Sunday, 13 September 2015

CCM MAFINGA MJINI CHA ZOA WANACHAMA 50 KUTOKA CHADEMA


Mgombea Ubunge Jimbo la Mafinga mjini akinadi sera na ilani za chama chake jana mjini Mafinga katika uzinduzi wa kampeni za ubunge.


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Mafinga Mjini ambalo ni jimbo jipya la uchaguzi kimezoa wanachama wapya kutoka Chama cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakati wa uzinduzi wa kampeni za ubunge zilizofanyika katika viwanja vya Mashujuu jana.


Wanachama hao wapya walikabidhiwa kadi za chama hicho na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatangu ambaye alikuwa mgeni rasmi.


Wanachama huo wapya wakiongea na Nipashe muda mfupi baada ya kukabidhiwa kadi za CCM kwa nyakati tofauti walisema wameamua kutoka CHADEMA na kujinunga na CCM kutokana sababu nyingi kubwa ni chama cha CHADEMA kuendesha siasa za kuhamasisha vujo.

Walisema kuwa wamechoshwa na maneno na vitendo vya Mgombea urais kupitia Chadema Edward Lowassa na makada wenzake wa CHADEMA na vyama shirika vya UKAWA toka wameanza kampeni katika maeneo mbalimbali ya nchi na kwa nyakati tofauti zimejaa ghiriba na ubaguzi uliokithiri. 

Waliendelea kusema kuwa tabia hizi za Lowassa ni moja ya sababu iliyopelekea CCM kutompa nafasi ya kugombea kupitia Chama hichi.

Mgombea ubunge jimbo la Mafinga mjni Cosato Chumi Jumapili wiki iliyopita alizindua rasmi kampeni zake za kuwania ubunge katika jimbo hilo mpya la Mafinga mjini ambalo limemegwa kutoka Jimbo la Mufindi Kaskazini na Tume ya Uchaguzi ya taifa (NEC). 

Chumi alisema atahakikisha anasimamia vyema ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo imekidhi mahitaji ya watanzania na amewataka wakazi wa Mafinga kutofanya makosa kwa kumpitisha mgombea kutoka vyama vingine kwani watapelekea kudumaza maendeleo ya Mafinga mjini. 

Aidha Chumi amesema endapo wananchi watamchugua pamoja na madiwani wa CCM watawapa nguvu na kupelekea maendeleo hasa utatuzi wa tatizo la maji ambalo limetokana na kuongezeka kwa idadi ya watu.




Mgombea ubunge jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akikabidhiwa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM na mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu.


Pia amesema usalama wa raia ni muhimu atahakikisha vituo vya polisi vinaongezwa katika kila kata hili kuongeza usalama pia amevitaja vipaumbele vifuatavyo endapo wakazi wa jimbo la Mafinga mjini watampa kura za ndio yeye, madiwani wote wa CCM pamoja na mgombea Uraisi wa chama hicho JOHN POMBE MAGUFULI ambavyo ni pamoja na kuongeza vituo vya afya, kuboresha elimu pamoja na mikopo kwenye vikundi vya kina mama.




Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa


Aidha mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Jesca Msambatavangu amesema Ilani ya chama ni mkataba kati ya CCM na watanzania kwa sababu imechukua mipango ya maendeleo tangu CCM imeanza kuitawala nchi hadi mwaka 2025.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...