Wednesday, 29 April 2015

KONGAMANO LA UHURU WA HABARI WPFD KUFANYIKA MOROGORO MEI 2-3



Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani (WPFD) yatakayofanyika tarehe 2 mwezi Mei mwaka huu mkoani Morogoro.

Na Modewjiblog team

Wanahabari na wadau wa habari wanatarajiwa kukutana Mkoani Morogoro kwa siku mbili kwa kusanyiko la maadhimisho ya siku ya Uhuru wa habari duniani (WPFD), litakalofanyika katika hoteli ya Nasheera, Mjini Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika), Ndugu Simon Berege alieleza kuwa, kusanyiko hilo la wandishi wa habari na wadau wa habari litafanyika mjini humo Mei 2-3, mwaka huu.

FANYENI REDIO ZENU ZITAMANIKE, WAMILIKI REDIO JAMII WAAMBIWA


Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Bw. Ramadhan Ahungu akiendesha mafunzo ya masoko na mpango biashara kwa viongozi wa redio jamii nchini wakati kuhitimisho la warsha ya awamu ya kwanza ya mradi wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo Redio hizo katika matumizi ya Tehama na Mawasiliano iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO ambayo imefanyika katika kituo cha Redio jamii Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.


Na Mwandishi wetu, Mwanza


WAMILIKI wa redio za jamii wametakiwa kujenga taswira njema za redio zao ikiwa wanataka redio zao zitamanike na kutumiwa na wadua mbalimbali wa maendeleo nchini.


Kauli hiyo imetolewa na Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Ramadhan Ahungu.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...