Na Gustav Chahe,
Tanga
YUBILEI
YA DHAHABU inatarajiwa kuadhimishwa katika Paroki ya Mt.
Theresia Barabara ya 20 katika Jimbo Katoliki la Tanga.
Adhimisho
hilo linakuja baada ya kukamilika kwa
mchakato wa maandalizi na mafanikio ya utaratibu wa kukusanya maoni ya
waamini na kuyaweka mazingira katika hali nzuri.
Katibu
wa Parokia hiyo Bw. Costantino Mwanga ameeleza kuwa adhimisho hilo
litakuwa ni la pekee tofauti na maadhimisho mengine ukilinganisha na
menginre yaliyokwisha kupita hata kutokana na mazingira yenyewe yalivyo.
Akifafanua
maana ya Yubilei ya Dhahabu, Bw. Mwanga ameeleza kuwa wameamua kuita
hivyo kutokana na tendo hilo kuadhimishwa
kwa mara ya kwanza katika Parokia hiyo na pili kutokana na kuadhimishwa
katika mwaka wa maadhimisho ya yubilei ya miaka 50 ya uhuru wa Taifa.
“Tumeiita
YUBILEI YA DHAHABU kwa sababu ya: kwanza, hatujawahi kuadhimisha
Yubilei ya miaka 25 ya Parokia hii kama wanavyofanya
wengine; hii ni mara ya kwanza kufanya hivyo na pili tumeangalia suala
zima na maadhimisho haya kwa kuwa yanakwenda sambamba na maadhimisho ya
Yubilei ya miaka 50 ya Uhuru wan chi yetu. Hii ni fahari kubwa ambayo
imetufanya tiite kwa jina hilo” anaeleza Bw.
Mwanga.
Ili
kufanikisha maadhimisho kama hayo, suala la ushirikiano
na mshikamano ni la muhimu. Imeelezwa kuwa bila kujali umri na uwezo wa
wadau, michango mbalimbali ya hali na mali
imekuwa ikipokelewa ikiwa ni pamoja na mawazo na ushauri mbalimbali
uliokuwa ukitolewa kwa mijadala ya pamoja.
“Tunachojivunia
ndugu mwandishi ni kuwa na ushirikiano. Suala hii si rahisi akafanya
mtu mmoja kwani ni gumu wala mawazo ya mtu mmoja hayawezi kufanikisha
tukio hili bali mawazo ya watu na michango yao ndiyo mhimili wa
mafanikio vinginevyo ni sawa na kutwanga pilipili mshahara kukohoa”
anaeleza na kuongeza kuwa “ushirikiano baina ya sisi viongozi na
waamini, viongozi na mapadre pamoja na waamini na mapadre ni mzuri ndiyo
maana imekuwa ni rahisi kwetu sisi kupata mafanikio haya”.
Parokia
inapoendelea kuadhimisha Yubilei hiyo imeonekana kukabiliana na
changamoto mbalimbali pamoja na kuwa na mafanikio mengi ambayo
yanatokana na ubunifu wa vyanzo vya mapato na matunda ya uvumilivu
katika kumtegemea Mungu.
Akizungumza
na mwandishi wa makala haya mweka hazina wa Parokia hiyo Bw. Marucus
Msekefu amevitaya vyanzo vya mapatoika Parokia hiyo kuwa ni Misaada
mbalimbali wanayojitoa waamini, Sadaka na mavuno, kupitia mchango wa
kulitegemeza jimbo, michango ya hiari kulingana na mtu anavyojisikia
kutoa”. Anaeleza.
Pamoja
na vyanzo hivyo, Parokia inatarajia kutumia zaidi ya shilingi 100
milioni katika ujenzi wa ukumbi na hosteli ambavyo ni vyanzo vya mapato.
“Tupo
katika ujenzi wa hosteli na ukumbi kwa ajili ya mapato ya Parokia yetu
ambapo tunatarajia kutumia zaidi ya shilingi milioni 100” anaeleza Bw.
Msekefu na kuongeza kuwa “hii ni matokeo ya jitihada za waamini kwa
kutoa michango yao ya hali na mali kwa ajili ya ujenzi huu”.
Hosteli
hiyo ina vumba 9 ambapo itakapokamilika inatarajia kubeba watu 6 hadi 8
kwa kila chumba na ukumbi unatarajia kubeba watu wasiopungua 200, shule
ya chekechea pamoja na kiwanja kikubwa ambacho kinatarajiwa kujengwa
hosteli kubwa itakayobeaba watu wengi zaidi.
Yubilei
hiyo ambayo kilele chake ni Oktoba 2, mwaka huu itatanguliwa na matukio
mbalimbali ambapo Mhashamu Baba Askofu Anthony Banzi wa Jimbo hilo
anatarajiwa kufungua shule ya awali Marungu, kufungua Golota la B.
Maria Marungu, ufunguzi wa Kanisa la Marungu ambako huko atatoa
Sakramenti ya Kipaimara na Ndoa ambayo hayo yatafanyika Septemba 30
mwaka huu.
