Monday, 18 July 2011

MHANDISI AKESHA ENEO LA MRADI WA MAJI

MHANDISI  WA MAJI LUDEWA ASHANGAZA KWA KUACHA FAMILIA NA KUKESHA ENEO LA MRADI KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA MAJI SALAMA NA KWA WAKATI.
          
WANANCHI katika Kata za Manda, Luilo na Masasi katika Tarafa ya Masasi Ludewa, mkoani Iringa wameiomba serikali kuongeza nguvu zaidi katika mradi wa maji uliokuwa umeshindikana muda mrefu ama kwa kukosa rasilimali wataalamu wenye uwezo au fedha ili kuweza kufikisha maji katika maeneo yaliyobaki baada ya Bw. Christopher Nyandiga (Mhandisi wa Maji wilayani humo) kufauru kufikisha maji katika baadhi ya maeneo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau, wananchi na watumiaji wa maji hayo hawakusita kumshukuru na kumpongeza mhandisi wa maji wilayani humo Bw. Christopher Nyandiga na kumtaja kama mkombozi wa maisha yao kwa kuwa ni miaka mingi maji ya bomba yamekuwa ndoto kwao kutokana na ukilitimba wa wataalam na wahandisi waliotangulia.
“Mradi wa maji katika Tarafa yetu ya Masasi una historia ya ajabu kuna wakati katika miaka ya themanini, Rais wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassani Mwinyi aliitwa kuja kuzindua tanki la maji kumdanganya kuwa maji hayo yametokana na bomba kumbe waliyachota ziwa nyasa na kuyajaza na baada ya kuzindua tu ukawa ndiyo mwisho,” alisema mmoja kwa masharti ya kutoandikwa jina gazetini.
Alisema wananchi wana kila sababu ya kuishukuru Halmashauri ya Wilaya kwa kusikia kilio chao, lakini pia kwa kuwapelekea mhandisi mbunifu, mwenye uwezo kitaaluma, lakini mwenye kujituma kwani hawajawahi kuona mtaalam kuacha familia yake na kuhamia katika eneo la mradi huku yeye mwenyewe akifanya kazi kama fundi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw. Matei Felician Kongo akizungumza katika eneo la mradi alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri Bi. Hilda Lauo kwa uwamuzi alioufanya hasa Mhandisi wa Maji Wilaya ya Ludewa Bw. Christopher Ndindiga kwa kuvua cheo chake na kuhamia eneo la mradi hadi ulipokamilika.
“Mradi huu si wa leo ni wa muda mrefu sasa ni zaidi ya miaka ishirini,  awali ulikuwa ukiitwa Lifua- Manda Project wakati huo kulikuwa na ugonjwa wa kipindupindu huku ukilenga kupeleka maji hayo katika Sekondari ya Manda,” alisema Bw. Kongo huku akifurahia mafanikio.
Bw. Kongo alisema katika miaka ya 1979 hadi 1980 mradi huo ulikuwa unategemea chanzo cha mto Kilumbila ambao sasa unaendeshwa na wamisionari, hata hivyo hakuwa na uhakika kama ni shilingi ngapi zilitumika katika miradi hiyo kwani ni muda mrefu sasa.
Mradi huu mpya chanzo chake ni mto Mchuchuma ambao unayomaji ya kutosha na unahudumia kwa sasa katika vijiji vya Luilo, Lihagule, Manda na Masasi, hata hivyo mradi wenyewe umekuwa wa kuungaunga hii ni kutokana na fedha kutofika kwa wakati na wakati mwingine kuwa kidogo.
Bi. Winfrida Kilumbo (Kizota) Diwani wa Kata ya Manda kwa upande wake alimshukuru na kumpongeza Mhandisi wa Maji, Bw. Christopher Nyandiga kwa moyo wa kizalendo kwani aligeuka kuwa fundi yeye mwenyewe na kuuweka uhandisi pembeni.
Kizota alisema Wananchi wa Manda wamekuwa wakitumia maji ya Ziwa Nyasa ambayo kwa kipindi cha masika si salama. Lakini mradi huu ni ukombozi mkubwa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Manda na walimu kwani wamekuwa wakitegemea maji ya ziwa yanayopatikana umbali wa zaidi ya kilomita tano.
“Wanafunzi wamekuwa wakibeba maji kichwani kwa matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na walimu wao kila siku wanapokwenda shuleni kwa kipindi chote cha miaka mine, lakini tunashukuru sasa tatizo hili limekwisha baada ya maji kufika shuleni hata ujenzi wa majengo umerahisishwa,” alisema Bi. Kizota.
Kwa upande wake, mhandisi wa maji wilayani Ludewa Bw. Nyandiga alisema alilazimika kufanya hivyo kutokana na shida wanayoipata wananchi wa Tarafa ya Masasi kwa muda mrefu sasa na kwamba amefanikiwa kuyafikisha maji katika baadhi ya maeneo machache na kwamba sehemu zingine zitaendelea kupata kadri ya upatikanaji wa fedha, lakini akawataka wananchi kutunza na kuyalinda mabomba hayo ili yaweze kuwatunza.

