Tuesday, 15 November 2016

SERIKALI KUBORESHA MITAMBO YA KUCHAPISHA NYARAKA YA KIWANDA CHA UHAMIAJI KIJICHI JIJINI DAR ES SALAAM




Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na baadhi ya wananchi waliokuja kupata huduma Makao Makuu ya Idaya ya Uhamiaji wakati wa ziara yake ya siku moja aliyoifanya leo Kurasini jijini Dar es Salaam.






Waziri Mwigulu akiwasili kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba za makamishna wa Uhamiaji zinazojengwa Kijichi jijini Dar es Salaam kuzikagua. 










Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Abbas Rovya (kushoto), akimpigia saluti Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) kabla ya kukagua nyumba hizo za kisasa. Kulia ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI), Shaban Hamza.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia), akiangalia nyaraka mbalimbali zinazochapishwa katika kiwanda cha kuchapa nyaraka za Uhamiaji alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kijichi jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji (ASP), Singwa Mokiwa na Kaimu Kamishna Generali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Mwigulu mbali ya kutembelea kiwanda hicho na mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa za makamishna wa Uhamiaji pia alizungumza na wafanyakazi wa Uhamiaji makao makuu Kurasini. 



Waziri Mwigulu akipata maelezo zaidi ya uchapishaji kwenye kiwanda hicho.



Kaimu Kamishna Generali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli (kushoto), akimuelekeza jambo Waziri Mwigulu.



Waziri Mwigulu akiangalia nyaraka mbalimbali kwenye 


kiwanda hicho.


Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Lusungu Ngairo (katikati), akimueleza jambo Waziri Mwigulu wakati wa ziara hiyo.




Na Dotto Mwaibale


SERIKALI imesema itaboresha mitambo ya kuchapisha nyaraka ya Uhamiaji ili kupata nyaraka zenye ubora wa kisasa.


Hayo yamebainishwa Dar es Salaam leo mchana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba wakati alipotembelea Kiwanda cha kuchapisha Nyaraka cha Uhamiaji kilichopo Kijichi Temeke jijini Dar es Salaam.


"Napenda kuwapongeza wenzetu wa Uhamiaji kwa kuwa na kiwanda cha kuchapisha nyaraka zao sisi kama serikali tutaongeza nguvu ndani ya taasisi hii ili kupata nyaraka bora zaidi " alisema Nchemba.


Mwigulu alisema nyaraka nyeti za serikali ni vizuri zichapwe na taasisi husika kama wanavyofanya uhamiaji jambo litakalosaidia kutozagaa hovyo mitaani.

Waziri Mwigulu aliongeza kuwa hivi sasa mpango wa serikali ni kutengeneza bidhaa zake kupitia taasisi zake kama ilivyo kwa viatu ambapo wameelekeza vitengenezwe na Magereza na kutumiwa na vyombo vyote vya ulinzi na usalama.

Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk.John Magufuli la kuzipa uwezo taasisi za serikali hasa majeshi kujiimarisha kwa kufanya kazi za viwanda zenyewe kama za utengenezaji wa madawati, uchapishaji wa nyaraka kama wanavyofanya Uhamiaji na nyingine nyingi.







SERIKALI KUJENGA VITUO VITATU KWA KILA HALMASHAURI KWA AJILI YA UCHUNGUZI WA SARATANI YA MATITI NA MLANGO WA KIZAZI



Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akizungumza kwenye Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza hii leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Bure ya Uchunguzi na Matibabu ya Saratani ya Matiti na Shingo ya Kizazi mkoani Mwanza.




Amesema serikali itaendelea kuboresha huduma za saratani ikiwemo kupatikana katika hospitali za rufaa Bugando Jijini Mwanza na KCMC Kilimanjaro ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Ocean Road Jijini Dar es salaam.


Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu, amesema watanzania wengi wanakabiliwa na magonjwa ya saratani na kuwahimiza kuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara.


Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza kwenye ufunguzi huo


Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonald Subi, akizungumza kwenye uzinduzi huo, ambapo amesema uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi uliofanyika katika halmashauri za Buchosa, Ukerewe na Kwimba umewafikia wanawake 1294 na kati yao, 58 wana dalili za awali za saratani ya matiti, 13 saratani ya kizazi na kwamba 15 wamepewa rufaa ya uchunguzi zaidi hospitali ya rufaa Bugando.


