Mhariri Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akiwasilisha mada kuhusu namna ya kufanya mahusiano ya kikazi kati ya bunge na wanahabari kwa baadhi ya wabunge, wahariri na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Picha na Geofrey Adroph
Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza jambo mbele ya baadhi ya wabunge pamoja na baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waliofika katika semina ili kujadili jinsi ya kutengeneza mahusiano ya kikazi kati ya Bunge na wanahabari yatakayoleta ukaribu kwa pande zote.
Baadhi ya wabunge wakichangia mada kuhusu kutengeneza mahusiano ya kikazi kati ya Bunge(wabunge) na wanahabari pamoja na kutoa maoni yao ili kuboresha utoaji wa habari kwa wananchi boila kujali itikadiza kivyama.
Mhariri Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akijibu maswali kutoka kwa wabunge katika mkutano uliowakutanisha wabunge, wahariri na waabdishi wa habari katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo.
Mhariri mtendaji wa Jamhuri Media, Deodatus Balile akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waandishi pamoja na wabunge walioudhuria mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Hazina ndogo mjini Dodoma.
Mmoja wa waandishi wa habari akitoa changamoto anazozipata kwenye kazi zake za kila siku za kuripoti habari mbalimbali
Baadhi ya wabunge, wahariri na waandishi wa habari wakiwakwenye mkutano
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Wakfu wa Taasisi Huru za Uwazi Afrika (OSIEA) wamewakutanisha wabunge pamoja na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
Mkutano huu ulikuwa na lengo la kuwajengea Wabunge na Wanahabari uhusiano mzuri katika utendaji wao wa kazi. Bunge na Vyombo vya Habari ni Mihimili miwili ya dola (Mmoja ukiwa Rasmi na mwingine usio Rasmi) inayotegemeana sana katika utendaji wake wa kazi.
Kutokana na kazi kubwa ya Bunge ambayo ni kutunga sheria na kuwakilisha Umma katika mijadala mbalimbali ya maendeleo katika ngazi za Taifa na Jimbo lazima kutumia vyombo vya Habari kwenye kazi ya kutafsiri mipango na mikakati mbalimbali inayofanywa na Bunge katika lugha ambayo mpiga kura/mwananchi wa kawaida anaweza kuelewa. Lengo kuu likiwa ni kuharakisha maendeleo ya mtu mmoja mmoja na jamii nzima.
Katika siku za karibuni kumetokea changamoto mbalimbali katika utendaji kazi wa muhimili huu rasmi na muhimili huu usiokuwa rasmi, na hasa kutoaminiana na kushutumiana kwa namna moja ama nyingine. Kutokana na changamoto hizo hakuna budi kwawaandishi wa habari paamoja ili kujadili changamoto na kuja na suluhisho la changamoto hizo.
Semina hiyo imeshirikisha watu 55 ikiwa ni pamoja na wabunge mbalimbali toka vyama vyote, Wahariri wa vyombo Habari vilivyoko Dodoma na Bureau Chiefs wa vyombo vya Umma na Binafsi vilivyopo Dodoma.