Thursday, 21 September 2017

SHAHIDI AIELEZA MAHAKAMA JINSI DC ALIVYOPEKUWA CHUMBA CHAKE



Na Woinde Shizza


SHAHIDI wa utetezi katika kesi ya kughushi Mukhtasari,wa serikali ya mtaa wa Levolosi ,mfanyabiashara ,Mathew Moleli ameieleza mahakama jinsi mkuu wa wilaya mstaafu alivyoingia kwa mabavu nyumbani kwake na kuamrisha askari polisi aliokuwa ameambatana nao wapekuwe chumba chake wakitafuta hati inayodaiwa kughushiwa.

Akitoa utetezi mbele ya hakimu Gwanta Mwankuga wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha ,anayesikiliza shauri hilo huku akiongozwa na wakili wa utetezi Ephraim Koisenge, aliieleza mahakama hiyo jinsi alivyofedheheshwa wakati askari hao,akiwemo mwendesha bodaboda na mlalamikaji Makanga walivyopekuwa chumba chake wakitafuta hati ambayo ni mali.

Shahidi huyo aliiendelea kueleza kuwa, mnamo oktoba ,2 mwaka 2014 alishtakiwa katika mahakama ya wilaya iliyopo Sekei mkoani Arusha, kwa shauri kama hilo huku mlalamikaji akiwa ni Danny Makanga na baadae oktoba 1,mwaka 2015 kesi hiyo ilifutwa baada ya upande wa jamhuri kuomba kuondoa shauri hilo mahakamani jambo ambalo anadai linampotezea muda wake.


Alidai kuwa kufutwa kwa shauri hilo aliandika barua kwa mkuu wa upelelezi wa mkoa wa ARUSHA (RCO) kuomba kurejeshewa hati yake ya nyumba iliyokuwa inashikiliwa ofisi ya RCO, jambo ambalo hakuwahi kujibiwa hadi oktoba ,28 mwaka 2016 alipokamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani akishtakiwa kwa makosa mawili ya kughushi Mukhtasari wa serikali ya mtaa wa Levolosi na kuwasilisha nyaraka za kughushi katika ofisi za jiji la Arusha ,

Hata hiyo upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali Mary Lucas ulimtaka mshtakiwa kueleza uhalali wa eneo anakoishi kwa sasa ,jambo ambalo shahidi huyo alisema ni mali yake na waliuziana kindugu na mlalamikaji Makanga bila kuandikishana na baadae alifuata taratibu zote za kuomba hati miliki kupitika kikao cha dharura kwa uongozi wa serikali ya mtaa wa Levolosi kilichoketi Septemba,10 mwaka 2006.


Pia shahidi huyo alieleza kuwa tangu kikao hicho cha serikali ya mtaa kiketi kwa dharura na baadae kupeleke maombi ya kupatiwa hati ya umiliki wa nyumba yake kiwanja namba 231 kitalu DD kilichopo Mianziani jijini Arusha ,hakuwahi kupata malalamiko yoyote kuhusu kughushi nyaraka za serikali,jambo ambalo ameiomba mahakama kuifuta kesi hiyo kwa sababu malalamiko hayo hayana ukweli wowote.


Kesi hiyo namba 430 ya mwaka 2016 inatarajiwa kuendelea tena ,Septemba 28 mwaka huu ,ambapo upande wa utetezi unatarajia kufunga utetezi wake kwa shahidi wa pili na wa mwisho baada yashahidi wa kwanza ambaye ni mshtakiwa kukamilisha utetezi,ambaye pia aliwasilisha nyaraka mbalimbali kama vielelezo mahakamani hapo.

Awali wakili wa serikali Mary Lucasi alipinga kuwasilishwa kwa baadhi ya nyaraka muhimu za mshtakiwa mahakamani hapo kwa madai kuwa nyaraka hiyo ni kivuli ,jambo ambalo lilipigwa na wakili wa utetezi Koisenge ambaye aliiomba mahakama izipokee kama kilelezo,jambo ambalo hakimu Mwankuga baada ya kuzipitia hoja ya upande wa mashtaka aliona hazina mashiko na kuzipokea ili zitumikea mahakamani hapo kama kielelezo.

