Na Friday Simbaya
MSEMAJI Mkuu wa shirika la TECONAREMAP Bw, Ochieng Anudo amesema kuwa Idara ya uchunguzi na upelelezi ya shirika
Mali anazodaiwa kulipwa Bi, Mwanaidi kwa kutmia cheti feki hicho cha ndoa akidai ametelekezwa ni mashamba hekari 4, ng'ombe 30, mbuzi saba, kuku 20, bata 30 meza moja, mapipa ya ujazo manne pamoja na vyombo vingine vya ndani na kumwacha Bw, Hussein Dodo akiwa masikini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake mjini Iringa Bw, Ochieng alisema ofisi yake ilipokea malalamiko ya kuhujumiwa kwa haki za mazingira mtu kutoka kwa Bw, Hussein Dodo ambaye ni mkazi wa wilaya ya Babati akidai kuwa Bi, Mwanaidi Musa hakuwa mke wake na kuwa cheti cha ndoa alichotumia hakikuwa halali.
Alisema kuwa baada ya taarifa hizo idara yake ya uchunguzi na upelelezi wa shirika hili ilifanya uchunguzi wa kina ambapo walibaini cheti hicho hakikuwa halali ambapo njama zilitumiwa kwa kupitia cheti bandia hicho ili Bi, Mwanaidi ajipatie
Alisema kuwa walipokea pia barua kutoka kwa Katibu wa Baraza la Usuluhishi la BAKWATA la wilaya ya Babati iliyosainiwa na Bw, Abdi Isuja yenye kumbukumbu namba BKT/BBC/BU/2/20 ya tarehe 23 June 2010 ambayo inamtaka Bw, Hussein Dodo amfikishe kwenye mkono wa sheria kutokana na kutumia cheti feki cha ndoa ili kujipatia mali za udanganyifu kwa kudai kuwa amemtelekeza muda mrefu.
"Hivyo kwa hati hiyo ilivyo inaonesha udanganyifu umefanyika kwa Bi, Mwanaidi kutumia cheti feki cha ndoa kuihadaa BAKWATA ili alipwe mali wakati hakuwa mwanandoa na kwa kuwa Mzee Dodo ameadhirika katika mazingira mtu anatakiwa kufikishwa mbele ya sheria ili Bi, Mwanaidi arudishe mali na fidia zote alizosababisha", ilieleza sehemu ya barua hiyo.
Bw, Ochieng alisema kuwa awali bw, Hussein Dodo alifika kwenye ofisi za TECONAREMAP na kwa kuwa shirika lake linafanya kazi mwa msaada wa sheria, ili aweze kusaidiwa kuzipata haki zake ambazo amepokonywa kwa njama na mwanamke huyo.
Aliongeza kuwa shirika hilo linatoa msaada wa sheria ili kuwasaidia watu waliopoetza haki zao kwa kuhujumiwa kupata haki zao ambao wamehujumiwa na kuweza kuzipata na kuongeza kuwa ndipo kamati yake ya uchunguzi na upelelezi ilipofanya kazi kwa kushirikiana na BAKWATA wilaya ya Babati hadi kubaini udanganyifu huo.
Akizungumzia swalahilo kwa njia ya simu Katibu wa Baraza la Usuluhishi la BAKWATA la wilaya ya Babati Bw, Abdi Isuja alikiri kupokea kesi ya Bi Mwanaidi Musa akidai kutelekezwa na Bw, Hussein Dodo ambayo ilisababisha kufikiwa maamuzi ya kuchukuliwa mali isivyo halali.
"Amekiri na kusaini mbele ya baraza letu kimaandishi katika barua yake ya tarehe 5 June 2010 kuwa ameihadaa baraza kwa kuonesha cheti ambacho siyo sahihi, na kutokana na barua hiyo baraza la BAKWATA tumemwandikia Bw, Dodo aende kwenye vyombo vya sheria ili haki zake alizohujumiwa arejeshewe", alisema Katibu Abdi Isuja.
Bw, Isuja alisema kuwa baada ya kutumia cheti hicho feki Bi, Mwanaidi alichukua mali kutoka kwa Bw, Dodo zikiwemo ng'ombe 30, shamba ekari Nne, mapipa manne, mbuzi saba, kuku 20, bata 30 pamoja na vyombo vingine vya ndani amesema kuwa maamuzi hayo yalikuwa siyo sahihi, hivyo Bw, Hussein Dodo ameshauriwa kwenda kwenye vyombo vya sheria ili azipate haki zake.
Aidha Afisa wa TECONAREMAP NA MSAADA WA SHERIA Bw, Ochieng Anudo ametoa wito kwa watu ambao wanahujumiwa haki zao kuyatumia mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi kwa msaada wa sheria ambayo yatawasaidia kutafiti hadi waweze kuzipata haki zao
Aliongeza kuwa kwa kuwa Bi, Mwanaidi amemvunjia haki za kibinadamu na kukiri mbele ya baraza lake na shirika hilo baada ya uchunguzi walioufanya hatua za kisheria zinatakiwa zichukuliwe juu yake ili kuondoa malalamiko ambayo serikali inatupiwa kuwa haifanyi kazi wakati watu wanatumia mbinu zao kuhadaa ili kujinufaisha.
Akizungumzia swala

Bi Mwanaidi Musa alipohojiwa alikiri kuihadaa kuwa niliihadaa baraza la BAKWATA kuwa ni hati ya kiisilamu kwa kuwapelekea cheti ambacho nilighushi na kuonesha kuwa alifunga ndoa na Bw, Hussein Dodo 22 Februari 1968 wakati siyo kweli.
“Nakiri kuwa cheti hiki cha ndoa siyo sahihi nilighushi ili nipate mali za Bw, Dodo, pia nakiri nililihadaa baraza hilo kwa hati hiyo ya ndoa kuwa ilitolewa na ni ya kiisilamu wakati siyo kweli”, alisema Bi, Mwanaidi na kuongeza kuwa alifikia maamuzi ya kutumia mbinu hizo baada ya Bw, Hussein Dodo kutompa haki zake pamoja na watoto wake ambao alizaa naye.
Aidha Bi, Mwanaidi alisema kuwa awali walikuwa wameoana na Bw, Dodo lakini walitengana baada ya kupewa taraka kisheria 1968 ila alitumia mbinu hizo ili apate mali kutokana na wakati akipatiwa talaka hakuweza kuzipata, alisema Bi Mwanaidi Musa
Ameliomba baraza la BAKWATA limsaidie ili apate haki hizo ili aweze kuwatunza watoto wake ambao alizaa na Bw, Hussein Dodo na kuongeza kuwa watoto hao kwa sasa hawana msaada wowote ndiyo maana alifikia maamuzi hayo.
Akizungumza leo kwa simu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Manyara RPC Parmena Sumari alipohojiwa alikiri kupokea barua katika ofisi yake ya madai ya Bi Mwanaidi Musa kutumia cheti cha ndoa cha kughushi na kujipatia mali isivyo halali na kuongeza kuwa ni mapema mno kulizungumzia lakini uchunguzi utafanyika ili kubaini ukweli wa jambo hilo.
"Ni kweli tumepokea barua yake inayodai Bi Mwanaidi hivyo polisi watafanya uchunguzi wa kina na kwa kuwa kughushi cheti ni kosa la jinai endapo Bi, Mwanaidi atapatikana na hatia hiyo atafikishwa mbele ya mkono wa sheria", alisema Kamanda Sumari.