Wednesday, 10 February 2016

ZIJUE AINA TANO ZA MITUNGI YA KUZIMIA MOTO



1.MTUNGI WA MAJI (WATER)

Mtungi huu una rangi NYEKUNDU wote. Mtungi huu hautumiki kuzimia moto wa umeme au mafuta, ila unazima aina nyingine zote za moto. Mtungi huu ni hatari sana kuutumia kwenye moto wa umeme

2. MTUNGI WA KABONDAYOKSAIDI (CO2)

Mtungi huu hutumika kuzima aina nyingi za moto ukiwamo umeme. Ni mwekundu lakini una lebo NYEUSI kama kitambulisho chake. Wakati wa kuzima moto usishike mwishoni mwa bomba kwakuwa gesi inayotoka ni ya baridi sana unaweza kuganda.

3. MTUNGI WA POVU (FOAM)

Mtungi huu una rangi ya KRIMU kama kitambulisho chake. kwingine kote ni mwekundu. Unazima moto wa vitu vya majimaji pamoja na vitu vigumu.

4. MTUNGI WA PODA (POWDER)

Mtungi huu una lebo ya BLUU kama kitambulisho chake. Unaweza kuzima moto wa gesi, majimaji, na vitu vigumu.

5. MTUNGI WA DAWA/KEMIKALI (Chemical)

Mtungi huu una lebo ya NJANO kama kitambulisho
chake. Unazima aina nyingi za moto ukiwamo wa mafuta.

KUMBUKA: Mtungi wa kuzimia moto si kwaajili ya kuufanya moto usiendelee kuwaka bali kukufanya upate njia ya kujiokole hasa ukiwa ndani ya nyumba yako. Kwa udogo wa ule mtungi huwezi kuzima moto unaunguza nyumba nzima. Kama moto umezuia mlango, chukua mtungi elekeza pale mlangoni ili moto uzimike upate kwa kutokea

Unapozima elekeza bomba la tingisha chini ulipo mot sio juu ya moto.Imeandaliwa na RSA na Dj sek Blog

Mitungi ya zimamoto hutofautishwa kutokana na lebo za rangi zake (codes). Mfano Dry powder-Bluu; Kabondayoksaidi-Nyeusi. Na kila mmoja una kazi maalumu tofauti na mwingine. Penginepo hutumia herufi A,B,C





Herufi A ni kwa mtungi unaozima moto wa karatasi, mbao, plastiki, nguo, mipira na takataka.

Herufi B ni kwa mtungi unaozima moto wa gesi, mafuta, rangi na solventi.

Herufi C ni kwa mtungi unaozima moto wa nishati kama umeme na mafuta. 









NEC YASEMA ELIMU YA MPIGA KURA HAIKUWAFIKIA BAADHI YA WANANCHI NCHINI




Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini NEC imebainisha kwamba, ukosefu wa elimu ya kutosha kwa Wapiga Kura, ulisababisha mapungufu mbalimbali kujitokeza katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 Mwaka jana.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani (Pichani juu) aliyasema hayo jana Jijini Mwanza, katika Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.

Ramadhani alisema katika baadhi ya Kata nchini, kulitokea mapungufu kadhaa katika zoezi la kupiga kura ikiwemo Kura kuharibika kutokana na wapiga kura kuchora michoro na alaza zisizostahili katika karatasi ya kupigia kura huku baadhi yao wakiandika matusi katika karatasi hizo.

Hata hivyo Kailima alitanabaisha kwamba, zoezi la utoaji wa elimu kwa mpiga kura, lilishindwa kufanikiwa zaidi kutokana na baadhi ya Asasi za kiraia nchini kutoa elimu kinyume na mwongozi wa NEC, ambapo baadhi ya Asasi hizo zilikuwa zikitoa elimu ya mpiga kura kwa kuangazia zaidi matakwa ya wafadhiri wake.

Edwin Soko ambae ni mmoja wa Wadau kutoka Asasi zilizohudhuria katika Mkutano huo ambao umejumuisha Asasi mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa, amesema kuwa katika Uchaguzi wa Mwaka jana, Asasi nyingi hazikuweza kuyafikia maeneo mengi hususani vijijini kwa ajili ya Kutoa elimu ya Mpiga kura, hii ikiwa ni kutokana na ukosefu wa fedha ambapo wameishauri Serikali kuwa na utaratibu wa kutoa ruzuku kwa asasi hizo ili kutoa elimu hiyo katika chaguzi zijazo.

Kando ya Tathmini hiyo, Suala la Kuahirishwa kwa Uchaguzi Visiwani Zanzibar likajitokeza, ambapo Wanahabari walitaka kujua sababu za Uchaguzi huo kuahirishwa, na hapo ndipo Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka NEC akatumia tena fursa hiyo kufafanua kwamba Uchaguzi Visiwani Zanzibar uliahirishwa na Tume ya Uchaguzi Visiwani humo ZEC kutokana na tume hiyo kubaini kasoro kadhaa katika karatasi zake za wapiga kura, kasoro ambazo
hata hivyo hazikujitokeza katika karatasi zilizokuwa zikisimamiwa na Tume ya Uchaguzi nchini NEC ikizingatiwa kwamba ZEC na NEC ni tume mbili tofauti zisizoingiliana katika majukumu.


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani akifungua Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani akizungumza na Wanahabari Jijini Mwanza nje ya Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani akizungumza na Wanahabari Jijini Mwanza nje ya Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.


Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.


Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.


Wanahabari na Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.


Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.


Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Geita.


Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Kagera.


Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Mwanza.


Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Shinyanga.


Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Mara.


Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Simiyu.




MAGAZETI YA LEO ALHAMISI

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...