WAKATI Taifa linadhimisha miaka 50 ya Uhuru wananchi katika Kata za Mundundi na Mkomang’ombe ya Wilaya Ludewa, Mkoa wa Iringa ni zaidi ya miaka miwili sasa wamekaa tu bila kufanya shughuli za maendeleo kutokana na maeneo wanayoishi kuwa ndani ya migodi ya madini ya chuma na makaa ya mawe.
Aidha katika hali nyingine maeneo mengi ndani ya Wilaya ya Ludewa yanamilikiwa na watu wasiojulikana kwa kupewa vibali na ofisi ya madini kanda ya mbeya huku wenyeji wakibaki midomo wazi wasijue la kufanya.
Hayo yalibainishwa hivi karibuni na madiwani wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa walipofanya ziara ya kushtukiza katika Kata ya Iwela na kuwakuta wachimbaji waliodhaniwa kuwa ni wavamizi wakiwa na vibali kamili na ndipo walipofumbuka macho baada ya kuona ramani inayoonesha vibali zaidi ya 70 vilivyotolewa na kamishna wa madini kanda ya mbeya.
Ni kutokana na hali hiyo, madiwani katika Baraza kuu walimtaka kamishna wa madini kanda ya Mbeya kufika haraka Ludewa kwa ajili ya kutoa ufafanuzi juu ya ni vigezo gani alitumia kutoa vibali hivyo katika makazi ya watu bila kuwataarifu wenyewe.
Madiwani hao walionya kuwa kama hali itabaki kama ilivyo ni wazi siku za mbeleni Ludewa itakujakuwa na migogoro mikubwa kuliko sehemu yoyote ile nchini kutokana na wananchi hao kuonesha subira, utii na uvumilivu juu ya madini hayo tangu walipoambiwa na Rais wa Awamu ya kwanza Hayati Baba Mwalimu Julius Nyerere kuwa wasubiri.
Akipunguza jazba kwa madiwni hao Afisa tawala Wilaya ya Ludewa Bw. John Mahali alisema ofisi ya Mkuu wa Wilaya imeshafanya mawasiliano na kamishna wa kanda Mbeya na kuahidi kuja Ludewa kuendesha elimu kwa wananchi juu ya haki yao.
Pamoja na kumwita Kamishna wa madini bado wananchi wamepigwa na butwaa na sasa wanasubiri hatma yao kwa kutega masikio kwa kamishna wa madini kanda, ili kujua nini mstakabali wa maisha yao katika suala zima la madini ma makazi.
Thursday, 28 July 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...