VIBALI VYA MADINI LUDEWA

LUDEWA

WANANCHI Wilayan ya Ludewa mkoani Iringa wako hatarini kugeuka wakimbizi katika siku za usoni kutokana na hofu ya maeneo yao kugawiwa kinyemela na ofisi za madini kanda zilizoko mkoani Mbeya imefahamika.
Hofu na mashaka vilitanda hivi karibuni kwa madiwani wote walipotembelea katika Kata ya Iwela ambako kulikuwa na wasiwasi miongoni mwa wananchi waishio katika maeneo hayokuwa baadhi ya wachimbaji wageni wenye mitambo wasio na vibali wameingia na kuvamia kwa kuanza shughuli za uchimbaji bila wananchi kujulishwa.
Katika Baraza la Madiwani (Full Council) madiwani katika halmashauri hiyo waliitaka Wizara ya Nishati na Madini kutumia busara na uungwana kuhusu suala la ugawaji maeneo kwa sababu pamoja na kuwepo Sheria za Madini,  lakini wananchi nao wanayo haki ya kusikilizwa na kuhusishwa ili kuepusha migongano ya baadaye.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw. Matei Felician Kongo akizungumza katika baraza hilo alioneshwa kusikitishwa kwake kusikia kila eneo ndani ya wilaya  limetolewa kibali bila wananchi kujulishwa kwa kufanya hivyo usalama wa wanaLudewa huko wapi kama eneo lote limejaa vibali? Aliuliza Bw.  Kongo huku akimwagiza mkurugenzi kufuatilia.
Kwa upande wake Bi. Hilda Lauwo ambayo ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ludewa alisema ni hatari sana kama wananchi hawaelewi kama maeneo yao ya makazi yamegawiwa kinyemela na kwamba watakapokuja kujua na kutakiwa kuondoka itatuletea matatizo na hasara kubwa kwa sababu uzoefu umeonekana katika maeneo ya wenzetu.
Bi.  Lauwo alisema tumeona matukio mengi ya mauaji huko kwenye maeneo ya madini na kuongeza kuwa kuna haja ya kufuatilia jambo hili kwa wahusika ili kujua mstakabali wa wilaya, hatutaki yaje yatukute na sisi baadaye.
“Kama hatutapata ufumbuzi wa hili tatizo mapema tutakuja kupata shida kubwa baadaye, hivyo ni vema kamishna wa madini kanda aje atueleze na wananchi waelewe mapema kabisa kabla haya mambo hayajakuwa magumu,”alisisitiza Bi. Lauwo.
Aliongeza kuwa bila kufanya hivyo hii Wilaya ya Ludewa itakuja kuwa na matatizo kuliko wilaya zingine kwa hiyo ni vizuri wananchi wakaambiwa na kujulishwa maeneo yote yaliyokwisha kugawiwa na pengine kamishna aeleze ni vigezo gani alitumia kugawa maeneo yote ya Wilaya hii bila taarifa na inasemekana hadi sasa kuna vibali 70 vimeshatolewa.

LUDEWA WAGOMA KUWAPOKEA WATANZANIA WAPYA

WANANCHI katika Wilaya ya Ludewa Mkoani Iringa, wamekataa katu kuwapokea wakimbizi kutoka Somalia na Ethiopia waliobatizwa kwa jina la watanzania wapya kwa madai kuwa watasababisha hasara kubwa kuliko faida imefahamika.

Mgomo huo umetokea jana katika kikao cha Baraza  la Madiwani ambao ni wawakilishi wa wananchi kilichofanyika Julai 15 mwaka huu ambacho pamoja na mambo mengine kilihusisha bajeti ya mwaka ujao wa fedha na kuangalia hali halisi ya utekelezaji wa miradi  ya maendeleo kwa mwaka wa fedha uliopita.

Awali akitoa taarifa ya kutaka ufafanuzi Diwani wa Kata ya Mawengi, Bw. Leodgar Mpambalyoto alisema kuna jambo lililoko mbele yetu linalowasumbua wananchi wengi ambalo ni agizo la serikali la kuwapokea watanzania wapya ambao wamebatizwa jina hilo kutokana na kuingia nchini na kupokelewa kama wakimbizi.

