Monday, 17 August 2015

DJ WA KINAIJERIA KUFANYA ONYESHO NA KUTOA MSAADA KWA JAMII JIJINI DAR ES SALAAM



Mtengenezaji wa muziki, mtunzi wa nyimbo na DJ raia wa Naijeria anayefanya kazi zake nchini Marekani Bi. Florence Ifeoluwa maarufu kama DJ Cuppy akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Slipway jijini Dar



Waandishi wa habari wakiwa kazini

WAZAZI MATINEJA WAHITIMU ELIMU MBADALA



Second Secretary wa Ubalozi wa Japan, Noriko TANAKA (kulia) akipokea kitabu cha wageni kutoka kwa Mratibu wa kata ya Segese iliyopo halmashauri ya Msalala, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, Bi. Victoria Maige alipofikia katika ofisi hizo kwa ajili ya zoezi la kusaini kitabu cha wageni kabla ya kuelekea kwenye mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga

WAZAZI wenye umri mdogo 149 mkoani Shinyanga ambao walipata mimba wakiwa shuleni wamekamilisha mafunzo ya miaka miwili ya stadi mbalimbali za maisha mkoani hapa.

Wazazi hao wenye umri mdogo ni miongoni mwa wazazi 220 walioanza mafunzo hayo miaka miwili iliyopita chini ya mradi wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhiliwa na Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.

Wazazi hao vijana kutoka wilaya tatu za mkoa wa Shinyanga za halmashauri ya Shinyanga, Msalala na Kahama walikuwa wanajifunza katika vituo 10.

Wengine walishindwa kuhitimisha mafunzo yao kwa sababu tofauti.

Pamoja na kumaliza mafunzo hayo na wengine kujiandaa kwa masomo ya sekondari, wanafunzi hao walijifunza shughuli mbalimbali ambazo zinawawezesha kujiajiri na kuongeza kipato kwa familia zao.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...