Thursday, 17 May 2018

WALIMU MANISPAA YA IRINGA WAMCHARUKIA MKURUGENZI KUHUSU MADENI YAO


WALIMU wa Manispaa ya Iringa wameomba Mkurugenzi wa Halmashauriya Manispaa ya Iringa kuwalipa madeni walimu wote fedha zao za uhamisho wanazodai, ambaz.o wanadai kwa muda mrefu. 

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Katibu wa Chama cha Walimu (CWT) manispaa hiyo, Fotunatafatuma Njalale, alisema pamoja na serikali kusema kuwa haitaki kuzalisha madeni mapya ya walimu, bado kumekuwa na uhamisho wa walimu kwenda kwenye vituo vipya bila kulipwa fedha za uhamisho. 

Njalale alisema kuwa wapo walimu waliohamishiwa nje ya Walaya ya Iringa na walikwenda kuripoti kwa nauli zao na baadaye kurudi kudai posho za usumbufu nauli na usafiri wa mizigo yao, 

Alisema kuwa walimu hao wa Manispaa wanadai pesa ya usumbufu kutoka eneo moja kwenda nyingine, wakati wale walimu wa vijijini wanatakiwa kulipwa pesa ya usumbufu na kujikimu. 

Alisema madai hayo ni ya muda mrefu lakini hawajalipwa hata senti huku wakilazimishwa kwenda kwenye vituo vipya vya kazi kwa vitisho na kuonekana ni watoro. 

Njalale alisema kuwa kumekuwepo na taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya habari kwamba walimu wa manispaa ya iringa wameanza kulipwa madeni yao uhamisho kitu ambacho kimeleta taharuki kwa walimu. 

Alisema kuwa baada yakupata taarifa hiyo baadhi ya walimu wamekuwa wampigia simu kutaka ufafanuzi kuhusu walimu walianza kulipwa madeni yao. 

Alisema kuwa anao walimu baadhi yao walidaiwa kulipwa madeni yao uhamisho lakini wamekiri kwamba hawajaona kitu chochote kwenye akaunti zao. 

Aidha, Nipashe iliongea na baadhi ya walimu ambao hawakutaka majina yao yatajwe gazetini walisema kuwa mkurugenziwa halmashauri amekuwa kuwapa ahadi zisizotekelezeka. 

Walisema kuwa tangu wabadilishiwe vituo vyao vya kazi hawajalipwa hata centi tano licha mkuruguzi kuwaahidi kuwalipa pesa zao za usumbufu pamoja na zakujikimu. 

Kwa upande wake, kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Omari Mkangama alsiema kuwa ,Halmashauri ya Manispaa ya Iringa inendelea kuwalipa madeni watumishi hao waliohamishwa vituo vyao vya kazi. 

Akizungumza na wanahabari jana Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa huyo alisema kuwa wapo baadhi ya walimu waliohamishwa katika shule za msingi na sekondari ambao walihamishwa na tayari wameanza kulipwa stahiki zao. 

Mkangama alisema kuwa katika walimu ambao walihamishwa toka Sekondari kwenda shule za msingi kati ya hao Halmashauri imewalipa asilimia 65 ya madai yao ambayo ni zaidi ya milioni 69 zimelipwa. 

Alisema kuwa halmashauri yake inaendelea kuwalipa watumishi wote wastaafu pamoja na walimu wa shule za msingi na sekondari waliohamishwa na tunaendelea kufanya mchakato wa malipo na wote watalipwa. 

Hata hivyo, alisema kuwa walimu hao walihamishwa kutokana na mrundikano wa walimu (over staffing) katika kituo kimoja, kwa mfano kituo kimoja kina walimu sita wote wanafundisha somo moja. 

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...