Monday, 20 June 2016

Watanzania wapata fursa ya kushiriki mafunzo kuhusu Tsunami

Kutokana na kuwa na athari kubwa ambazo zimekuwa zikisababisha majanga makubwa, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeandaa mafunzo ya siku tano ambayo yatashirikisha watu mbalimbali nchini ili kuwapa elimu kuhusiana na majanga.

Akizungumzia Mafunzo hayo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Zulmira Rodrigues alisema kupitia mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kupata elimu kuhusiana na Tsunami ikiwa ni pamoja na madhara ambayo yanasababishwa na hivyo ni matarajio yao watakuwa mawakala wazuri kwa kusambaza elimu hiyo kwa Watanzania wengine.

"Watu wengi wamepoteza maisha tukumbuke Tsunami la Japan zaidi ya watu 20,000 walipoteza maisha kwahiyo tunataka mafunzo haya yasaidie kufahamu ni kwa kiasi gani Tsunami linakuwa na madhara hata kama limetokea mbali na hapa," alisema Bi. Rodrigues.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamuriho alisema ni vyema kwa watanzania kupata elimu hiyo kutokana na madhara ambayo yamekuwa yakitokea ikiwemo Tsunami la mwaka 2004 ambalo lilitokea eneo lililombali na bahari ya Hindi lakini lilisababisha athari nchini na kusababisha vifo vya waogeleaji watano.

"Mafunzo haya yanatakiwa kufanyika kwa wananchi wote na mwezi Septemba yatafanyika mengine na yatahusisha watu wengi lengo kila Mtanzania ajue nini cha kufanya siku athari zikitokea wajue nini wanafanya ni muhimu kwa kila mtu kujua athari za Tsunami hata likitokea mbali," alisema Dk. Chamuriho.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kitengo kinachoshughulikia Tsunami, Ardito Kodijat akifungua mafunzo hayo kwa kuwaeleza washiriki aina ya mafunzo ambayo watapatiwa. (Picha na Rabi Hume, MO Blog)

2. Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akitoa neno la ufunguzi kwa niaba ya UNESCO Tanzania na kueleza sababu ya kufanyika mafunzo hayo.
3. Mkuu wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hewa nchini (TMA, Dk. Ladislauds Chang`a akizungumza jinsi TMA imejipanga kuendeleza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Tsunami na kuwataka Watanzania kuwa na utaratibu wa kufatilia hali ya hewa nchini hasa katika kipindi hiki ambacho ni kuna mabadiliko ya tabia ya nchi.
4. Baadhi ya washiriki ambao wameshiriki katika mafunzo hayo ambayo yanataraji kufanyika kwa siku tano.
5. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamuriho akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo yanayohusu kuwapa elimu washiriki ya kuhusu Tsunami. (Picha na Rabi Hume, MO Blog)
6. Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja. (Picha na Rabi Hume, MO Blog)

Tanzania yatajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez akielezea jinsi UN waevyojipanga kuwasaidia watu wenye ualbino. Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero.
Tanzania yatajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino.

Pamoja na juhudi ambazo serikali imekuwa ikizifanya ili kuhakikisha Watanzania wenye ualbino wanakuwa salama na amani lakini bado Tanzania inaendelea kuwa nchi ya hatari kwa watu hao kwa kuwa katika orodha ya nchi ambazo zina kiwango kikubwa cha unyanyasaji.

Akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha kongamano la kikanda kwa ajili ya hatua kuhusu ulemavu wa ngozi Afrika lililofanyika Dar es Salaam, Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero alisema kuwa kwa ripoti ambazo wamekuwa wakizipokea inaonyesha Tanzania ni moja ya nchi ambazo zina unyanyasaji kwa watu wenye ualbino.

"Tangu nimeingia sijawahi kufanya uchunguzi hata katika matokeo ya uchunguzi wa nchi 29 sijaujua sana lakini kwa taarifa ambazo nimekuwa nikipata kutoka kwa taasisi mbalimbali inaonyesha Tanzania ni unyanyasaji wa hali ya juu kwa watu walio na uablino," alisema Ero.
Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Shirika la Kimataifa la Under The Same Sun, Vicky Ntetema na kulia ni Mkuu wa Mawasiliano wa Shirika la Standing Voice, Sam Clarke.

Nae Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanguga alisema katika kongamano hilo wametoka na maazimio ambayo wanaiomba serikali iweze kuyafanya ili kuwezesha watu wenye ualbino kuwa na usalama wa uhakika.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga. Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero na kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez.


"Tumejadili mambo mengi lakini tunaiomba serikali ihusike moja kwa moja kupinga unyanyasaji, ukatili na ubaguzi nia tunaiona kwahiyo tunaomba waendelee kuwa hivyo na pia waongeze bajeti na zaidi katika matibabu kwa watu wenye ualbino," alisema Nyanduga.

Kwa upande wa Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia Mratibu Mkazi wa mashirika hayo, Alvaro Rodriguez alisema ni wataendelea kuwasaidia watu wenye ualbino ili kuwezesha kupunguza changamoto ambazo zinawakabili.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...