Kwa upande, wake Mpambalyoto aliishauri serikali kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi na baadhi ya wadau wakiwemo madiwani. “Ni wajibu wa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri kupokea maelekezo kutoka Serikali Kuu, lakini baraza lina uwezo wa kukataa au kukubali kwani ndiyo wawakilishi wa wananchi,” zoezi la kuwapokea watanzania wapya bila maelekezo litakuwa na athari kubwa sana tunaomba lisipuuzwe,” aliongeza.

Akichangia hoja hiyo Mbunge wa Ludewa Bw. Deogratius Haule Filikunjombe alisema kuwa waraka huu ulishasainiwa na rais tayari na ulishapitishwa, lakini ukiangalia zaidi watu hawa wakija wanamadhara zaidi kuliko faida.

“Pamoja na kwamba rais ameridhia mila za watu hawa na zetu hazifanani, wanakotoka ni watu wa vita, leo hii Ludewa tunaletewa watu elfu tatu je, wana Ludewa wameandaliwa?  Sisi tupo tayari?  Kama sehemu nyingine wanawahitaji, sisi Ludewa hatuwataki,”alisisitiza mbunge huyo.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ludewa Bi. Hilda Lauwo aliwaambia madiwani hao kuwa anataarifa kuwa wahusika walisema wangekuja kutoa mafunzo hayo ili kupata uelewa aliwataka wasikatae mafunzo hayo na kwamba wayapate kwanza ndipo wayakatae.

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria baraza hilo walishtushwa na hatua ya serikali kuleta wageni nyumbani kwao bila kuwashirikisha na kukubaliana, walisema pamoja na kwamba waraka huu umetoka kwa mkuu wa nchi ambaye ni Rais Jakaya Kikwete, siyo vizuri kuwaleta watu hawa wanaotoka kwenye vita katika maeneo yetu hatuwezi kujua wamekuja na nini.

“Sisi wenyewe hatuna sehemu ya kulima tunahangaika kwa umaskini sasa hawa watanzania wapya wanaotaka kuja katika miji yetu, kwani huko kwao walikotoka hawawezi kurudishwa?” waliuliza wajumbe hao kwa maskitiko.

 Taarifa hiyo ya utengamanishaji wa mkakati wa kufungua makazi mapya na kuwezesha ukaaji wa watanzania wapya waliopewa uraia katika maeneo tofauti nchini,  inasema serikali ya Tanzania kuwezesha uhamiaji wa makazi ya kaya za Watanzania wapya waliopewa uraia zipatazo 35,500 kutoka katika makazi ya wakimbizi.

Katika zoezi hilo serikali imeteua wilaya zaidi ya 50 kutoka mikoa 16 ambayo ni pamoja na Iringa kaya
3,000, Rukwa 3,000, Dodoma 3,500, Ruvuma 3,000, Shinyanga 1,600, Morogoro 1,600, Tabora 1,600, Tanga 1,600, Kigoma 1,000, Singida 1,600, Pwani 2,000, Mtwara 3,500, Mbeya 1,500, Manyara 1,500, Lindi 3,500, na Kagera 1,500 vigezo vilivyotumika katika uteuzi wa mikoa hiyo ni upatikanaji wa ardhi ya kulima na hali ya msongamano wa watu.

Wilaya ya Ludewa inazo tarafa tano, kata ishirini na tano na vijiji sabini na sita wakazi wake wako laki moja na nusu kwa mujibu wa Sense ya Mwaka 2000. Ludewa inavivutio vingi ikiwemo milima ya Livingstone, samaki wa mapambo Ziwa Nyasa, madini aina nyingi tofauti.
                  
WANANCHI LUDEWA WAPIGANA VIKUMBO NA MIFUGO KISA MAJI

Na Friday Simbaya, Ludewa

WANANCHI wa Ludewa Mjini Makao Makuu ya Wilaya ya Ludewa mkoani Iringa wamesema kuwa hawaoni umuhimu wa kuwa na mamlaka ya maji mjini yaani ‘Ludewa Water Supply and Sanitation Authority (LUDSSA) kwa sababu tatizo la maji kwao linazidikuongeka kila kukicha huku mabomba yakitiririsha maji mitaani ovyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao walisema Serikali ya Wilaya ya Ludewa haioni haja ya kusumbua vichwa kwa ajili ya kuondoa kero ya maji kwa sababu katika nyumba zao maji yamejaa mpaka wanashindwa kwa kuyapeleka kwani mwenye shibe hamjali mwenye njaa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Ludewa mjini, Bw Omary John Kiowi alisema kuwa wananchi wanayo haki ya kulalamika kwani kero hii ni aibu kwa wataalam wetu ambao miaka nenda rudi wanatoa sababu kuwa maji hayatoshi kwenye matanki huku waamebweteka bila kutafuta njia mbadala kuikabili hali hiyo.