Oktoba
1, Mhashamu Baba Askofu Banzi anatarajiwa kuweka jiwe la msingi kwa
ajili ya ujenzi wa Kanisa katika kigango cha Duga kilichop ndani ya
Parokia hiyo pamoja na kufanya ufunguzi wa ukumbi na hosteli parokiani
hapo.
Siku
ya kilele chenyewe, Mhashamu Baba Askofu Banzi atatoa Sakramenti ya
Kipaimara, Sakramenti ya Ndoa kwa watu mbalimbali wakiwemo walioishi
katika umba sugu pamoja na kuwaombea waliotimiza Yubilei ya miaka 50 ya
ndoa.
Licha
ya kuwepo kwa mafanikio katika Parokia hiyo, imeelezwa kuwa kuna
changamoto mbalimbali zinazoikabili katika kaziya uinjilishaji ambazo
zinatoa fursa kwa waamini hao na uongozi kukabiliana nazo kwa nguvu zote
bila kuchoka.
Akizungumza
na mwandishi wa makala haya parokiani hapo, mwenyekiti wa Parokia hiyo
Bw. Karol Makungu anaeleza kuwa zipo changamoto mbalimbali zinazoweza
kukwamisha uinjilisha katika parokia hususani katika jimbo zima.
“Tusiseme
tuna mafanikio pekee yake bali tunakabiliana na changamoto mbalimbali
ambazo bila ya kupambana nazo kwa uvumilivu, uinjilshaji unaweza
ukayumba” anasema na Bw. Makungu na kuongeza kuwa “changamoto kubwa ni
kujitokeza kwa wale wasiomjua Kristo na kutaka kutuvuruga lakini kwa
pamoja tunasimama na kumtukuza Kristo kwa nguvu zote ili hata wale ambao
bado kwao ni msamiati, wapate kumjua na baadaye waweze kumkiri ya kuwa
Kristo ni Bwana na mwokozi wa maisha yao”.
Hata
hivyo, akizungumzia suala la Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo Bw. Mwanga
anaeleza kuwa kunamafanikio ingawa zipo changamoto ambazo kama
zingezingatiwa lisinkuwa ni tatizo sana.
“Kwa
upandea wa Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo, kuna changamoto lakini
kubwa zaidi inatokana na akina Baba kutohudhuria kwa sababu za kusema
kuwa wamebanwa na majukumu ya utafutaji lakini kama hili
lingezingatiwa na wakaweza kujitoa kwa wingi basi, tunaweza tukalimaliza
lakini akina Baba ndio ambao kwenye Jumuiya hawaonekani”. Anaeleza.
Kwa
upande wa uhai wa vyama vya kitume pia nako hakusita kuzungumza kwa
kile alichosema uhai upo wa kuridhisha na kuwataka waamini kuimarisha
mshikamano, upendo na uadilifu katika kumtumikia Mungu,
“Ndugu
mwandishi, kwa upande wa vyama vya kitume kwa ujumla kuna uhai
unaoridhisha na labda ambacho ningeweza kusema, ni kwamba wasikate tamaa
bali waendelee kudumisha upendo, mshikamano bila kusahau matendo ya
huruma kwa kila mtu bila kujali itikadi mbalimbali na madhehebu au dini”
anaeleza.
Wakati
huo huo Makamu mwenyekiti wa Parokia hiyo Bw. Feddy Rocky amewakumbusha
waamini kuwa katika mapambano dhiti ya wokovu hakuna kulala wala hakuna
kujisahau kwani shetani anaweza akawateka.
“Mimi
ninachoweza kusema ni kwamba, katika mapambano ya wokovu tusijisahau
kwani mwovu shetani anaweza akatuteka ila wakumbuke kuwa kanisa
litajengwa na sisi wenyewe wala katika miaka ya leo tusitegemee watu
kutoka nje kuwa watalijenga Kanisa letu; kazi kubwa imebaki mikoni mwetu
hawawezi kurudi tena kuja kutujengea, tujitoe kwa moyo wetu wote kwa
hali na mali ili tuweze kujenga Kanisa letu” anaeleza Bw. Rocky
Mbali
na adhimisho la yubilei hiyo, siku hiyo kutakuwa na uzinduzi wa albam
ya Kwaya ya Mt. Alois Gonzaga yenye jina la “TUISHI KAMA NDUGU” yenye
jumla ya nyimbo 10.
Parokia
ya Mt. Teresia ina jumla ya vigango 10 ambavyo ni Kigango
Mama, Kigombe Bago, Marungu, Mapojoni, Mbuyukenda, Kirare Korosini na
vingine ni Kirare Bango, Mgwisha, Neema pamoja na kigango cha Duga
ambapo kila kigango kina makatekista wakutosha.
Parokia
imefanikiwa kuto Padre mmoja mwaka 2007 ambaye ni Pd. Augustino Temu
pamoja na masista 2 ambao ni Sr. Aristidia Mchunguzi na Sr. Sara Mpera
Parokia
ya Mt. Teresia Ngamiani Tanga ilianzishwa mwaka 1961 chini ya mapadre
wa misionari Warosmini ambapo awali kilikuwa kigango mojawapo cha
Parokia ya Mt. Anthony Chumbageni.
| |
Saturday, 1 October 2011
Waijua Yubilei ya Dhahabu?
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...