Kujumuishwa kwa wabunge wa vyama vya CUF na Chadema ni matunda ya kuundwa kwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakati wa Bunge la Katiba.
Hivi karibuni, Mbowe alikaririwa na gazeti hili akisema hatua hiyo imefikiwa baada ya "kila upande kukubali kuwa unamhitaji mwenzake katika harakati za kuikomboa nchi hii."
Ukawa ndiyo iliyowaongoza baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu kutoka nje kususia mchakato wa Katiba Mpya kutokana na kile ilichodai kuwa ni kutokuridhishwa na jinsi mambo yanavyokwenda.
Wakati huohuo; wabunge wamekubaliana kuwa shughuli za Bunge zitakuwa zikianza saa 3:00 asubuhi na kusitishwa saa 7:00 mchana na kurejea tena saa 10:00 alasiri hadi saa 2:00 usiku.
Ratiba hiyo itahusisha pia Ijumaa na Jumamosi.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah alisema utaratibu huo utaongeza nafasi za wabunge kuchangia katika Bunge la Bajeti.
Imeandikwa na Sharon Sauwa, Daniel Mjema na Edwin Mjwahuzi
Chanzo: Mwananchi