Tuesday, 31 May 2016

MKUTANO WA 12 WA BARAZA LA WADAU WA MAZIWA TANZANIA

Kutoka kushoto ni Msajiili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Nelson Kilangozi, Kaimu wa Mwenyekiti wa Baraza la Wadau wa Maziwa Tanzania, Mark Tsoxo, Mwenyekiti wa Baraza la Wadau wa Maziwa Tanzania Dr. Ally Majani, Mwenyekit wa Bodi ya Maziwa Tanzania Aichi Kitalya na mwakilishi kutoka wizarani. 


Mwenyekiti wa Baraza la Wadau wa Maziwa Tanzania Dr. Ally Majaniakifungua mkutano wa mwaka wa kumi na mbili (12) wa baraza hilo ,unahusisha wajumbe wote waliochagauliwa toka katika wilaya zote Tanzania unaofanyika mkoani Njombe, wakati wa maadhimisho ya Kitaifa ya wiki ya Maziwa.

Maadhimisho ya wiki ya maziwa kitaifa yanafanyika katika viwaja vya shule ya sekondari Mpechi mkoani Njombe ambapo kesho ni kilele.




















NJOMBE: Kaimu Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Anatory Choya Amewaagiza Walimu Wa Kuu Na Wakurugenzi Kuanzisha Utaratibu Wa Kufuga Ng'ombe Wa Maziwa Kwa Shule Za Sekondari Na Msingi Ili Wanafunzi Waweze Kunufaika Na Elimu Ya Ufugaji Wa Ng'ombe Hao Na Kutambua Umuhimu Wa Kunywa Maziwa Na Kuendelea Utalaamu Wa Kufuga Hata Wakirudi Uraiani.

Kauli Hiyo Na Kaimu Mkuu Wa Mkoa Huyo Choya Wakati Akiwa Mgeni Rasmi Kwenye Uzinduzi Wa Wiki Ya Uhamasishaji Wa Unywaji Maziwa Ambayo Kilele Chake Kinatarajia Kufanyika June Mosi Mwaka Huu Yakifanyikia Katika Uwanja Wa Shule Ya Sekondari Mpechi Mjini Njombe Ambapo Endapo Shule Zitakuwa Na Ng'ombe Mmoja Itasaidia Wanafunzi Kupata Maziwa Na Kujifunza Namna Wanavyoweza Kufuga.

Choya Amesema Wakurugenzi Wanatakiwa Kwenda Kufanya Kila Liwezekanalo Kwaajili Ya Kuhakikisha Shule Hizo Zinakuwa Na Ng'ombe Hao Na Kupeleka Watalaamu Wa Mifugo Ambao Watasimamia Na Kuelimisha Wanafunzi Namna Ya Kuwafuga Ng'ombe Hao Huku Akitaka Wazazi Kuhakikisha Wanapunguza Tatizo La Udumavu Kwa Watoto Kwa Kuwapatia Maziwa Kama Lishe Bora Kwa Watoto.

Katika Hatua Nyingine Choya Amewataka Wafanyabiashara Wa Maziwa Kuacha Tabia Ya Kuuza Maziwa Yaliyokwisha Muda Wake Wa Matumizi Kwa Binadamu Kwani Siku Chache Zilizopita Kuna Baadhi Ya Wafanyabiashara Wamekamatwa Wakiwa Na Maziwa Yaliyokwisha Muda Wake Jambo Ambalo Linasababisha Wananchi Kupata Madhara Ya Magonjwa Bila Kujitambua.

Awali Akizungumza Mwenyekiti Wa Bodi Ya Maziwa Tanzania Daktari Wa Mifugo Aichi Kitalyi Pamoja Na Kupongeza Wananchi Wa Mkoa Wa Njombe Kwa Juhudi Za Kuzarisha Na Kuendeleza Mpango Wa Unywaji Maziwa Lakini Amesema Wananchi Wanatakiwa Kunywa Maziwa Kama Chakula Na Siyo Kama Dawa Na Elimu Itaenea Kwa Wananchi Wote Katika Kipindi Hiki ChaMaadhimisho Hayo.

Kwa Upande Wake Makamu Mwenyekiti Wa Baraza La Wadau Wa Maziwa Bwana Mark Tsoxo Amesema Mkoa Wa Njombe Una Hali Ya Hewa Nzuri Inayoruhusu Ustawishaji Wa Ng'ombe Wa Maziwa Na Hivyo Wadau Na Wananchi Wanatakiwa Kuwekeza Kwenye Ufugaji Wa Ng'ombe Wa Maziwa Huku Akiomba Serikali Kusaidia Kuweka Mazingira Mazuri Yanayovutia Uwekezaji Wa Maziwa Kwa Sekta Binafsi.

Kauli Mbiu Ya Maadhimisho Hayo Kwa Mwaka Huu Inasema Jenga Tabia Ya Kunywa Maziwa Kwa Afya Na Uchumi.

MAANDALIZI YA UTAFITI WA VIASHIRIA NA MATOKEO YA UKIMWI TANZANIA 2016/2017 YAANZA RASMI



Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa Akizungumza na wadau wa Utafiti wa Viashiria na matokeo ya Ukimwi wakati wa mkutano wa wadau hao uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na masuala ya Afya – ICAP kutoka chuo cha Colombia New youk, Dkt. Fernando Morales akizungumza mbele ya wadau wa Utafiti wa Viashiria na matokeo ya Ukimwi wakati wa mkutano wa wadau ha oleo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Kudhiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Bibi. Fatma Mrisho Akizungumza na wadau wa Utafiti wa Viashiria na matokeo ya Ukimwi wakati wa mkutano wa wadau hao uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wadau. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa wa tatu kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa NBS jijini Dar Es Salaam leo.

