WANANCHI wa Manispaa ya Iringa Mkoani humo wametakiwa kutotupa taka ovyo na badala yake wahifadhi taka hizo kwenye vyombo maalumu vya kuwekea taka.
Kauli hiyo imetolewa jana na Meya wa manispaa ya Iringa Alex kimbe wakati akipokea msaada wa mapipa 40 ya kuhifadhia taka kutoka kwa kampuni ya Zanzibar and Nyihita ya mazingira.
Alisema pamoja na kuwa manispaa hiyo imekuwa ikishika nafasi ya kwanza hadi tatu za kuwa safi kitaifa lakini bado kuna baadhi ya wananchi wamekuwa wakitupa taka ovyo,hivyo lazima wahakikishe wanatupa taka kwenye vyombo husika.
Kimbe alisema pamoja na kuwa vyombo vya kutupiataka ni vichache lakini kila mmoja akalichukulia jambo la usafi ni la kwake basi Iringa itaendelea kung’ara kitaifa katika usafi.
“Tunajua manispaa ya iringa imekuwa na uhaba wa vyombo vidogovidogo vya kuhifadhia taka hasa katika maeneo ya stendi na makutano ya barabara ambapo kuna mkusanyiko wa watu wengi lakini tunaendelea kusisitiza watu wahifadhi taka katika vyombo hivyo vichache vilivyokuwepo,”alisema .
Naye kaimu mkurugenzi wa manispaa ya iringa omary mkangama ameishukuru kampuni ya kwa msaada huo na kuahidi kwamba watazitumia dustbin ndogo kwa malengo yaliyokusudia.
Alisema kuwa halmashauri ya manispaa ya iringa ina mpango wa kununua vyombo vya kuhifadhia taka sivyopungua kumi kwa ajiri ya kuwa katika kata ambazo zipo pembezoni mwa manispaa kama vile Nduli, Kitwiru na Isakalilo.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi mtendaji mwingeraza Ismail alisema kuwa kampuni ya Zanzibar and Nyihita co Ltd ni kampuni si serikali inayoshughurikia masuala ya mikopo.
Alisema kuwa kampuni hiyo inafanya kazi kwa ukaribu na jamii kwa kutoa misaada ya mbalimbali katika sekta afya, mazingia na elimu.
Ismail alisema kuwa kampuni hiyo inatoa mikopo mbalimbali kama mikopo ya vikundi, mikopo ya mtu mmoja mmoja na dharura.