Na Friday Simbaya,
S ongea
PAROKO Padre Joseph Ndimbo wa Parokia ya Peramiho Jimbo Kuu
la Songea aliwaasa waombolezaji kuacha
mara moja tabia kugombeana maeneo ya kuzika marehemu.
Alisema kuwa kuna mtindo umezuka wanandugu kuvutana wapi
wamzike marehemu na kuongeza kuwa huku ni kumdhalilisha marehemu.
Pd. Ndimbo alisema hayo Jumamosi wakati wa mazishi ya aliyekuwa
mwenyekiti wa Tanzania labour Party (TLP)wilaya ya Songea, Bw. Kalo Kombe
katika makaburi ya Liangano karibu na Kijiji cha Lipinyapinya Kata ya Peramiho.
Alisema kuwa sio tabia nzuri kwa wanandugu kugombeana maiti
, kumbe maeneo yote yanafaa kuzikia.
“Imezuka tabia katika jamii ya watu kugombania maiti yaani
mvutanao wa watu wawili kugombania maiti wakati wa mazishi kila mtu anataka kuzika mahali pake, huku
kote ni kuhangaika na kumtesa marehemu. Kuzikwa ni kuzikwa tu hata kama
atazikwa Peramiho ‘A’ au Peramiho ‘B’,” alitoa mfano paroko huyu.
Aidha, paroko alisisitiza kuwa watu wasitafute mchawi kwamba
marehemu amerogwa bali waendelee kumuonbea marehemu kuwa astarehe kwa amani kwa
Mungu Baba.
Aliwaambia waombolezaji kuwa kuumwa kwa mwanadamu ni mateso
kwa sababu mtu yeyote atakayependa maisha lazima afe lakini anayechukia maisha
ataishi maisha ya milele.
Aliongeza kuwa WaTanzania vilevile tunakiwa kufanya kazi kwa bidii sio kutafuta kwa njia
ya mkato. Alisema kuwa mtu lazima apate mateso ili afe kama vile mtu anatakiwa
kuteseka ili apate chakula. Aliongeza kuwa mateso ni sehemu ya maisha ya
binadamu, kwa hiyo mtu akiuugua ni mateso, vilevile mtu kuchapakazi kwa bidii
ni mateso pia ili kuweza kuishi maisha bora.
“Hakuna maisha bora kama hujishughulishi kwa sababu maisha
bora huja kwa kufanyakazi kwa bidii na kuaacha uvivu,” alisema paroko. “Asiyefanya
kazi na asile huo ndio wito wangu kwenu” alisisitiza.
Mwenyekiti huyo wa TLP
alifariki dunia juzi katika hospitali ya Misioni ya St. Joseph Peramiho
baada ya kuugua vidonda vya tumbo kwa muda mrefu.
Marehemu Kombe alistaafu katika Jeshi la Polisi tangu 1995,
ambapo alifikia renki ya inspector kabla ya kustaafu na kuanza kujishughulisha
na mambo ya siasa. Marehemu Kombe alipenda magauzi ndiyo maana alijiunga na
upinzani, alikuwa anaishi maeneo ya Mjimwema katika Manispaa ya Songea mkoani
Ruvuma.