Wednesday, 11 March 2015
BREAKING NEWS: BASI LA MAJINJA LAUA ZAIDI YA ABIRIA 40...!
Hali ya sintofahamu baada ya kontena kuangukia Basi T 438 CDE lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Dar. Abiria 48 wamefariki papohapo wawili wamenusurika akiweno mama na mtoto. Eneo la ajiri hiyo linaitwa Changarawe nje kidogo ya mji wa Mafinga.
Ajali imetokea changarawe Mafinga mkoani Iringa basi la Majinja lilikuwa linatokea Mbeya kwenda Dar limeangukiwa na kontena muda huu na watu wengi wanakadiriwa kufariki na hali ni mbaya sana.
Taarifa za awali kutoka jeshi la polisi mkoani Iringa zinaeleza kuwa basi la kampuni Majinja lililolaliwa na lori lilikuwa limebeba jumla ya watu 49, idadi hiyo ni pamoja na dereva na kondakta wa basi hilo.wengi wa watu hao wamefariki dunia idadi ya majeruhi haijajulikana bado.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa kwenye mizigo mingi ya abiria waliokuwa kwenye basi hilo kumepatikana madaftari mengi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam hivyo jeshi hilo linaendelea kufanya mawasoliano ma wamiliki wa gari hilo ili kujua kama lilikuwa limekodishwa kubeba wanafunzi wa chuo hicho ama ni mchanganyiko wa kawaida wa abiria.
IRINGA KIBIKI CHILDREN CUP KUANZA KUTIMUA VUMBI IRINGA
MRATIBU WA KIBIKI CUP HARUNA SALEH AKIWA NA MDAU WA SOKA FRANK KIBIKI
MRATIBU WA KIBIKI CUP HARUNA SALEH AKIWA NA MDAU WA SOKA FRANK KIBIKI na wanahabari
NA MWANDISHI WETU, IRINGA
LIGI inayoshirikisha watoto walio chini ya umri wa miaka 16, inaloitwa Iringa Kibiki Childrens Cup 2015 yenye lengo la kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino) inatarajia kuanza kutimua vumbi Jumamosi ikishirikisha timu nane za manispaa ya Iringa.
DAMPO LA MTAA WA IDUNDA NI SHIIIIDA...!
Wakazi wa Manispaa ya Iringa wakipita haraka haraka kwa kuongopa harufu ya dambo lililopo mtaa wa Idunda katika Kata ya Mtwivilla kutokana wa kazi wa eneo hilo kupita taka hadi barabarani, mbali ya Manispaa ya Iringa kuongoza kitaifa kwa usafi mwaka 2014.Wananchi wengi wameonyesha kukerwa na dambo hilo.
Kata ya Mtwivilla ni moja kata ambazo zipo kwenye mradi wa usafi wa mazingia unaofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya (EU) uliyopewa jina la 'Usafi Iringa' wa miaka mitano.
Lengo la mradi huu ni kuimarisha afya na hali ya usafi katika maeneo hayo ya pembezoni kwa kuangalia zaidi masuala ya mazingira na uendelevu wa kijamii na uchumi.
FRANK KIBIKI:VIJANA MSIKUBALI KUTUMIKA KISIASA...!
Mwanahabari Frank Kibiki (wa pili kutoka kulia) akibadilishana mawazo na wanahabari wenzako jana walipokutana katika jengo la NSSF-Akiba House ambapo karibu na ofisi za nipashe na majira. |
MWANAHABARI FRANK KIBIKI ambaye pia nimtangaza nia ya ubunge katika Jimbo la Jringa mjini kupitia tiketi ya CCM amewataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
MWANAHABARI FRANK KIBIKI ameeleza kuwa wanawake waondoe hofu ya kugombea hasa kukiwa na ushindani wa wagombea wanaume kwa kuogopa kuchafuliwa kwa mambo yasiyokuwepo.
Ameendelea kusema kuwa wananchi wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na badala yake wachague viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka katika chama chochote.
Aidha ameongeza kuwa viongozi wawe na sera za kutekelezeka ili kuwatendea haki wapiga kura wao hali itakayowafanya waaminike katika jamii.
Mbali na hayo MWANAHABARI FRANK KIBIKI amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa kiongozi kutokana na sera za chama chake.
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
Habari ndugu msomaji wetu wa blog, Natumaini unaendelea vyema. Leo tutaanza kujifunza kilimo cha bora cha nyanya, na tutaanza kufahamu vit...