Sunday, 15 November 2015

JUHUDI BINAFSI ZINATAKIWA KUMALIZA UKEKETAJI, UNYANYASAJI KIJINSIA – ROSE HAJI MWALIMU



Afisa Maendeleo ya Jamii (W) Ngorongoro, Teresia Irafay (wa pili kushoto) akiitambulisha meza kuu kabla ya kumkaribisha Katibu Tawala wa Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kileo, (wa tatu kulia) kufungua kongamano la viongozi wa mila wa kabila la wamasai (Laigwanan/Ngaigwanani) na wanawake Mashuhuri yenye lengo la kushawishi uondoaji wa mila potofu zinazorudisha nyuma maendeleo katika jamii za wafugaji. Kushoto ni Mtaalamu wa masuala ya vyombo vya habari vya kijamii na Mkufunzi kutoka (UNESCO), Bi. Rose Haji Mwalimu, Kiongozi wa Malaiboni wilaya ya Ngorongoro Bw. Sangau Naimodu (wa pili kulia) pamoja na Katibu wa Baraza Mila (W) Ngorongoro, Laanoi Munge, (kulia), Mwenyekiti wa Baraza la Malaigwanan wilaya ya Ngorongoro, Joseph Oletiripai (wa tatu kushoto). (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Na Modewjiblog team

JAMII ya wafugaji imetakiwa kutumia juhudi zao binafsi kubadilisha mawazo na imani ya jamii kwamba mila na desturi hazibadiliki ili kutengeneza mfumo bora mpya unaothamini maisha ya wanawake.

Wito huo umetolewa na Mtaalamu wa masuala ya vyombo vya habari vya kijamii na Mkufunzi, Bi. Rose Haji Mwalimu wakati akiwasilisha mada kwenye kongamano la viongozi wa mila wa kabila la wamasai (Laigwanan/Ngaigwanan), Laiboni na wanawake Mashuhuri yenye lengo la kushawishi uondoaji wa mila potofu zinazorudisha nyuma maendeleo katika jamii za wafugaji.

Aliwataka washiriki wa warsha kusimama kidete na kutumia elimu waliyoipata katika kushawishi jamii kubadilika na kuachana na mila za ukekeketaji,ndoa za utotoni na pia unyanyasaji mwingine wa kijinsia unaoonesha ubabe wa wanaume na mfumo dume.

Aliwataka wanajamii hao kutumia njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari, rediojamii, vikao mbalimbali vya kata na vijiji pamoja na nyumba za ibada kuhimiza watu kubadilika na kuacha mila hizo za ukeketaji na kuozesha watoto katika umri mdogo.

Aidha Bi. Rose Haji Mwalimu katika kongamano hilo lililoandaliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, (UNESCO) amewataka wanawake kuvunja ukimya na kuacha uoga na kuibua vitu vinavyowanyima haki zao za msingi.


KatibuTawala wa Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kileo akifungua kongamano la viongozi wa mila (Laigwanan/Ngaigwanan na Laibon) pamoja wanawake mashuhuri lenye lengo la kuondoa mila potofu zinazokwamisha maendeleo katika jamii za wafugaji ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro.

Aliwataka wanawake kujitambua ili kutumia sheria zinazowalinda kuondokana na unyanyasaji pamoja na ukatili wa kijinsia unaoendelea katika jamii za kifugaji na kuwaomba viongozi wa mila washiriki katika kuondoa mfumo dume.

Naye Ofisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, Benezeth Bwikizo, amesema kama watuw atajitokeza na kueleza ukweli serikali itachukua hatua hasa ya kulinda wanawake na watoto kupitia mamlaka iliyokabidhiwa na Katiba ya nchi.

Alisema kwa mujibu wa sheria Serikali ina mamlaka ya kuhakikisha kwamba haki za watoto zinalindwa kupitia sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwamba mtoto lazima alindwe na apate haki zake zote za msingi.

