Wednesday, 10 February 2016

NEC YASEMA ELIMU YA MPIGA KURA HAIKUWAFIKIA BAADHI YA WANANCHI NCHINI




Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini NEC imebainisha kwamba, ukosefu wa elimu ya kutosha kwa Wapiga Kura, ulisababisha mapungufu mbalimbali kujitokeza katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 Mwaka jana.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani (Pichani juu) aliyasema hayo jana Jijini Mwanza, katika Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.

Ramadhani alisema katika baadhi ya Kata nchini, kulitokea mapungufu kadhaa katika zoezi la kupiga kura ikiwemo Kura kuharibika kutokana na wapiga kura kuchora michoro na alaza zisizostahili katika karatasi ya kupigia kura huku baadhi yao wakiandika matusi katika karatasi hizo.

Hata hivyo Kailima alitanabaisha kwamba, zoezi la utoaji wa elimu kwa mpiga kura, lilishindwa kufanikiwa zaidi kutokana na baadhi ya Asasi za kiraia nchini kutoa elimu kinyume na mwongozi wa NEC, ambapo baadhi ya Asasi hizo zilikuwa zikitoa elimu ya mpiga kura kwa kuangazia zaidi matakwa ya wafadhiri wake.

Edwin Soko ambae ni mmoja wa Wadau kutoka Asasi zilizohudhuria katika Mkutano huo ambao umejumuisha Asasi mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa, amesema kuwa katika Uchaguzi wa Mwaka jana, Asasi nyingi hazikuweza kuyafikia maeneo mengi hususani vijijini kwa ajili ya Kutoa elimu ya Mpiga kura, hii ikiwa ni kutokana na ukosefu wa fedha ambapo wameishauri Serikali kuwa na utaratibu wa kutoa ruzuku kwa asasi hizo ili kutoa elimu hiyo katika chaguzi zijazo.

Kando ya Tathmini hiyo, Suala la Kuahirishwa kwa Uchaguzi Visiwani Zanzibar likajitokeza, ambapo Wanahabari walitaka kujua sababu za Uchaguzi huo kuahirishwa, na hapo ndipo Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka NEC akatumia tena fursa hiyo kufafanua kwamba Uchaguzi Visiwani Zanzibar uliahirishwa na Tume ya Uchaguzi Visiwani humo ZEC kutokana na tume hiyo kubaini kasoro kadhaa katika karatasi zake za wapiga kura, kasoro ambazo
hata hivyo hazikujitokeza katika karatasi zilizokuwa zikisimamiwa na Tume ya Uchaguzi nchini NEC ikizingatiwa kwamba ZEC na NEC ni tume mbili tofauti zisizoingiliana katika majukumu.


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani akifungua Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani akizungumza na Wanahabari Jijini Mwanza nje ya Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani akizungumza na Wanahabari Jijini Mwanza nje ya Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.


Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.


Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.


Wanahabari na Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.


Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.


Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Geita.


Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Kagera.


Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Mwanza.


Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Shinyanga.


Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Mara.


Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Simiyu.




No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...