IRINGA: Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa mjini chapinga vikali shutuma zinazotolewa na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kwamba kinafanya biashara ya kununua madiwani wake.
Akizungumza na Tumbusi blog jana katika mahojiano maalum katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Iringa mjini Edwin Bashiri alisema kuwa chama hicho hakifanyi mnada wa kununua au kuuza madiwani kutoka chama kikuu cha upinzani Chadema isipokuwa madiwani wanahamia CCM baada ya kuchoshwa na uongozi ndani ya chama chao.
Alisema kuwa madiwani wanaohamia CCM kutoka Chadema wanafanya hivyo kwa hiari yao wenyewe baada ya kuona kwenye chama chao kutokana na migogoro ya kiuongozi inayoendelea ndani ya chama hicho.
Bashiri alisema kuwa chama cha mapinduzi hakijawahi kufanya biashara ya kununua madiwani kwa sababu hakuna mnada wakununua au kuuza madiwani.
Naye katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza alisema kuwa wananchi wanatakiwa kupuuza maneno ya uongo kutoka kwa wapinzani kwamba chama hicho hakifanyi biashara yoyote ya kununua madiwani kutoka Chadema.
Baraza alisema kuwa katika ilani ya chama hicho ya mwaka 2015- 2020 imeainisha vitu gani chama hicho kiliahidi wananchi katika kampeni mwaka 2015 ni pamoja ujenzi wa barabara ikiwemo barabara ya kutoka Iringa mjini kuelekea hifadhi ya taifa ya ruaha kwa kiwango cha lami.