Alisema pamoja na katika na sheria zilizotungwa, mtoto pia analindwa na mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto wa Novemba 20, 1989 inayotoa ufafanuzi wa kulinda na kuhakikisha kwamba haki za mtoto zinalindwa na kuheshimiwa.

Aliongeza kuwa pia ulindaji huo wa haki za mtoto unakwenda sanjari na mkataba wa Umoja wa nchi za Afrika ya mwaka 1990 unaotoa ufafanuzi juu ya haki za msingi za mtoto na namna inavyotakiwa kuheshimiwa na kulindwa bila kuathiri haki zao.


Ofisa Elimu ya Uzazi na UKIMWI kutoka UNESCO, Mathias Herman akizungumzia malengo ya kongamano hilo kwa washiriki.

Bw.Bwikizo, alitaja haki za muhimu kwa mtoto zinazotakiwa kulindwa na kuheshimiwa ili kuhakikisha mtoto anakua katika malezi bora ni huduma za afya, chanjo, matibabu, Lishe na malezi bora kupata haki ya kuishi, haki ya kuendelezwa na haki ya kulindwa.

Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano hilo, KatibuTawala wa Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kileo, amelishukuru Shirika la UNESCO kwa kuendesha mafunzo hayo ya kutoa elimu na kujenga uwezo kwa viongozi wa mila na wanawake mashuhuri ili kuondoa mila potofu katika jamii ikiwemo Ukeketaji, mimba za Utotoni na ndoa za umri mdogo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Bw. Kileo aliwataka viongozi na washiriki wa warsha hiyo watumie nafasi hiyo waliyoipata kwenda kufikisha ujumbe kwa jamii ili kupeleka maendeleo mbele kwa kupunguza vifo vya akinamama na wasichana wenye umri mdogo, kuondokana na ukeketaji pamoja na mimba za umri mdogo.


Mtaalamu wa masuala ya vyombo vya habari vya kijamii na Mkufunzi kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu akisisitiza jambo kwa washiriki wa kongamano.

Kwa upande wa mmoja wa wakufunzi wa warsha hiyo kutoka UNESCO akizungumzia malengo ya warsha hiyo, Ofisa Elimu ya Uzazi na Ukimwi wa shirika hilo, Mathias Herman, amesema warsha hiyo ni mwendelezo wa warsha zinazotolewa na UNESCO kwa ajili ya kutoa elimu ya kuwajengea uwezo na kugawa majukumu kwa viongozi wa kimila (Laigwanan), wa mama mashuhuri, viongozi wadini, wakunga wa jadi pamoja na waandishi wa habari kufanya ufuatiliaji wa afya ya uzazi na malezi bora kwa watoto.

Aliongeza kuwa UNESCO inatarajia mafunzo hayo kutaleta mabadiliko kupitia nafasi ya viongozi hao mashuhuri katika jamii kwa kuwa wanaaminika ili kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo wanaotoa mafunzo kuhakikisha kwamba suala la mimba za utotoni, ndoa za utotoni pamoja na ukeketaji linafika mwisho katika jamiii ya kifugaji.



Mwenyekiti wa Baraza la Malaigwanan wilaya ya Ngorongoro, Joseph Oletiripai akisisitiza jambo kwa Malaigwanan pamoja na wakina mama mashuhuri ambapo aliwataka watumie nafasi waliyopewa na jamii na fursa ya elimu waliyopata kutoka kwa wadau wa maendeleo UNESCO kuwa italeta mabadiliko na mpango chanya katika jamii ya Kimasai.


Ofisa Ustawi wa Jamii wa wilaya ya Ngorongoro, Benezeth Bwikizo (kuhoto) akizungumzia haki za watoto. Kulia ni Mkalimani wa lugha ya Kimasaai Mchungaji Mark Murenga.


Mama Mashuhuri kutoka kijiji cha Olopiri, Nolarir Pashuku, akitoa maoni yake kwenye kongamano.


