Saturday, 21 October 2017
SAUTI YA TUNDU LISSU YAMTOA MACHOZI HADHARANI ASKOFU HUYU ...
Moshi. Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo amesimulia alivyobubujikwa machozi baada ya kusikia sauti ya Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu.
Dk Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, amesema hayo baada ya Jumatano Oktoba 18,2017 Lissu kutoa salamu akiwashukuru Watanzania kupitia video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Lissu anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7,2017 mjini Dodoma.
Soma: Lissu: Mungu alisema huyu hatakufa
Sauti ya Lissu katika video hiyo ilikuwa ni ya kwanza kusikika tangu apelekwe jijini Nairobi Septemba 7. Alisikika akiwashukuru madaktari wa Nairobi na Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kwa kuokoa maisha yake.
Pia, amewashukuru viongozi wa dini na wananchi kwa kumuombea, na taasisi za kitaaluma ndani na nje ya nchi ikiwemo TLS ambazo zilionyesha mshikamano mkubwa.
Akizungumza na Mwananchi, Askofu Shoo amesema alijikuta akitokwa machozi aliposikia sauti ya Lissu, akisema kupona kwake ni onyo kwa wale waliohusika.
“Ninazidi kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyomuokoa na anavyozidi kumpa uponyaji. Kupona kwa Lissu ni jibu la Mungu na onyo kwa wale wote waliohusika. Mungu amesema hapana,” amesema.
Askofu Shoo amesema, “Mwenye masikio na asikie. Uhai wa mwanadamu ni kitu cha kuheshimu. Tusijaribiwe kujichukulia madaraka ya kuondoa uhai wa mtu hata kama uwezo tunao kwa maana Mungu hataki na wala hataacha kumwadhibu yeye aondoaye uhai wa ndugu yake kwa hiana.”
Job Ndugai kuondolewa Bungeni ?
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kuwa katika Bunge ambalo linatarajiwa kuanza Novemba 7, 2017 anakusudia kupeleka hoja ya kumuondoa Spika wa Bunge, Job Ndugai
Msigwa amesema hayo leo kupitia moja ya mtandao wake wa kijamii na kusema kuwa kwa kuzingatia kanuni ya 137 ya kanuni za kudumu za Bunge atapeleka hoja yake hiyo ya kumuondoa Spika wa Bungue.
"Ninakusudia kupeleka hoja ya kumuondoa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Job Ndungai, kwa kuzingatia Kanuni ya 137 ya kanuni za kudumu za bunge ina complement ibara ya 84 (7) (d) ya Katiba" alisema Msigwa
Mbunge Peter Msigwa ni kati ya wabunge ambao wamekuwa wakilalamika kuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai amekuwa akiendesha bunge kwa shinikizo na upendeleo na kudai kuwa hastahili kuendelea kuongoza kiti hicho.
Source: EATV
KUELEKEA UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO...
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Ramadhani Kailima.
WAKATI ikiwa imebakia mwezi mmoja tu kuelekea kwenye uchaguzi mdogo wa marudio wa udiwani kufanyika kutokana na kata mbali mbali kuwa wazi,TUME ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), imesema hati ya kiapo cha mahakama ya kudhibitisha majina ya mtu(Affidavit), haitatumika katika kupiga kura kwenye uchaguzi mdogo wa kata 43.
Hati za kupigia kura zitakazotumika katika uchaguzi huo ni leseni ya udereva, Kitambulisho cha Utaifa na hati ya kusafiria.
Hayo yamebainishwa Dar es Salaam leo na Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima akizungumza na TUMBUSI BLOG na kwamba matumizi ya hati hizoyatapunguza biashara ya watu kununua au wizi wa vitambulisho vya kupigia kura na kuongeza uwanda mpana wa mtu kupiga kura.
"Hati ya kiapo cha mahakama cha kuthibitisha majina yako na taarifa zako haitaruhusiwa kupigia kura katika uchaguzi huu mdogo, kuna hati tatu tu ambazo zitaruhusiwa kutumika,"amesema.
Kailima amesema hati mahakamani haitatambuliwa na kutoruhusiwa kwa namna mbili ikiwemo kutokuwa na mtiririko wa majina ya mpiga kura na kwamba yanatakiwa mtiririko huo ufanane kwa maneno na herufi.
"Huna kitambulisho cha NIDA, leseni ya udereva, hati ya kusafiria umekwenda mahakamani umeapa haitakubalika, Tume kwa mamlaka iliyonayo imesema kwa mujibu wa Sheria mwenye vitambulisho vitatu na hivi vitatumika kwenye uchaguzi mdogo wa Kata 43,"amesema.
Amesema ukifika uchaguzi Mkuu, Tume itatoa maelekezo mengine na kwamba hayo ni maelekezo ya uchaguzi mdogo wa Kata hizo kutokana na matakwa ya sheria na kutokuboreshwa kwa daftari la kudumu la wapiga kura.
"Hii ndiyo tunaanza kupiga kura kwa hati hizo tatu, kutokana na kutokuboresha daftari,ili isipoteze haki ya mtu kupiga kura na tumeona uwanda wa NIDA ulipofika watu wanaweza kuwa na vitambulisho, pia leseni za udereva watu wengi wanazo ikiwemo maeneo ya vijijini madereva wa pikipiki wanazo"amesema.
Amesema fomu za uchaguzi huo imeanza kutolewa leo hadi Oct 26,mwaka huu ambazo zinapatikana kwa Mkurugenzi wa Halmashauri au Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata.
