na kutoa msaada wa vyakula kama ssehemu ya maadhisho ya siku ya ukimwi duniani.
Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa
Gervas Ndaki ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ilala akisaini kitabu cha wageni kabla ya kukabidhi msaada wa
vyakula kwa watoto yatima wa kituo cha Huruma kinachomilikiwa Kanisa ka
Kiinjili la Klutheri Tanzania - Dayosisi ya Iringa leo. Viongozi wa
halmashauri ya iringa kwa kushirikiana na baraza la madiwani wa
halmashauri hiyo wafanya ziara katika kituo hicho na kutoa msaada wa vyakula kama ssehemu ya maadhisho ya siku ya ukimwi duniani.
Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa
Gervas Ndaki ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ilala akikabidhi mafuta ya kula lita 20 kwa watoto yatima wa kituo cha Daru Bilali cha Dhinureyn Islamic Foundation leo. Viongozi wa
halmashauri ya iringa kwa kushirikiana na baraza la madiwani wa
halmashauri hiyo wafanya ziara katika kituo hicho na kutoa msaada wa vyakula kama ssehemu ya maadhisho ya siku ya ukimwi duniani.
Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa
Gervas Ndaki (kulia) akipeana mikono na mkuu wa kituo cha watoto yatima Dhinureyn Islamic Foundation, Isaa Shabani baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji ya kituo hicho wakati wa ziara ya viongozi wa
halmashauri ya iringa kwa kushirikiana na baraza la madiwani wa
halmashauri na kutoa msaada wa vyakula kama ssehemu ya maadhisho ya siku ya ukimwi duniani.
Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa
Gervas Ndaki akikabidhi boksi la biskuti kwa watoto wa kituo cha Daru Fatma.