Wito umetolewa kwa wadau pamoja na wananchi ili kushiriki kikamilifu katika kuwezesha upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.

Akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema wananchi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wana mchango mkubwa katika kufanikisha upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.

“Leo hii tumekutana na wadau mbalimbali wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu kwa ajili ya kujadili na kushauriana namna ya kufanya utafiti huu kwa ufanisi ili kupata takwimu bora zitakazosaidia katika kutunga sera na kupanga mipango ya maendeleo nchini”, amesema Dkt. Chuwa.

Dkt. Chuwa amefafanua kuwa utafiti huu unategemea sana ushiriki wa wananchi kwani wao ndio wadau na wahusika wakuu ambao wanapaswa kutoa ushirikiano wa kutosha ili kurahisisha upatikanaji wa takwimu rasmi zitakazosaidia Taifa katika kuboresha huduma za afya kwa manufaa ya watanzania wote.

Dkt. Chuwa amesema Ofisi ya Taifa ya Takwimu ipo katika harakati za kukamilisha maandalizi ya utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania 2016/2017 ambao utaanza kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi Juni mwaka huu. 

Aidha Dkt. Chuwa amesema utafiti huu ni wa kipekee ukilinganishwa na tafiti zilizotangulia kutokana na kuongezeka kwa viashiria vitakavyo chunguzwa ikiwemo kuangalia kiwango cha CD4, kiwango cha maambukizi mpya, upatiakanaji wa huduma zinazohusiana na UKIMWI pamoja na kupima watoto wadogo wenye umri chini ya mwaka mmoja.

Amesisitiza kuwa kukamilika kwa utafiti huu kutasaidia Serikali katika kuboresha huduma za afya nchini hasa katika kupambana na maambukizi mapya ya UKIMWI na namna ya kuboresha upatikanaji wa vifaa tiba.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa ICAP nchini, Dkt. Fernando Morales amesema utafiti huu ni wa muhimu katika kupima viashiria na matokeo ya UKIMWI kwa nchi ambazo zimekuwa zikipata msaada wa kupambana na UKIMWI kutoka Serikali ya Marekani.

“Lengo la Utafiti huu ni kupata viashiria ambavyo vinasababisha maambukizi mapya pamoja na kupima jinsi gani Taifa limeweza kupambana na ugonjwa wa UKIMWI nchini”, amesema Dkt. Morales. 


Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 unafanyika katika nchi Ishirini (20) Afrika ambapo kwa sasa nchi nane (8) zinaendelea na utafiti huu zikiwemo Zimbabwe, Zambia, Malawi, , Lesotho, Swaziland, Uganda, Namibia na Tanzania.

SAKATA LA MAUAJI YA FAMILIYA BILIONEA MSUYA,KAMANDA SIRRO AMDAKA HUYU


Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) juu ya Jeshi lake kuendelea na operesheni mbalimbali jijini Dar es salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii


JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikiria mtu mmoja kwa tuhuma za mauaji ya Anneth Msuya aliyeuawa kwa kuchinjwa hivi karibuni, Kigamboni wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon Sirro amesema kuwa wanamshikilia mtu huyo kwa uchunguzi wa tuhuma za mauaji ya mwanamke huyo.


Sirro amesema kuwa katika tukio la mauji ya mwanamke Anneth Msuya polisi wako katika upelelezi na hawezi kutaja jina la mtu wanayemshikilia kutokana na sababu za kiusalama na kuhofea kushindwa kuwakamata watu wengine.


Tukio la kuuawa kwa Anneth Msuya lilitokea Mei 26 nyumbani kwake Kibada, Kigamboni jijini Dar es Salaam, limekuwa ni mwendelezo wa matukio mengine ya uhalifu kwa familia yao yaliyowahi kutokea baada ya kifo cha kaka yake, Msuya aliyeuawa Agosti 2012 kwa kupigwa risasi, tukio lililofanyika mkoani Kilimanjaro.


Wakati huo huo majambazi wawili wameuawa kwa kupigwa na polisi na mmoja aliuawa wananchi baada ya bastola yake kuishiwa risasi huko maeneo ya Mburahati Minazini akiwa anawatupia risasi, huku mmoja akikamatwa akiwa na pikipiki aina ya boxer yenye namba za usajili MC 444 BFY na wananchi walimshambulia.


Bunduki waliokuwa nazo ni bastola yenye namba za usajili 649440 na bastola nyingine aina ya Chinese Star ambazo silaha hizo ndizo walikuwa wanafanyia uhalifu.


Amesema pia jeshi la polisi linaendelea na operesheni mbalimbali na wanapata ushirikiano na wananchi ikiwa ni pamoja na kukamata watoto wadogo wanaotembea kundi kubwa na kuvamia na kupora kwa wananchi (maarufu panya road)


Pia alimalizia kwa kusema, Jeshi la polisi limekusanya sh. 548, 160,000 kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabara kwa magari na pikipiki.




Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon Sirro akionyesha silaha mbili aina ya bastola, zilizokamatwa katika Matukio ya Uhalifu jijini Dar.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon Sirro akionesha gari iliyo tumika kufanya uhalifu leo jijini Dar es Salaam.


Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Kamishina (CP), Simon Sirro akionesha silaha mbalimbali zinazo tumika kufanyia uhalifu (Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Ja Jamii)

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...