"Mwisho Oct 26 mwaka huu saa kumi jioni, baada ya hapo fomu za wateule zitawekwa sehemu za wazi ili kutoa fursa ya kuwekewa pingamizi ambapo wanaoruhusiwa kufanya hivyo ni Mgombea mwenza wa Udiwani kwenye Kata husika.
"Si kutoka Kata nyingine, Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Msajili wa Vyama vya siasa kutokana na sheria za gharama za uchaguzi na kama msimamizi wa uchaguzi akimwekea pingamizi mgombea itabidi aweke rufaa ikishindikana inaamia NEC iwapo kama pande mojawapo ikishindwa kukubaliana na maamuzi ya kamatiya rufaa ya pingamizi itakuwa kesi baada ya uteuzi.
Katika uchaguzi huo wapiga kura zaidi ya 300,000 wanatarajia kupiga kura katika vituo zaidi ya 800 na Kata 43.
Miaka 100 ya Skauti: Mkuu wa wilaya Sophia Mjema atoa agizo la uanzishwaji wa klabu za skauti kila...
Mkuu wa wilaya akizindua mapango wa mawasiliano kwa njia ya redio maalumu njia ya upepo na inteneti kwa skauti ‘Jamboree on the Air (JOTA),
Mkuu wa wilaya ya ilala Sophia Mjema Akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake akiwa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wilaya ya ilala.
Na Michael Utouh
Mkuu wa wilaya ya Ilala ambae ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya wilaya akikagua gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake na wanafunzi wanaopata mafunzo maalumu ya scout alipofika kwa ajili ya kufunga makambi yao ya mafunzo siku ya leo.
Mkuu wa wilaya akiwahutubia wanafunzi wa scout.
Mmoja wa wakilishi wanafunzi wanaopata mafunzo ya scout wakisoma risala yao mbele ya mgeni rasmi.
Mkuu wa wilaya akikapewa maelekezo juu ya mpango anzilishi wenye lengo la kumkomboa mwana scout na baadhi ya mambo mengi kama vile Elimu nk.
Akitembezwa pamoja na kukagua baadhi ya makambi ambayo wameyaweka wanafunzi hao kwa ajili ya mafunzo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amemuagiza afisa elimu wa wilaya ya Ilala kuhakikisha kila shule inafanya uandikishaji wa wanafunzi kwa ajili ya mafunzo ya vikundi vya skauti nakila shule ihakikishe inatoa mwalimu mmoja kwa ajili ya kusimamia vikundi hivyo.
Mjema ameyasema hayo katika kuadhimisha miaka 100 ya skauti tangu kuanzishwa kwake 1917 sambambana kuzindua wiki mawasiliano ya anga kwa njia ya upepo na inteneti kwa skauti ‘Jamboree on the Air (JOTA), Jamboree on the Internet (JOTI)’yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Pugu Jijini Dar es Salaam.
“Ikama ya walimu wa skauti ni ndogo natoa agzio kwa afisa elimu kufanya uandikishaji wa skauti wakike na wakiume katika kila shule na kuhakikisha kila shule kunakuwa na mwalimu mmoja ambaye atakuwa anawafundisha skauti hao” Amesema Mkuu wa wilaya
DC Mjema ameeleza kuwa skauti wengi ni vijana wakifundishwa maadili mema Tanzania itakuwa ni yenye umma bora na watu wake watakuwa na uzalendo na Taifa la Tanzania.
“Skauti wengi ni Vijana hivyo ni wajibu wao kutengeneza ulimwengu bila madawa ya kulevya, bila maovu , kutengeneza skauti wazalendo wenye tija na Taifa la Tanzania, pia wanapopata fursa mbalimbali za nje ya nchi wasisite kuitangaza Tanzania kwa kueleza mema ya Tanzania ikiwemo Amani, Muungano na Rasilimali zilizopo” Amesema.
Pia DC Mjema ametoa wito kwa watoto na skauti wote pindi wanapoona matukio ya kidhalilishaji au kufanyiwa watoe taarifa kwa mamlaka kwa mamlaka husika kwani serikali ipo kwa ajili yao na itawalinda.
“Wenyeviti wa Serikali za Mtaa, Wakuu wa Wilaya, Mawaziri, mpaka ngazi ya juu ya Rais chini ya Rais John Pombe Magufuli tutahakikisha tunazilinda na kuzitetea haki za mtoto hivyo wasiogope kutoa taarifa za unyanyasaji kijinsia hata kama wakitishiwa maisha yao” Amesema.
Katika hatua nyingine DC Mjema amehaidi kushughulikia moja ya changamoto iliyotolewa na wawakilishi wa uongozi wa skauti kuhusiana na eneo la kambi na eneo kwa ajili ya kilimo ambapo amewahakikishia uwepo wa maeneo hayo kwa kumuagiza Mkurugenzi kuwapa kipaumbele pale watakapo ainisha maeneo kwa ajili ya viwanda vidogo kwani kufanya hivyo ni kuwakwamua kiuchumi.
“Namuagiza Mkurugenzi kushughulikia suala la eneo la kilimo, pia ni vyema mkaja ofisini kwangu siku ya Alhamisi ili niwakutanishe na Afisa Maendeleo kwa ajili ya kujadili na kufikia malengo yenye tija kwa skauti na taifa kwa ujumla” Amesema.
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
Habari ndugu msomaji wetu wa blog, Natumaini unaendelea vyema. Leo tutaanza kujifunza kilimo cha bora cha nyanya, na tutaanza kufahamu vit...