AVUNJWA MGUU KWA RISASI


Mkazi wa kitongoji cha Endevesi ,kata ya Oljoro wilaya ya Arumeru,Hwanga Ndaskoy(30)amefunjika mkuu wake wa kulia baada ya watu wanaodaiwa kuwa ni askari polisi mkoani Arusha, wapatao nane kumvamia na kumpigwa risasi ,akiwa shambani kwake .


Akizungumza kwa masikitiko nyumbani kwake, baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Mount Meru alikokuwa amelazwa kwa zaidi ya wiki moja,Ndaskoy ameeleza kwamba tukio hilo limetokea mnamo,Agost 31,mwaka huu majira ya saa saba wakati akivuna mahindi shambani kwake akiwa na familia yake.


Alisema kua alifuatwa na askari hao waliokuwa wamevalia kiraia na mmoja mwenye silaha akiwa amevaa sare za kipolisi.


Pia askari hao walikuwa wameongozana na mkazi mmoja wa kitongoji hicho aliyemtaja kwa jina la ,Yohane Palay aliyemtambua kuwa ni baba mkwe wake .



‘’Nilimsikia baba mkwe akiwaelekeza askari hao wanikamate huku akiwatahadhalisha kuwa mimi ni mkorofi na wasinisogelee nitawakata na sime jambo ambalo sio kweli,ndipo askari mmoja mwenye silaha aliponifyatulia risasi ya mguu na kuanguka chini’’alisema Ndaskoy 


Aidha alisema askari baada kumpiga risasi walimpakia kwenye gari lao na kumpeleka katika hospital ya Mkoa Mt,Meru ambapo walimweleza daktari kuwa ameanguka na pikipili Jambo ambalo si kweli.


Alieleza kuwa kabla ya tukio hilo ,Agost 26 mwaka huu ,aligombana na mke wa kaka yake aitwaye ,Jehova Baraka ambaye wanaishi jirani baada ya mbuzi kula mahindi yake yaliyokuwa nyumbani .


Alisema ugomvi huo ulienda mbali zaidi kiasi cha kutoleana maneno makali ,ambapo Jehova aliamua kwenda kwa baba yake mzazi aitwaye Yohane Palay na kutoa taarifa kuwa amepigwa na shemeji yake .


Palay aliamua kwenda kituo cha polisi cha Mbauda jijini hapa na kutoa taarifa juu ya tukio hilo,hata hivyo viongozi wa kitongoji hicho wakiwemo wazee wa ukoo waliingilia kati na kumtaka Palay alirejeshe nyumbani ili wazee wa ukoo walipatie ufumbuzi wa kudumu jambo ambalo waliafikiana.


Alisema Kikao cha ukoo kiliketi,agost 30 na kukubaliana kumaliza jambo hilo kwa kuwatoza faini za kimila wahusika wote wawili baada ya kubaini wote wanamakosa,hata hivyo walishangaa kesho yake agost 31 kufuatwa na polisi na kupigwa risasi.


Kwa upande wake,Palay alikiri kupeleka malalamiko yake kituo cha polisi ,Mbauda ,akidai kuwa mtoto wake,ambaye ni mke wa kaka yake na majeruhi alipigwa na kudhalilishwa. Hata hivyo aalikana kuwarubuni Polisi ili wampige risasi mtuhumiwa





Akizungumzia tukio hilo,kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo alisema kuwa anafuatilia undani wa tukio hilo ikiwemo kubaini ni askari gani walienda kwenye tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi.


"Kwa kweli sina taarifa ya tukio kama hilo ila nitachunguza kama lipo nitalitolea ufafanuzi" Kauli ya Mkumbo.


Mkumbo alisema analifanyia uchunguzi jambo hilo kupitia wasaidizi wake na kuahidi kuchukua hatua kali iwapo itabainika hapakuwa na ulazima wa matumizi makubwa ya silaha ya moto kwa askari wake.


Na Woinde Shizza 





WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...