Rais wa Chama cha Madaktari Wanawake nchini MEWATA, Dkt.Sarafina Mkuwa, amesema lengo la kampeni hiyo ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi ni kuhamasisha wananchi kupata huduma hizo mapema kwani magonjwa hayo hutibika ikiwa mgonjwa ataanza matibabu mapema.


Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (kushoto), akisalimiana na Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Angelina Mabula (kulia) ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ilemela mkoani Mwanza.


Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na diwani wa Kata ya Kirumba, Alex Ngussa, wakati akiwasili kwenye uwanja wa Furahisha


Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akilakiwa kwenye uwanja wa Furahisha


Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (kushoto), akisalimiana na Grace Shindika ambaye ni Katibu wa UWT Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.


Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akilakiwa kwenye uwanja wa Furahisha


Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na mwakilishi kutoka Marie Stops Tanzania, wakati akiwasili kwenye uwanja wa Furahisha


Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akilakiwa kwenye uwanja wa Furahisha


Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akilakiwa na wawakilishi kutoka Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania MEWATA, wakati akiwasili kwenye uwanja wa Furahisha


Mwakilishi kutoka MEWATA akitoa maelekezo kwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (kulia), wakati akikagua mabanda ya huduma kwenye Uwanja wa Furahisha


Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akiteta jambo na Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu 


Kutoka kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu pamoja na Rais wa MEWATA, Dkt.Sarafina Mkuwa.


Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga (kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ilemela (kulia), wakiwa kwenye uzinduzi huo.


Meza kuu, aliyesimama ni mbunge wa jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula, akisalimia


Mmoja wa akina mama akielezea kufurahishwa kwake na huduma za bure za uchunguzi wa saratani ya matiti na shingo ya kizazi


Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza wamesema hawamudu gharama za uchunguzi wa saratani ya matiti na shingo ya kizazi hivyo kampeni hiyo ya bure itawasaidia na wanaomba iwe inafanyika mara kwa mara


Wanafunzi nao wamenufaika na uchunguzi huo ambapo wamesema ni jambo jema kwani wanatambua afya zao mapema na wameshauri watanzania kuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara


Wamesema bado upimaji na matibabu ya saratani nchini ni ghari hivyo wengi wao hawamudu gharama zake ambapo wameomba kampeni hiyo iwe endelevu.


Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza wakiwa kwenye foleni kupata huduma ya uchunguzi wa saratani ya matiti na shingo ya kizazi bure


Mamia ya wanawake Jijini Mwanza waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti na shingo ya kizazi bure.



Na George Binagi-GB Pazzo


Serikali inatarajia kujenga vituo vitatu kwa kila halmashauri nchini ili kuboresha huduma za uchunguzi na matibabu ya mapema ya saratani ya matiti na mlango wa kizazi kwa akinamama kwa lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa hayo.


Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, amebainisha hayo Jijini Mwanza wakati akizindua kampeni ya bure ya upimaji wa awali na matibabu wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto imetenga shilingi bilioni saba kwa ajili ya ununuzi wa dawa za magonjwa hayo huku benki ya dunia ikiwa imetoa shilingi bilioni tano kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa huduma hizo katika ngazi za halmashauri nchini.

Ameongeza kwamba serikali itaendelea kuboresha huduma za saratani ikiwemo kupatikana katika hospitali za rufaa Bugando Jijini Mwanza na KCMC Kilimanjaro ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Ocean Road Jijini Dar es salaam pamoja na vifo kwa akina mama ambavyo ni zaidi ya asilimia 60 nchini.

Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu, amesema watanzania wengi wanakabiliwa na magonjwa ya saratani na kuwahimiza kuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara.

Baadhi ya wananchi mkoani Mwanza wamesema bado upimaji na matibabu ya saratani nchini ni ghari hivyo wengi wao hawamudu gharama zake ambapo wameomba kampeni hiyo iwe endelevu.

Rais wa Chama cha Madaktari Wanawake nchini MEWATA, Dkt.Sarafina Mkuwa, amesema lengo la kampeni hiyo ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi ni kuhamasisha wananchi kupata huduma hizo mapema kwani magonjwa hayo hutibika ikiwa mgonjwa ataanza matibabu mapema.


WANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI WAANZA MITAHANI YAO LEO



NA KAROLI VINSENT
Jumla ya wanafunzi 435,221wa kidato cha pili nchi nzima leo wametarajia kuanza mitihani yao ya taifa ya kidato cha pili.
Ambapo kati yao wavulana ni 214,013 sawa na asilimia 49.17 na wasichana 221,208 sawa na asilimia 50.83.
Mbali na hao wapo wanafunzi wenye mahitaji maalum ambao watahiniwa wasioona ni 67 na watahiniwa wenye uoni hafifu ni 306 ambao watapewa maandishi ya karatasi hukuzwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Katibu mkuu wa Baraza la Mitihani nchini,Dkt Charles Msonde amesema mtihani huo ambao umeanza mapema hii leo ambao unatarajia kumalizika Nombemba 25 ya mwaka huu.

Amesema mtihani huo unalengo la kuwapima uwezo na uelewa kwa wanafunzi katika yote wajifunzayo kwa miaka miwili ya masomo yao huku wanafunzi wanaofeli wanakosa nafasi ya kuendelea na kidato cha tatu.

Dkt Msonde amesema maandalizi yote ya mtihani huo yamekamilika ikiwemo kusambazwa kwa mitihani itakayotumika katika upimaji huo pamoja na nyaraka muhimu katika mikoa na halmashauri zote ndani ya Tanzania bara.
Hata hivyo,Dkt msonde amesema Jumla ya wanafunzi 10,045,99 wanatarajia kuanza mitihani ya darasa la nne mwaka huu siku ya tarehe 23 na 24 Novemba ambapo kati yao wavulana ni 507,732 sawa na asilimia 48.54 na wasichana na 538,267 sawa na asilimia 51.46.
Pamoja na hayo dkt msonde amewataka wanafunzi pamoja na wasimizi kutohusika na vitendo vya udanganyifu huku akisema hatua kali za kisheria kwa waliohusika
Pamoja na hayo Dk Msonde amefafanua kuwa mafunzo ya ualimu wa shule ya msingi ngazi ya stashahada yamefutwa lakini wanafunzi waliopo vyuoni watamalizia masomo yao kwa muda uliobaki.

Dk Msonde amesema mafunzo hayo ya walimu yataendelea kwa utaratibu wa zamani ambao ulikuwa ngazi ya cheti.

Amesema usimamizi wa mitihani hiyo itakuwa chini ya Necta kama ilivyokuwa zamani badala ya Nacte.

"Wanafunzi walio vyuoni wataendelea na mafunzo hayo, isipokuwa kuanzia mwaka huu hatutadahili kwa ngazi ya diploma, tutadahili ngazi ya cheti kama ilivyokuwa zamani," amesema Dk Msonde.

WAIDAIWA SUGU WA BODI YA MIKOPO WAPEWA SIKU 90,SOMA HAPO KUJUA



Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo Abdul-Razaq Badru amesema kuwa hadi sasa kuna jumla ya wadaiwa sugu 142,470 wenye mikopo ya shilingi 239,353,750,170.27 iliyokwishaiva hawajajitokeza wala kuanza kulipa mikopo yao.


Akitolea ufafanuzi wa maana ya neo "Wadaiwa Sugu", Badru amesema kuwa ni wanufaika waliokopeshwa, muda wa matarajio ukapita bila kuwasilisha taarifa zao na kulipa madeni ya mikopo waliyokopeshwa tangu mwaka wa masomo 1994/1995.



Kuhusu hatua zinazochukuliwa na bodi hiyo, Badru amesema mbali na kutoa siku 30, bodi hiyo inakamilisha taratibu za kuwafikisha mahakamani kwa kuvunja sheria ya bodi ya mikopo kifungu cha 19A(1).


Hatua nyingine ni pamoja na kuyawasilisha majina hayo katika taasisi za mikopo, kuwasiliana na wadhamini wao pamoja na kuyatangaza hadharani majina ya wadaiwa sugu wote ili waajiri, wadhamini na wadau wengine wayajue na kutoa taarifa katika bodi hiyo.


Kuhusu takwimu za mikopo iliyotolewa, amesema tangu 1994/95 hadi 2015/16 jumla ya shilingi 2,595,932,575.56 zimekopeshwa kwa jumla ya wanufaika 379,179.


Amesema kati ya mikopo yote iliyokopeshwa, mikopo iliyoiva ni shilingi 1,425,708,285,046.48 kwa wanufaika 238,430 ambao tayari wamemaliza kipindi chao cha matazamio.


Badru amesema kuwa jumla ya wanufaika wa mikopo 93,500 wamebainika na kupelekewa ankara za madeni yao, ambapo kati yao wanufaika 81,055 wanaendelea kulipa.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...