Mmoja wa washiriki katika warsha hiyo ambaye ni Laigwanan , John Olekulinja kutoka kata ya Malambo akizungumzia mafunzo hayo.


Kiongozi wa Malaiboni wilaya ya Ngorongoro Bw. Sangau Naimodu (katikati) akieleza namna inavyofaa kueneza elimu ya mabadiliko.


Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto, tarafa ya Loliondo (W) Ngorongoro, Bi. Nailejileji Joseph akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa washiriki wa kongamano hilo.


Pichani juu na chini ni viongozi wa mila wa kabila la wamasai (Laigwanan/Ngaigwanan), Laiboni na wanawake Mashuhuri walioshiriki kwenye kongamano hilo yenye lengo la kushawishi uondoaji wa mila potofu zinazorudisha nyuma maendeleo katika jamii za wafugaji lilioandaliwa na Shirika la UNESCO.








TIGO YAUMWAGIA MILIONI 100 KUFANYIKISHA MTIKISIKO WA EBONY FM



Mkurugenzi wa Tigo wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusunudhamini wa tamasha la Mtikisiko ikiwa ni sehemu ya sera ya kampuni hiyo ya kusaidia makundi mbalimbali ya jamii wakiwemo vijana na wasanii. (Picha na Friday Simbaya)



Mwenyekiti wa waandaji wa tamasha la ‘mtikisiko’, kanda za nyanda za juu kusini,
Bon Zachariah ametoa wito jana kwa vijana waume kwa wake walio na vipaji vilivyojificha kujitokeza na kushiriki kwenye fursa hii ya nadra iliyoongia ukanda huu.

Alisema tamasha la mtikisiko linawataka vijana kujitokeza kushiriki tukio la mwezi mmoja ambalo linahusisha mikoa ya Iringa, Ruvuma, Njombe na Mbeya ambapo uzinduzi wake utakiwa mjini Songea.

“Tunatoa wito kwa vijana walio na vipaji vilivyojificha kujitokeza na kushiriki kwenye fursa hii ya nadra iliyongia kwenye ukanda huu. Inaweza kuwa ndio fursa yako ya kuwa nyota,”alisema Zachariah.

Alisema kuwa lengo kuu la tamasha ambalo ya la msimu kwa mwaka mara moja ni kurudisha fadhila kwa watu ambao walifanyakazi nao kwa mwaka mzima.

Zachariah alisema kuwa kuna makundi matatu ya watu ambao Ebony FM Entertainment wanarudisha fadhila hizo amabao ni wafanyabiashara na makampuni ambayo wamekuwa wakifanyakazi kama Tigo, wasikilizaji pamoja na wasanii ambao nyimbo zao zilikuwa zikitumika katika media mbalimbali.

Kupitia tamasha hilo mwenyekiti huyo alisema kuwa watatumia pia kusambaza ujumbe kwa vijana kuhusu maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa vile ukanda huu umeadhirika na ugonjwa huo

Alisema tamasha la mtikisiko lilianza mwaka 2007 ambapo wakati huo lilikuwa linaitwa ‘Together Time’ na kubadilisha jina lake mwaka 2008 na kuitwa ‘Mtikisiko’ mpaka sasa.

Tigo Tanzania kupitia huduma yake ya “Tigo Music” imedhamini tamasha la muziki liitwalo ‘Mtikisiko’ katika nyanda za juu kusini kama sehemu ya sera ya kampuni hiyo kusaidia makundi mbalimbali katika jamii wakiwemo vijana na wasanii kufikia ndoto zao za kimaisha.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Kuu Kusini, Jackson Gideon Kiswaga alisema kuwa kampuni yake imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono vijana katika nyanja mbalimabli ili kuwawezesha kufikia ndoto zao katika teknoljia, michezo, muziki, elimu na mengine mengi.