Bw Benito Mgimba makazi wa Mtaa wa Kanisa B aliliambia Nipashe kuwa sasa ni miaka zaidi ya kumi maji katika mtaa wao ni ndoto hivi hata watoto wanaozaliwa wakiyaona mabomba katika mitaa mingine wanashangaa na kuogopa kwa sababu ni vitu vigeni kwao.

“Miaka miwili iliyopita tuliambiwa tuchimbe mitaro kwa nguvu zetu wenyewe ili tuletewe maji mtaani kwetu, lakini hadi leo hakuna kinachoendelea mitaro tumechimba bure na maji hayaletwi na hakuna taarifa yoyote, sisi hatuna kwa kwenda kulalamikia wanyonge,”alilalamika Benito.

Oscar Chaula na Romward Kiowi kwa upande wao walisema watendaji katika idara husika wameshindwa kuwajibika. “Katika mtaa wetu wa kanisa tuliweka bomba la kwanza wakasema ni dogo tukachanga fedha na kununua lingine kubwa, ni mwaka wa ishirini sasa tunakunywa maji yanayotumiwa na wanyama kama nguruwe, ng’ombe na punda kwenye madimbwi,” alisema Chaula.

Romwardi Kiowi alilalamika kuwa ni miaka mitatu tangu wachimbe mifereji kwa nia ya kutandaza mabomba, lakini hakuna kinachoendelea na kwaamba ni zaidi ya miaka zaidi ya mitano hajaona maji ya bomba,  ila anashuhudia watoto wakiugua magonjwa ya matumbo kwa kunywa maji yasiyo salama kutoka kwenye madimbwi huku watendaji wakisubiri mishahara na kunywa pombe tangu asubuhi.

Cathbert Haule mkazi wa Mtaa wa Kanisa, Castory Mwachiro wa Mtaa wa Kanisa B, Tiemo Kayanda, Stephano Mahundi mkazi wa Mtaa wa Mkondachi, Valentina Mgeni, Lucy Haule wameilaumu serikali ya wilaya kwa kutoshughulikia kero ya maji ambayo ni muhimu sana kwa matumizi ya binadamu.

“Inashangaza na haiingii akilini wanaposema maji hayatoshi wakati mitaani maji yanamwagika ovyo, hakuna usimamizi wala uwajibikaji, mkurugenzi na watendaji wake tunataka huduma ya maji inawezekana vyanzo havitoshi, lakini tuyadhibiti haya yaliyopo watendaji acheni kushinda maofisini.””alilalamika Bw. Haule.

Akijibu malalamiko hayo Meneja wa Mamlaka ya maji mjini Ludewa (LUDWSSA), Bw. Atanasio Munge alikiri kuwapo kwa tatizo la maji katika baadhi ya maeneo ya mji wa Ludewa kama mtaa wa Kanisa B, miundombinu yaani mabomba yamechakaa, lakini pia bomba linalotoa maji kwenye Tanki na kuleta mjini ni dogo sana lina ukubwa wa 3 inch tu, wakati linachukua maji katika matanki mawili.

Bw. Munge alisema kutokana na tatizo hilo watu wanaopata maji tena ya mgao ni 65% ya wakazi wote wa Ludewa na kwamba hao wanalazimika kupata mara tatu kwa wiki na kuongeza kuwa mbali na uchakavu wa mabomba ongezeko la watu ni kubwa sana linafanya maji kuwa machache.

Hata hivyo, alitoa matumaini kwa wakazi wa Ludewa kwamba mamlaka ya maji ina mipango kabambe ya muda mfupi na mrefu katika kukabiliana na kero ya maji mjini kwa kupima na kusanifu chanzo cha maji cha Mapetu pamoja na kile cha Mwangacha ili kuhakikisha mitaa ya kanisa na kwingineko maji yanapatikana kwa uhakika.

Munge aliutaja mpango wa muda mrefu kuwa ni Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji Maalum kwa Kata ya Ludewa mradi ambao utasimamiwa na mamlaka ya maji Ludewa (DED) na Msimamizi wa maji kutoka Mamlaka ya Maji Iringa Manispaa (IRUWASA) na tayari mzabuni Don Consultant ameshaanza kwa hatua ya kwanza ya vitabu vya zabuni na kwamba matanki mawili yenye ujazo wa m.300 yatajengwa Ludewa (K) na tanki moja lenye ujazo wa m.1000 litajengwa Ludewa (M) eneo la Kilimahewa.
                             
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...