Friday, 20 March 2015

ONDOKA

POLISI WAMALIZA MZOZO WA TUNDUMA


JESHI la Polisi mkoa wa Mbeya, limefanikiwa kuzima mzozo na vurugu zilizodumu kwa siku tatu eneo la Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya.

Vurugu hizo zilitokea baada ya kiongozi wa Mtaa wa Makambini kata ya Sogea (chadema) kuwadanganya baadhi ya wananchi anaowaongoza kuwa alikuwa ameshinda kesi ya kiwanja kinachomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi(CCM), na kuamuru uchimbwe msingi ili ijengwe hospitali.

Je Wajua Kilimo cha Nyanya kwenye Banda-kitalu




Kama ilivyo kwa vijana wengi wanaohangaikia maisha, Darius Cheruiyot wa Silibwet, Tarafa ya Bomet, amejaribu kushindana na maisha kwa njia nyingi, amejaribu ufundi makanika, udereva hadi kuwa dereva wa bodaboda. 

Huko kote hakukumfanikisha kimaisha hadi alipojishughulisha na kilimo. Darius (36) mkulima wa nyanya anapenda kuwashirikisha kwenye kilimo cha nyanya kwa kutumia banda kitalu (green-house). “ Wazo la kuanzisha banda kitalu ili kulima nyanya liliibuka mwaka 2012 baada ya kutembelea shamba la binamu yangu. Nilivutika sana na kile nilichokiona.” Cheriiyot alibainisha. Aliamua kulima kwa kilimo cha banda kitalu kwani alikuwa amejaribu kulima nyanya kwenye eneo la wazi; alipata hasara kwa kuwa nyanya zilishambuliwa na magonjwa na wadudu waharibifu.

SAMAKI WAADIMIKA MTERA


Soko Kuu la Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa linakabiliwa na uhaba wa samaki kutokana na uvuvi haramu unaoendelea katika Bwawa la Mtera.

Baadhi ya wafanyabiasha wa samaki walioongea na gazeti la Nipashe leo walisema uhaba wa samaki katika soko hilo unatokana na sababu nyingi na kubwa zaidi ni uvuvi haramu uliyokidhiri katika Bwawa la Mtera.

TANZANIA, JAPAN WATILIANA SAINI UJENZI WA KITUO CHA UFUNDI STADI ILEJE


Signing the grant contract, witnessed by Hon. Janet Mbene, Deputy Minister of Industry and Trade, and Hon. Rosemary Senyamule, Ileje District Commissioner. Front line from the left: Mr. Mussa Otieno, District Executive Director, Mr. Simon Mwango'nda, Executire Director of the recipient organisation, Integrated Rural Development Organisation, Mr. Kazuyoshi Matsunaga, Chargé d'affaires of the Embassy of Japan.

Na Mwandishi wetu

MKATABA wa Ujenzi wa kituo cha mafunzo ya ufundi stadi katika Wilayani Ileje, Mkoani Mbeya umetiwa saini.

Mradi huo uliobuniwa na Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Janet Mbene na Simon Kamiyoge umelenga kuwawezesha wakazi wa Ileje kuwa na taaluma ya ufundi na baadae kutumika kuendelea wilaya hiyo.

Mkataba huo ulitiwa saini kati ya Kazuyoshi Matsunaga wa ubalozi wa Japan nchini na na Mwakilishi wa Integrated Rural Development Organisation (IRDO) Simon Kamiyoge wakishuhudiwa na Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Janet Mbene , Mbunge wa Ileje Rosemary Staki na Mkuu wa wilaya ya hiyo Mohamed Maliyao Mwala, na Mwenyekiti wa halmashauri ya Ileje Musa J. Otieno na maofisa wengine wa wilaya hiyo.

Kaimu Balozi wa Japan Kaziyoshi alisema amefurahishwa sana kutiwa saini kwa mkataba huo kwa kuwa unamkumbusha miaka 70 iliyopita katikati ya vita kuu ya pili ya dunia ambapo Japan ilijikuta katika uharibifu mkubwa pamoja na kubomolewa kwa majengo ya shule.

Alisema katika vita hiyo Japan ilijikuta si tu hawana shule bali hakukuwa na nyumba, maji, umeme hamna chochote kile lakini sasa hivi Japan ni ya tatu kiuchumi.


Discussion between Mr. Kazuyoshi Matsunaga, Chargé d'affaires of the Embassy of Japan, and Hon. Janet Mbene, Deputy Minister of Industry and Trade. From left: Hon. Janet Mbene, Deputy Minister of Industry and Trade, Hon. Rosemary Senyamule, Ileje District Commissioner, Hon. Mohamed Maliyao Mwala, Chairperson of Ileje District Council, Mr. Mussa Otieno, District Executive Director, Mr. Kazuyoshi Matsunaga, Chargé d'affaires of the Embassy of Japan.

MAMA WA MITINDO ASIA IDAROUS KUPAMBA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI ZANZIBAR MACHI 22


..burudani kutolewa na Baby J, Coconut na Zanzibar One Modern taarab

Na Andrew Chale wa Modewji blog

Machi 22 mwaka huu Kisiwa cha Unguja, Zanzibar kinatarajiwa kuwa na tukio moja kubwa litakalowakutanisha Wanawake mbalimbali na kusheherekea siku ya Mwanamke Dunia, ndani ya ukumbi wa Bwawani Hoteli.

Katika tukio hilo, linatarajiwa kuwa pia na shamra shamra ikiwemo za mitindo ya mavazi kutoka kwa gwiji wa mitindo Nchini, Mama Asia Idarous Khamsin atakaye onesha mavazi mbalimbali siku hiyo akiwa sambamba na Mbunifu wa mavazi wa Zanzibar, Matilda Revelian wa Matty Designs.

Sherehe hizo zimeandaliwa na kikundi cha akina mama cha Zanzibalicious Women Group, chenye maendeleo makubwa kwa sasa hapa nchini.


Usiku huo utapambwa na burudani mbalimbali akiwemo mwanamuziki Baby J. Wengine ni bendi ya Coconut na Zanzibar One Modern taarab.

MKURUGENZI WA TIGO JACKSON KISWAGA ATUMIA ZAIDI YA SH MILIONI 10 KUFANIKISHA LIGI SOKA WILAYA YA IRINGA MAARUFU KAMA KISWAGA CUP




Kamu Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Cecile Tiano akikabidi jezi kwa moja ya timu zinazoshiriki ligi ya wilaya ya Iringa (Kiswaga Cup) anayeshuhudiakushoto ni mdhamini wa ligi hiyo Jackson Kiswaga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini. 









Kiswaga akieleza sababu za kufadhili ligi hiyo kwa lengo la kukuza sekta ya mchezo wa soka wilayani Iringa. 





Wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa timu hizo 

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...