“Udhamini huo wa Tigo wa shilingi milioni mia moja (100m/-) utajumlisha kuwasafirisha wasanii, kuwalipa posho, kujenga majukwaa pamoja na kuwalipa waandaji,”alisema Kiswaga.

Aliongeza kuwa Kampuni ya Tigo imekuwa mstari wa mbele katika kunyanyua maisha ya vijana na jamii kwa ujumla. 

Alisema kuwa kupitia msaada kwa wasanii, wameweza kuchangia kuibua nyota maarufa wa muziki wanaofahamika kama Ally Kiba, Diamond, Vanessa Mdee na wengineo.

“Tunaamini kwamba tamasha la mtikisiko litaenda mbali katika kuibua vipaji vipya amabvyo vitakuwa nyota wa baadaye, wazuri kushinda hata hao niliwataja,” alisema Kiswaga.

Tigo imetoa udhamini huo ilikuhakikisha kuwa tamasha la mtikisiko linasukika kwenye ukanda wote wa nyanda za juu kusini kwa kuwa ni tukio la mwezi mmoja ambalo litahusisha mikoa ya Iringa, Ruvuma, Njombe na Mbeya.

Kuanzishwa kwa Muziki wa Tigo (Tigo Music) nchini Tanzania kumetokana na mafanikio ya uzinduzi wake nchini Ghana mwaka 2014 na Amerika ya Kusini mwaka 2012. 

######################################################

By Friday Simbaya, Iringa


THE Chairman of the organizers of the festival of downturn called ‘Mtikisiko’ in the southern highlands regions, Bon Zachariah has appealed yesterday to the young men and women who have lie in wait emerging talent and to participate in this rare opportunity coming in this zone.

He called upon youth to participate in the festival which comes every year once and it is a one month event that brings together regions of Iringa, Ruvuma, Njombe and Mbeya.

The launching done in Songea Ruvuma Region and the closing of the event will be in Njombe Region but last year it was done Iringa Town, Iringa Region.

"We call on the youth and talent lurked in emerging and participates in this rare opportunity that is entering into this zone. It could be your opportunity to be the star, "said Zachariah.

He said that during the event they will also distribute messages of HIV and AIDS to youth as the regions in the southern highland zone were heavily affected with the pandemic. 

He said that the main purpose of the festival that the season of a year once it is restoring a courtesy to people who have worked with them throughout the year.

Zachariah said that there are three groups of people who Ebony Entertainment are repeats these virtues who are corporate companies that have been working together with like Tigo, the listeners and artists, whose their songs have been used in various media.
He said the ‘Mtikisiko’ festival began in 2007 and at that time was called "Together Time" and changed its name in 2008 and called ‘Mtikisiko’ until now.

Tigo Tanzania through its service "Tigo Music" has sponsored the music festival called ‘Mtikisiko’ in the southern highlands as part of the company's policy to support various social groups, including young people and artists to achieve their dreams in life.

Speaking at the launch of the festival yesterday, Zonal Director-South, Jackson Gideon Kiswaga said that his company has been in the forefront to support young people in all walks of life to enable them to achieve their dreams in technology, sports, music, education and much more.

"Tigo's sponsorship of one hundred million shillings will include the transporting of artists, to pay allowances, to pay for building platforms and also w the organizers," said Kiswaga.

He added that Tigo has been at the forefront in uplifting the lives of young people and society in general.

He said that through the assistance of artists, they can contribute visually to music stars that became known as Ally Kiba, Diamond, Vanessa Mdee and others.

"We believe that the festival is going a long way in the discovering of new talents that will be stars of the future," said Kiswaga.

Tigo has provided sponsorship to the festival in order to ensure that the event is heard in the regions of the southern highlands will involve Iringa, Ruvuma, Njombe and Mbeya.

The introduction to the Tigo Music in Tanzania has been driven by the success of its launch in Ghana in 2014 and South America in 2012.
Ends

AMKA NA MAGAZETI LEO JUMATATU NA SIMBAYABLOG





WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...